Matokeo ya Kilimo kwanza bila Viwanda na hasara za wakulima.

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
Wana JF,

Nguvu nyingi zilizotumika kuutangazia umma mikakakati ya kilimo kwanza nia ilikuwa mzuri lakini anayefaidika zaidi ni mlaji wa kawaida ambaye anakaa mjini, huku kwa wakulima hali ni mbaya sana baada ya kuchukua mikopo mikubwa kuanzisha kilimo, kuitikia sera ya ccm, kwa sasa kuna mkwamo kwani chakula ni kingi masoko kidogo, hata sehemu ya kuhifadhia hakuna, hii ni kutokana na kukosa viwanda vya serikali vya kusindika mazao, pia kukosa madawa ya kutunzia vyakula hivi, Mchele sasa ni kilo hadi tshs 1300 kwa kilo kutoka shinyanga, mbeya tshs 1500 ,ukija kwenye nyana sabdo ilikuwa 5000 sasa 2300 imefikia sasa buguruni na kariakoo watu wanakosa soko wanazikimbia nyanya zao, hivi kweli hakuna kiwanda cha kuprocess zikapakiwa kwenye makopo? njoo sasa kwenye vokado, yani hapa ni hasara kwa kwenda mbele, kwa sasa serikali inamtegemea MO na Bahresa ndiye anayesaidia wakulima kununua mazao yao. Kuna kilimo cha Alizeti, serikali imeacha mafuta mengi kutoka uarabuni yakiingizwa nchini , huku alizeti ikikosa soko,

Wanasema kuanzisha kilimo cha ukumbozi katika mikoa ya kanda ya ziwa kuwakomboa wananchi baada ya zao la biashara kama kahawa, ndizi, mihogo kuharibika, lakini hakuna juhudi za makusudi kuwa udongo wa kanda ya ziwa unategemea sana mbolea ya mifugo, mifugo yote ilikufa kwa kukosa madawa, kuna majosho kibao, yameanza kuibiwa vyuma na kuviuza kama chuma chakavu. siku hizi hakuna sehemu ya zizi la pamoja ambalo linatumika kunyunyuzia dawa mifugo, hii hali imewafanya watu wa kanda ya ziwa kuichukia serikali yao , kwa kuwa imewaacha kwenye lindi la umaskini.
 
Back
Top Bottom