Elections 2010 Matokeo ya mwisho: JK aambulia 61.17%

mh hii mijadala inachosha sasa kila siku ni NEC, TISS, Kova na CLOUDS FM, KIKWETE &Rithwaan, Makamba, SLaa, Chadema , Uchakachuwaji,, POLICE Forces, Shimbo mh. Invisible naomba hii mijadala ufanye mpango mwisho iwe wiki hii
 
Is better we become positive thinkers....CCM kushinda kwa asilimia 64 inaonyesha kukua kwa demokrasia ya vyama vingi....siyo lazima Upinzani ushinde kiti cha Urais ndiyo Uchaguzi uonekane huru na waHaki....afterall, CHADEMA kushinda kiti cha Urais mwaka huu is the last thing I would expect to happen....
 
JK amepoteza umaarufu mkubwa kutokana na kundesha nchi kwa ubabaishaji na kwa kisanii. Mwaka 2005 alipata asilimia 84. Kaporomoka kwa asilimia 20!! Ni anguko kubwa, kwa tafsiri yoyote.
 
DAWA NI WAPINZANI KUTOITAMBUA SERIKALI, WABUNGE WAENDE BUNGENI WAAPE ILI WASIWAACHIE MAFISADI KULA POSHO YAO. KISHA WAHAKIKISHE HAWACHANGII CHOCHOTE MIAKA HIYO MITANO. Ila basi wahakikishe majimboni kwao wanashiriki shughuli za wananchi vilivyo.

Hili lilifanyika kwa Karumeee:smile-big:
 
Is better we become positive thinkers....CCM kushinda kwa asilimia 64 inaonyesha kukua kwa demokrasia ya vyama vingi....siyo lazima Upinzani ushinde kiti cha Urais ndiyo Uchaguzi uonekane huru na waHaki....afterall, CHADEMA kushinda kiti cha Urais mwaka huu is the last thing I would expect to happen....
una element ya ukweli na busara, ila kidogo umechakachua kasehemu... you didnt expect chadema kushinda kiti, neither did i, tatizo ni kwamba baada ya watu kumchoka gafla JK na msomali wake walimtupa JK chini, na kusema ukweli kama sio wizi, angeambulia around 45-50% na chadema 35-45%
 
atapata 61, projection zimefanywa na Synovate, kwa hiyo matokeo yao yalilenga direct hapo maana synovate imefanya kazi kubwa kumuokoa mkuu
 
Angalau nafarijika kuona kuwa walifanya rafu huku wanaona aibu. ningeshangaa sana kusikia huyu Bwana eti kashinda kwa asilimia zaidi ya 80 kama walivyokuwa wanajigamba.
 
JK amepoteza umaarufu mkubwa kutokana na kundesha nchi kwa ubabaishaji na kwa kisanii. Mwaka 2005 alipata asilimia 84. Kaporomoka kwa asilimia 20!! Ni anguko kubwa, kwa tafsiri yoyote.

Hatuna uhakika pia kama hata hizo 84% anazodai kupata mwaka 2005 zilikuwa za haki. Bila usaidizi jamaa alikuwa maji ya shingo mwaka huu.
 
JK amepoteza umaarufu mkubwa kutokana na kundesha nchi kwa ubabaishaji na kwa kisanii. Mwaka 2005 alipata asilimia 84. Kaporomoka kwa asilimia 20!! Ni anguko kubwa, kwa tafsiri yoyote.

Penye red: Wananchi wengi wana hofu kwamba pindi atakapomaliza mwaka 2015, bei ya sukari itakuwa sh 8,000/- kwa kilo. Mwaka 2005 aliikuta sukari ikiuzwa sh 450/- kwa kilo na sasa imefikia karibu 2,000/- kwa kilo.

Hiyo ni sababu mojawapo ya yeye kukataliwa na wengi mwaka huu.
 
Kufuatana na habari katika Nipashe ya leo, matokeo ya mwisho ya urais kwa wagombea wakuu watatu ni kwamba Kikwete kapata kura milion 5.169, Dr Slaa kura milioni 2.193 na Prof Lipumba kura mil 0.649. Kwa mahesabu ya haraka haraka ni kwamba Kikwete kaambulia asilimia 64 ya jumla ya kura za watatu hao na Dr Slaa asilimia 27.3, Lipumba asilimia 8.0. Kama zikijumlishwa na za wagombea wengine, zilizoharibika nk -- asilimia hizo zote zitateremka na huenda JK kwa mfano akaambulia asilimia 61 hivi.

Inawezekana TCIB walikuwa sahihi kidogo?

Na Zawadi Ngoda je? Maana naye takwimu zake zilimpa Kikwete 62%.

KUNA KILA SABABU KWA WOTE WENYE KUTAKA MAKADIRIO MAZURI KWA SIKU ZA MBELE KUMKODI ZAWADI NGODA KUWA FANYIA UCHUNGUZI WA KURA. Timu yangu ni timu ya wataalam wanaoaminika, waliobobea na waliosomea ndani na nje ya nchi. Kumbuka nilandika kuwa CHADEMA itapata wabunge kama 24 na hivyo natarajia ndivyo itavyokuwa mwisho wa mchezo.

Usiposikia la mkuu utavunika guu! Mh Slaa kubali matokeo.
 
