Matukio ambayo sitasahau kwenye siasa 2015

Kibosho1

JF-Expert Member
Dec 12, 2017
2,491
3,998
Mwaka 2015 kulikua na vuguvugu kubwa sana la upinzani,yani kifupi ulikua ukivaa nguzo za CCM unazomewa na kila mtu,kijana yeyote alionekana CCM alijihatarisha maisha yake kama atapita mitaani na sare za chama.

Pamoja na hayo kati watangaza nia niliokuwa nawahofia kabisa na alikua tishio ni Edward Ngoyai Lowassa. Huyu mtu aliogopeka Chamani na upinzani pia.

Siku ile jina lake limekatwa tu ilikuwa asubuhi niliingiwa na furaha isiyo kifani mpaka nilishindwa kunywa chai na chakula cha mchana kwa kushangilia. Boss wangu alimpenda sana, furaha yangu moja kwa moja nikajua Dkt Slaa anaenda kuwa rais sababu waliobak wote hakuna wa kupambana nae,kisera, kuishawishi na kiuwezo.

Mara nikasikia Edo anataka kuja CHADEMA,mh!! Kimoyo sikukubali nikaanza kujiuliza "mtu huyu nilikua namkataa akiwa CCM na hata nilitamba akipewa nchi ataiuza" alitembea nchi nzima akigawa pesa kwenye vikundi na nyumba za ibada pesa yake itarudije? Nilinyongonyea sana lakini sikuwa na jinsi sababu anakuja upinzani. Akatangazwa kishingo upande nikakubali hivyo hivyo.

Sitosahau hilo tukio,katika siasa kuna unafiki mkubwa sana, namshukuru Mungu kwa sasa nimeachana nao,sio mwana siasa tena.
 
Tatizo sio unafiki tatizo ni refa. Huyo mchezaji unaesema angeshinda baada ya yule kutolewa(kukatwa), unajidanganya.
 
Nakumbuka kuna baadhi ya wagombea badala ya kusema watasaidia vipi kupitia chama cha wenyewe wakajikita kusema wapinzani wao ni wagonjwa!!!Mwisho wa siku!!!
 
Back
Top Bottom