Matokeo ya kidato cha pili 2021 shule haziko 'Alphabetically'

HOPEfull

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
1,642
1,977
Hii inaitwa pambana na hali yako. Kuna shule naitafuta toka juzi siioni. Sasa kwa upangaji huu labda inaonekana hayana umuhimu sana na watu hawana mpango nayo.

Sidhani kama watu wote wanatumia vifaa 'advance' vya kuweza kuwasaidia kupata kitu anachokitaka kwa haraka.

Sijui tunakwama wapi.
 
Acha uzembe , bonyeza 'find on page' kisha type jina la shule fastaa tu linakuja.
 
Tafuta found on page utachekwa kutafuta ni rahisi zaidi.Kuliko yaliyo pangwa kwa alfabeti.
 
Ingia kwenye website kawaida yakishafunguka bonyeza vile vidoti vitatu juu kulia kisha itakuja menu fulani, shuka ubonyeze kwenye Find in page utakuja uwanja wa kuandika sms , andika jina la shule utakuja ukurasa wenye hilo jina na hilo jina litakuwa na rangi tofauti na mengine, bonyeza pale. Imeisha hiyo.
 
Hiyo found on page ipo na kwetu watumiaji wa Tecno? mm siioni kabisaa!!!
Kinachokupa option ya kufind siyo simu ila ni software/ app unayoitumia.

Hua nasema Tz tumekuta tech iko mbele na tumeirukia. Hivi ni vitu vidogo sana ambavyo kila aliyefika angalau kidato cha kwanza anatakiwa kujua
 
Ingia kwenye website kawaida yakishafunguka bonyeza vile vidoti vitatu juu kulia kisha itakuja menu fulani, shuka ubonyeze kwenye Find in page utakuja uwanja wa kuandika sms , andika jina la shule utakuja ukurasa wenye hilo jina na hilo jina litakuwa na rangi tofauti na mengine, bonyeza pale. Imeisha hiyo.
Haya ngoja nijaribu
 
Nimepata mkubwa. Shukrani umeniongezea maarifa.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom