Elections 2010 MATOKEO ya kura za awali CCM August 1, 2010

...Hope ni kweli, maana tulishasema wanyalu sio wajinga kiasi hicho, na hawa wabwege waliokubali hela za wizi ili kumtoa mpiganaji wa wanyonge leo wamepata haki zao ! CCM wakifanya kosa tu la kumuengua, basi upinzani utajichukulia jimbo kiulainii......

Wapi kelele za wale wendawazimu wasiojua hata CV zikoje......???
 
JOHN SHIBUDA ana hali ngumu sana katika jimbo la Maswa. nimepewa taarifa kutoka kwa mmoja wa mawakala, matokeo bado yanaendelea kukusanywa - analalamika kwa kufanyiwa hujuma kubwa sana.

Rejea Tamko lake kuwa "CCM ITAANGUSHWA KWA RUSHWA" aliyoitoa juzi.
 
Breaking newss

sio tu kama Dr Mwakembe kashinda kwa kishindo Kyela pia Madiwani 22 waliokuwa wapo upande wa wanaompinga Dr Mwakyembe wamepoteza nafasi zao,ni diwani mmoja tu wa kata ya Kajunjumele Mzee Mujuni ndiye kaweza kutetea nafasi yake ingawaje alikuwa hasimu wa Mwakyembe,yeye kamuangusha kocha Dan Oscar Koroso ktk uchaguzi mkali sana kupata kutokea kwenye kata hiyo!

Asilimia ngapi kazipata Dr Mwakyembe tunasubiri Afande Samwel au Sikonge wenyewe waje kusema hasa ukizingatia kuwa kuna vituo George Mwakalinga hajapata kura hata moja!
 
Wamekula kwa Mwakalinga wame KURA kwa Mwakyembe

Uko wapi Afande Samwel?

Hii nimeipenda,jamaa alisema,Tz hakuna mabwege tena,yaani kuanzia Kyela hakuna mabwege tena. Mtu akija na hela zake tunalamba halafu kura tunampa tunayemwamini. Majimbo mengi yakifanya hivi siku ya uchaguzi itakuwa poa kweli. CCM siwaamini,wanaweza kupiga tikitaka na tukasikia dr chali.:A S shade:
 
Na wakithubutu kufanya hivyo Nguvu ya wananchi wataiona October 31
 
Maskini 'mh rais ajaye' kaburuzwa. Kama ubunge tu hoi ingekuwaje alipotakaa urais wa inji? Pole jiandae kwa duru ijayo mzee.
 
Wacha apigwe chini,juzi katudanganya kuwa atatoa upinzani kwa jk,mara kachomoa,bora huko wamchomoe kwa kumbwaga asirudi tena mjengoni. Ndio adhabu ya msaliti.
 
CCM siwaamini, wanaweza kupiga tikitaka na tukasikia dr chali.:A S shade:

CCM hawana jeuri hiyo kwa sasa, sana sana utashangaa ukiona CC na NEC inapitisha majina ya "wapiganaji" watakaoshika nafasi ya pili au tatu kabisa.

Zaidi ya wale wanaojipambanua kwamba ni wapiganaji, CCM hakuna ambaye anaweza kufungua mdomo kwamba anapambana na ufisadi japo hata hao wapiganaji wanapambana kisanii. Kikwete hawezi kukubali ku-risk apunguze kura nyingi kwa kuwatema maana hao ndio watamuokoa na atawatumia kama mtaji kujibu hoja za ufisadi.
 
I salute u Mkuu....you have read the game well
 
mnafikiri ajui atavuna alichopanda
ukipanda bangi utavuna bangi asubiri matokeo ya mdomo wake
 
Huwa hatuna HARAKA na habari kama hizi. Ukweli ukifahamika, nitakuja hapa KUMPA HONGERA MSHINDI.

Haya ni mashindano tu na Demokrasia inataka mmoja ashinde na wengine washindwe. Kama mtu alifikiri nitataka Mwakalinga ashinde kwa NGUVU basi anafanya makosa makubwa sana kwani mie siyo Dictator. Kama Mwakalinga kashinda, HONGERA ZAKE na kama Mwakyembe kashinda basi HONGERA ZAKE. Kama Mwanjala kashinda pia HONGERA ZAKE.

LIFE GOES ON. Asiyekubali kushindwa si MSHINDANI. Ila siamini kuwa Mwakalinga amekuwa wa TATU.
 
Back
Top Bottom