Penye red: Wananchi wengi wana hofu kwamba pindi atakapomaliza mwaka 2015, bei ya sukari itakuwa sh 8,000/- kwa kilo. Mwaka 2005 aliikuta sukari ikiuzwa sh 450/- kwa kilo na sasa imefikia karibu 2,000/- kwa kilo.

Hiyo ni sababu mojawapo ya yeye kukataliwa na wengi mwaka huu.
Halafu adha hii itatupata sote haitabagua kwa kuwapendelea waliompa kura.
 
ukimfuata Juha na wewe utakuwa juha tu....... Zawadi Ngoda tabiri basi mwisho wa dunia utakuwa lini.
 
kuna kitu hapa sikielewi hii takwimu yako imenigusa, hivi hawa wanaopokea rushwa za laki tano, laki sita kuiba kura na kuiweka ccm madarakani hizo pesa zitatosha kukidhi mahitaji yao japo bei hiyo ya sukari uliyoweka hapo juu hadi kufikia 2015
 
Kama hivyo ndivyo, basi huenda matokeo yamewakilisha the will of the people. Hii si kusema hakuna fradu bali nikusema fraud haikuzuia matokeo halisi ya kura za watu.
La muhimu watu waanze kufikiria mikakati ya kupambana na ills za serikali ijayo. Pia ni dhahiri Kikwete hatakuwa Kikwete yule wa miaka 5 iliyopita. Mimi haja yangu ni mabadiliko....yafanywe na yeyote yule, kwangu sawa! Ila tutawaadhibu CCM hapo 2015 kutokana na fraud waliyoifanya.
 
Huu si ushindi kwa CCM na Kikwete, maana wao walitaka 80%++. Kutoka asilimia 80 kushuka kuja 65 si ushindi bali ni kushindwa.

PAMOJA na kuchakachua kwa kiasi ambacho hakijapata kutokea hapa nchini, bado wameambulia 65% tu. Hii inakuonyesha kwamba Kikwete alikuwa ameshindwa uchaguzi huu, tena kushindwa kwa aibu.

I'm not sure atakuwa anajisikiaje kukaa pale magogoni huku akijua yeye ni MWIZI tu...just like a common and ordinary thief in Kariakoo
 
ukimfuata Juha na wewe utakuwa juha tu....... Zawadi Ngoda tabiri basi mwisho wa dunia utakuwa lini.

Utabiri unaofanywa na kundi langu si sawa na ule wa Sheikh Yahya Hussein. Utabiri huu unafanywa kwa kuchukua takwimu halisi za wahusika (wapiga kura), ambao wanaweka tiki kwa mgombea mmoja wa urais kati ya wagombea wote. Matokeo hayo ndio huchukuliwa kama ridhaa ya wananchi ukifikiria kuwa kama uchaguzi ungekuwa siku hiyo walipofanya hivyo, basi matokeo yangekuwa hivyo

Tulipofanya ktk mikoa 16, ndio tulipata, Mh Kikwete 62 + -, Mh Slaa 18+ -, Mh Lipumba 15+ -

Wabubge CHADEMA 24 + -

Hivyo nakiri kuwa siwezi kufanya utabiri wa mwisho wa Dunia, kwasababu sina vigezo vya kutumia.
 
Kufuatana na habari katika Nipashe ya leo, matokeo ya mwisho ya urais kwa wagombea wakuu watatu ni kwamba Kikwete kapata kura milion 5.169, Dr Slaa kura milioni 2.193 na Prof Lipumba kura mil 0.649. Kwa mahesabu ya haraka haraka ni kwamba Kikwete kaambulia asilimia 64 ya jumla ya kura za watatu hao na Dr Slaa asilimia 27.3, Lipumba asilimia 8.0. Kama zikijumlishwa na za wagombea wengine, zilizoharibika nk -- asilimia hizo zote zitateremka na huenda JK kwa mfano akaambulia asilimia 61 hivi.

Inawezekana TCIB walikuwa sahihi kidogo?

Bila ubishi kwa ushindi huo twauita ni USHINDI WA KISHINDO WA UCHAGUZI HURU NA WA HAKI, JAPO HAMTAKI KUSIKIA MANENO HAYO MASIKIONI MWENU.
 
PAMOJA na kuchakachua kwa kiasi ambacho hakijapata kutokea hapa nchini, bado wameambulia 65% tu. Hii inakuonyesha kwamba Kikwete alikuwa ameshindwa uchaguzi huu, tena kushindwa kwa aibu.

I'm not sure atakuwa anajisikiaje kukaa pale magogoni huku akijua yeye ni MWIZI tu...just like a common and ordinary thief in Kariakoo

Ulitaka apate asilimia ngapi kama unavyoamini wewe?
 
PAMOJA na kuchakachua kwa kiasi ambacho hakijapata kutokea hapa nchini, bado wameambulia 65% tu. Hii inakuonyesha kwamba Kikwete alikuwa ameshindwa uchaguzi huu, tena kushindwa kwa aibu.

I'm not sure atakuwa anajisikiaje kukaa pale magogoni huku akijua yeye ni MWIZI tu...just like a common and ordinary thief in Kariakoo

EU wameisha sema UCHAGUZI ULIKUWA HURU NA WA HAKI. Na hebu tuambie kura zinaibiwa vp ?
 
Back
Top Bottom