MATOKEO ya Kidato cha Nne a mjadala wa kuboresha Kufaulu

Seminari wanasimamia misingi ya nidhamu, maadili na uwezo wa kitaaluma. Wastani wa kuvuka kuingia darasa lingine ni hamsini jini ya hapo huna chako hata ule wastani wa serikali wa form two hawaujali ukichemka wastani wao wanakutimua. Kila mwezi wanafanya monthly test. Pia wanazingatia muda wa kusoma taa zote zinazimwa sa nne usiku na hakuna anayeruhusiwa kusoma zaidi ya hapo labda kwa kujificha. Zaidi ya hapo wako wachache darasani hivyo inakua rahisi kuwa administer. Ukiwa mtukutu wanakutimua bila kujali una uwezo gani darasani ndio maana wengi wanaotimuliwa seminari wakienda shule nyingine za private wanaendelea kuongoza labda na huko wanafanya udanganyifu...
 

Thanks Mkuu
Hii inatakiwa tuiweke kama New Post
 
nakubali, lkn kwan ini high view walishtuka, walipanga mkakati? huku seminary hakufanyiki mkakati kama huo?

Mkulu
Heshima mbele, huko shule ya High view NECTA walistuka kwa sababu shule hiyo ilikuwepo kwa muda mrefu na ghafla ikatoa matokeo hayo unayosema kwamba ni mazuri mno.

Shule nyingi za seminari performance yake ni mzuri from the start.Ingawa binafsi sikubali kuwa hizo ni shule bora kwa sababu minimum requirements i.e alama wanazoweka ili mwanafunzi apate admission ni za juu sana , hivyo matokeo yake ni kwamba by default wanachagua wanafunzi ambao ni wenye uwezo wa juu sana.

Mwanafunzi kama huyo haitaji kufundishwa sana na mwalimu ili afanya vizuri kwa sababu tayari anamsingi mzuri wa kielimu.

Shule hizi hata style ya ufundishaji wake siyo kama sekondari nyingine ni kama vyuo fulani hivi, wanafunzi wanapewa references zakusoma then assignments inatolewa , lastly kipindi kinachofuata they sit for discussions on areas ambazo zinahitaji ufafanuzi zaidi.

Binafsi naamini shule nzuri ni ile ambayo mwanafunzi anapokelewa akiwa na alama 30 , then walimu wanaanzia hapo, mtihani unaofuata anapata 40 , then 60 kadri siku zinavyokwenda mwanafunzi ana-improve gradually kitaaluma

Hata hivyo nawapongeza viongozi,wafanyakazi,walimu na wanafunzi wa shule za seminari, ijapokuwa sizioni kama ni shule za kumjenga mtoto asiye na uwezo mkubwa gradually , ambao ni watoto wetu hao,wao wanataka wale walio na uwezo tayari.

kwa muktadha huo, hizo siyo shule.
 
wapi naweza kupata matrix moja yenye matokeo yote?
mi nadhani pia kuweka kumi bora kwa shule zaidi ya 3000 ni usumbufu tu, bora kuweka shule 50 au 20 bora na vile vile kwa zile za chini
 

mi nakubaliana na wewe,ila natoa angalizo kwamba duniani hamna anayempenda kilaza. Hata timu za mpira duniani zinachuja kutafuta best wachezaji ndo wanapewa mikataba,kuajiriwa kuna vigezo pia,mf.work experience,skillr level,serikali yenyewe ya tz form1,form5 hata chuo usipopata minimum qualifications huwezi enda huko. Hapa minimum inabaki kuwa subjective,how minimum is that minimum?
 
nakubali, lkn kwan ini high view walishtuka, walipanga mkakati? huku seminary hakufanyiki mkakati kama huo?

Madrasa zinawa-confuse watoto!! Wanajifunza kuandika kwenda kulia na kwenda kushoto wakati mmoja!! Wakristo wanajifunza kuandika kwenda kulia tu. Watoto wasipelekwe madrasa wakiwa wadogo.
 

mi nakubaliana na wewe,ila natoa angalizo kwamba duniani hamna anayempenda kilaza. Hata timu za mpira duniani zinachuja kutafuta best wachezaji ndo wanapewa mikataba,kuajiriwa kuna vigezo pia,mf.work experience,skillr level,serikali yenyewe ya tz form1,form5 hata chuo usipopata minimum qualifications huwezi enda huko. Hapa minimum inabaki kuwa subjective,how minimum is that minimum? Upande mwingine elimu ni malezi tu. Angalia mf. St.Ignasius Loyola high school ya majesuit reg.S0800 Loyola. Hapa wanafunzi wote karibia 140 wamepita fom4 na wote wanaweza kuendelea na f5. Hapa kuna waislam na wakristo kwa ujumla japo ni shule ya Majesuit,yani Watu wa Yesu,hamna ubaguzi. Ikumbukwe pia mwaka jana ndo loyola iliyopata Udsm best student,SALOME MARO. Hapa tuache udini shule zote zinajiweza. Waislam wasiogope kukalia dawati,achana na ushauri wa Muhogomchungu.
 
