Halima Mdee na vijana wengine mlio kwenye siasa, kuna maisha nje ya siasa!

Masanja

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
4,819
8,884
Swala la Halima linasikitisha na kufundisha pia. Halima wengi tunamfahamu kama shabiki kindakindaki wa CHADEMA tangu akiwa university nilipomfahamia Mimi.

Wengi tunayafahamu yaliyotokea kwenye uchaguzi 2020. Ni mjingaa pekee anaweza kusema kwamba hawa Covid 19 waliingia bungeni kwa baraka za chama chao. Wenyewe wanajua.

CCM na mashabiki wake wanajua na hata sisi wavuja jasho tunajua. Lakini kwa vile ukweli na reasoning kwenye siasa zetu leo siyo mahala pake, ndo maana leo hii tuna huu mjadala.

Halima amekuwa mbunge for more than 15 years kama sikosei. Mtoto aliyezaliwa anaanza ubunge, kama ni wale familia bora, soon anaitafuta university.

Kabla ya 2020 Halima Aliaminika kwa kujenga hoja na kuangalia maslahi mapana ya taifa. baada ya 2015, lakini zaidi 2020, wote tunajua kilichowapata wana siasa wa Tanzania. Ni somo la wakati mwingine.

Hili saga la Halima liwe fundisho kwa vijana walio active kwenye siasa za Tanzania. Iwe CCM au upinzani. Kuna maisha nje ya siasa. Msiwe career politicians. Msiwe waoga kurudi Mtaani na kujipanga. Chadema imemfanyia mengi Halima.

Asijivue nguo wala Kuharibu mahusiano yake na chadema au wana chadema. Hata wasio wana chadema wanamdharau. Haaminiki. Ukweli si kwamba wana ccm wanampenda. Bali wanamuona kama fursa ya kudeal na chadema. Wakishafanikiwa, watamtosa kama wengine kabla yake. Hawa wanaomuona na kumuita mwanasheria nguli….wamemjua leo? walivyompora ubunge wake kawe hawakujua kama ni mwanasheria nguli?

wanasiasa vijana jitahidini sana kulinda integrity zenu ( kama bado mnazo) Kwa kujitambua. Msikubali kutumika. Mnakoenda ni mbali kuliko mlikotoka. Zaidi huyu Halima ameonja madhira ya siasa za CCM especially chini ya Utawala uliopita. kila kitu kina majira yake. Hata Giza liwe totoro vipi lazima kutakucha tuu.

Kuna wana siasa waliona mwisho wao umefika baada ya 2015. Leo ndo wako high table. kuna wanasiasa kama akina Makonda na Bashiru walijua ufalme wao ndo umeanza na hautakuwa na mwisho..wote tunajua kilichofuata. Kama ilivyo kwenye mambo mengine, kamwe usiweke au kujenga maisha yako kwa kumtegemea mwanadamu.hata vitabu vya dini vimetuasa!

Mwenyezi Mungu anaweza kukujaribu kwa kukupa kila kitu kwa wakati mmoja au kukunyima kila kitu kwa wakati mmoja. Kwa mwenye uelewa yote ni majaribu. Namna unavyokabili hizo nyakati ndo ukomavu na uelewa.
 
Mwenyezi Mungu anaweza kukujaribu kwa kukupa kila kitu kwa wakati mmoja au kukunyima kila kitu kwa wakati mmoja.

Kwa mwenye uelewa yote ni majaribu. Namna unavyokabili hizo nyakati ndo ukomavu na uelewa.
 
Wanasiasa wote wanatumika.

Kina Halima Mdee walipelekwa na Dola ndio iliyowalinda.

Hata Mbowe maamuzi ya kuwafuta uanachama ilibidi akutane na Rais Samia kabla ili wakubaliane.

In short, Wanasiasa wanajuana..

Siku zote, Wafuasi wao ndio wapumbavu.

Ndani ya CHADEMA kila mtu Ni MSALITI MTARAJIWA isipokuwa Mbowe tu.
 
Back
Top Bottom