Mwanakili90
JF-Expert Member
- Nov 24, 2010
- 1,568
- 245
Tafadhali, mtoa hoja uko wapi? Niko Dodoma sema yako wapi? Nikashuhudie na kuondoa kiwingu cha siasa hapa JF
Nimeku inbox fata hayo maelekezo then utafika.
Tafadhali, mtoa hoja uko wapi? Niko Dodoma sema yako wapi? Nikashuhudie na kuondoa kiwingu cha siasa hapa JF
Mimi nipo Dodoma nathibitisha kwamba yapo. Area D barabara ya kwenda Morogoro sehemu inayoitwa Njedengwa. Yapo mengi sana tu.
Kimsingi mpango wa trekta ungeliwezesha taifa sana katika mambo ya uchumi. Lakini ugumu unakuja pale ambapo unalima halafu mipaka ya nchi inafungwa na hawa viwavi jeshi. Hivi ni nani anayetaka hasara. Mimi ninunue trecta huku nikijua kabisa, nachezea shilingi kwenye mdomo wa choo? Haiwezekani hata kidogo.
Wengi tunapenda sana kutumia mashine kwenye kilimo lakini sera za nchi hii ni kama moshi ndani ya tembe siku ya mvua kubwa. Sheria zinazunguka tu, hazieleweki kabisa.
Unajua miaka haifanani, serikali ingekuwa na sera za kuwalinda watu wake, mfano umelima mwaka wa kwanza na umepata hasara. Kimsingi kungekuwa na tathmini na serikali ione ni kwa namna gani inaweza kumsaidia mtu huyu lakini ndo kwanza wanachelea kumpokonya kila kitu. Haya ndiyo matokeo yake. Nakwambia watashusha bei lakini bado yataoza.
Kama ilivyo kawaida serikali yetu huanzisha mipango kabambe ambayo kwa sababu moja au nyingine utekelezaji wake huwa mgumu.Miaka michache iliyopita serikali ilikuja na mpango wa KILIMO KWANZA. Ili kukamilisha azma hiyo power tilers na matrekta yaliagizwa kwa wingi nchini ili wakulima waweze kuyanunua.
Jambo la kusikitisha ni kwamba yale yaliyopelekwa kwenye 'yard' ya Dodoma ni mengi na hayanunuliwi. Kwa sasa yamesongwa na kufunikwa na nyasi ndefu. Inasikitisha, na pengine naweza kusema serikali ilikurupukia mpango huo.
Taarifa imejaa porojo, usanii ni kama imetoka mtaa wa mchikichini karikaoo kwa wauza mitumba.
mliokuwa mnaulizia yapo wapi mmepewa data, nendeni huko mlikoambiwa harafu mje mkanushe hapa. tujue mbivu na mbichi
mliokuwa mnaulizia yapo wapi mmepewa data, nendeni huko mlikoambiwa harafu mje mkanushe hapa. tujue mbivu na mbichi
Angalia mbele, siyo kuweka macho yako utosini!Niko Dodoma ni mji mdogo mbona sijaona matrekta hayo yapo eneo gani la Dodoma na mimi nikajionee sasa hivi kama ni kweli. Nitauliza na wahusika kama nitawakuta