Ukweli unabaki pale pale kuwa bado tuna kazi kubwa ya kuzifanya shule zetu nyinginezo kama za islamic na za kata ziweze kufaulisha kama zilivyo shule za seminary za kikristo,inasikitisha na kuzidi kuweka chuki baina ya watoto na mwishowe ianatengeneza tabaka na kuonekana kuna watu fulani wanapendelewa katika shughuli fulani za kijamii hapo baadae wakati hali halisi tunaiona sasa
 
hakuna mxzazi mwenye uwezio anaye weza kumpeleka mwanae kwenye hizi shule so solition ni serikali kutatua hili tatizo na wala hii sio solution..wazazi ambao hawana uwezo ndio wapo wengi nchini

Na hao hao ndio wapiga kura wazuri kwa CCM kwa kisingizio cha kulinda amani tuliyorithishwa na Baba wa Taifa. Acha wakome; maana wanavuna walichopanda.
 

Kukazia hoja yako hata wanaozijenga Dubai, Saudi Arabia etc .....ambazo ni nchi za Kiislam damu ni watu kutoka nje ....wahindi kwa wingi wakisaidia na wataalaam wa kizungu. Indigenous Arabs unawakuta very few kwenye game. Hii inaashiria kuna tatizo sehemu fulani na ni kazi yako kulitafuta.
 
Jaman nasikitika sana. Iyo shule ya kwanza ni shule au wanachama waliamua pia majina yawepo necta. Hapa muhogomchungu ndo adhihirishe aliyoyasema kwenye thread zake kuwa seminari wanaiba pepa. Pia wizara ichunguze sifa za walimu wao,isije kuwa sifa ni imamu,ustadh tu,kwa kwa nini wote wafaulu kiislam tu na vpindi vingne puu! Inauma sana.
 
Isije ikaishia kukuuma tu........... hayo maumivu unayoyapata uya-TRANSLATE kwenye kurekebisha yafuatayo...........
1. walimu wanaofundisha shule hizo............. haiwezekani wanafunzi wabadirike kila mwaka na matokea yanabaki yale yale kila mwaka..............
2. Majengo
3. Kinachofundishwa.
4. etc..etc
 

Cha kushangaza hao waliofaulu vizuri kwa viwango vya juu wanaanza kuomba hivyo vyuo ulivyoviita vya kata na sio hivyo vya seminari - kama ilivyo shule za seminari. Mwisho wa siku elimu ya juu - Chuo Kikuu ni tofauti na elimu ya sekondari au msingi. Hivyo elimu ya juu vyuo vya serikali ni nzuri kuliko private universities, ndo maana hao waliomaliza kwa alama za juu - whether wamemaliza public or private schools, when joining wana-disco mwaka wa kwanza. Jiulize elimu waliyopata huko Seminari au shule za serikali ilikuwaje? Jibu ni simple haikuwaandaa kuwa varsity students.
 


ACHA HADITHI MKUU..UNASEMA UMEFANYA RESEARCH HAYA ATTACH HIZO CORRESPONDENCE ZAKO WEWE NA WIZARA NA VODA AND ZANTEL... nadhani ujumbe umefika kwa wahusika wengine tuona vitu hivi...
 

Nadhani Ujumbe Umefika kwa Wahusika next time Tender nadhani tutaziona kwenye Magazeti! Mission Accoumplished.
 

Sasa mbona umesema yote bana, sisi wengine tutasema nini?

seriously, badala ya watu kutafuta mchawi, wapeleke watendaji wa wizara kujifunza kwenye seminary setu jinsi mazingira, nidhamu, na upatikanaji wa vifaa na chakula unavyoweza kukuza uwezo wa mtoto kujifunza.

Nakumbuka mara ya kwanza nilipoona kwanafunzi anavyoibia mtihani (baada ya kuwa nimetoka seminary) pale UDSM. Nilijisikia kama nimekaa karibu na mwanaume shoga? Ninamaanisha it was something so unethical and which i had never seen in my life.
 
Shule za kata ni gharama kwa taifa!!!!!!!!fidia yake sidhani kama tutaweza kulipa.
hatutaweza kulipa,
itaandikwa kwenye historia ya Tanzania MILELE, ndio kumbukumbu NA URITHI ambayo kizazi hiki imeamua kukiachia kizazi kijacho!!!!! UJINGA

 
Na mimi ninakubaliana na hilo ni kweli kuna mchujo mkubwa sana katika shule hizo za seminari.Kwa mfano enzi za miaka ya 80s st Anthony ilikuwa bila ya wastani wa 50 kwa kila somo huwezi kuingia darasa linalofuata na pia kulikuwa na motisha ya kulipa nusu ada iwapo utapata wastani wa 65 na kuendelea.ukipata wastani wa 80 na kuendelea hutalipa ada kabisa.Hii ilisababisha watu wasome kwa bidii sana,na hii haikuangalia anayepata alama za juu ni dini gani na kuna ushahidi kwamba kuna hata waislam waliopata msamaha wa ada kwa kupata alama za juu.
Na hii ilikuwa hata kw ashule zingine kama Msola.Ila kwa sasa sina uhakika kama bado hii system bado inatumiwa na st Anthony but that is what i know na kwa wakati huo na kuna shule kama Mzizima nayo haikuwa na lele mama kwenye wastani na walikuwa wanafanya vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…