Matokeo ya Bunge la Afrika Mashariki: Saba washinda, Mnyaa safi, Wagombea wa CHADEMA waangukia pua

Mara nyingi kwa sheria na kanuni kama hizi nimekuwa nikiona zikitumika. Akiwa mgombea hana mpinzani straight hutangazwa yeye kuwa mshindi bila kupingwa. Sasa nafasi ni mbili wagombea ni wawili si ni dhahili kuwa wamepita bila kupingwa?
 
Mara nyingi kwa sheria na kanuni kama hizi nimekuwa nikiona zikitumika. Akiwa mgombea hana mpinzani straight hutangazwa yeye kuwa mshindi bila kupingwa. Sasa nafasi ni mbili wagombea ni wawili si ni dhahili kuwa wamepita bila kupingwa?
KWA HIYO Mnataka bunge litumIke kama rubber stamp???oo
 
Nilicheka Mbowe alipoulizwa wafanywe nini akasema wapigiwe kura ya ndio, yeye mwenyewe alijicheka! Kwa muono yangu hata wakipigiwa kura za sio zote , wao ni wabunge automatically! Kura za sio hazibatilishi qualification zao bali kuonesha dissatisfaction ya wabunge wa CCM. Hongera technical team ya Chadema na UKAWA kwa ujumla.

Wanakuwa wabunge automatically? Hii si kweli kabisa. Kwa hiyo bungeni wameenda kufanya nini sasa?
 
Mara nyingi kwa sheria na kanuni kama hizi nimekuwa nikiona zikitumika. Akiwa mgombea hana mpinzani straight hutangazwa yeye kuwa mshindi bila kupingwa. Sasa nafasi ni mbili wagombea ni wawili si ni dhahili kuwa wamepita bila kupingwa?
Spika amesema hakuna kitu kama hicho, lazima kura zipigwe aidha kwa mdomo au kwa karatasi.. Kama wakishapitishwa na vyama vyao ndo tayari basi haina maana ya Bunge kukutana na kupiga kura
 
Ni bora wabgekubali Ile ya (Ndiyo au Siyo) Halafu wakati wa kuitikia wakawazimia Mic upande wa CCM kama walivyokuwa wakiwafanyia wakati wa kuchangia hoja...
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Kuna ambao hawajaelewa mantiki ya kipengele cha kwanza

Sheria inataka nchi mwanachama kupeleka wabunge (kwa idadi waliyopewa ambayo kwa Tanzania ni wabunge 9) ambapo kati yao, theluthi iwe uwakilishi wa wanawake.
Kwa nchi yetu vyama vimegawiwa nafasi za uwakilishi kulingana na idadi yao bungeni. Sasa ili kuipata hiyo theluthi KILA CHAMA KIWE NA MGOMBEA WA JINSIA KE.... Ili kwenye hao wanawake, WAWEZESHE kuifikia ile theluthi. Haimaanishi kuangalia kama CCM imeweka wanawake ndio waje kuhesabiwa kama 1/3. Kama CCM wangeleta wanaume pekee yao, je ninkwa namna gani 1/3 ingepatikana?
Kama ambavyo upinzani wanaona ugumu KUCHANGIA wanawake ndivyo na CCM wanavyofeel. Hata hao waliowaweka wanatamani WASIWEPO na ndivyo hali ilivyo, sasa sheria inawabana, na kikombe hiki kila mtu akinywe mpaka wakabadilishe sheria!

Wengi wamehoji kwenye viti viwili 1/3 ni nini?
Someni muelewe...
Imeandikwa..... ILI KUWEZESHA UTEKELEZAJI WA SHERIA.....
Haimaanishi kila chama kilete 1/3 bali kila chama KIWEZESHE utekelezaji wa sheria ya 1/3 kwa kuweka wanawake. Wenye viti vichache wao wanaweza kujikuta wakileta wanawake pekee mfano CUF au nusu (CHADEMA)....
Hili linaweza kuwafanya wajisikie kuwa wamepunjwa au wameweka kiasi kikubwa cha wanawake, lakini ndio njia pekee ya KUWEZESHA utekelezaji wa sheria hii.

Sasa kama hamleti wanawake mnawezeshaje matakwa hayo ya kisheria? HUWEZI KUWEZESHA BILA KUCHANGIA

Ni wapi au sheria ipi imesema kuwa wenye viti vingi (CCM kwa sasa) ndio wanapaswa kuwa na wanawake ili sheria hiyo itekelezeke? Ni hivi, kama vyama vya upinzani haviwezi kuweka wanawake, wasifikiri ccm ndio wenye kulazimika kuleta wanawake. Na ndio kusema wanaikataa hiyo kanuni ya 1/3

IELEWEKE
Kuhusu Theluthi ya wanawake, HAIMAANISHI KILA CHAMA KIWE NA 1/3 Bali kila chama KICHANGIE wanawake ili kupatikana hiyo theluthi kwa idadi yote. Na kwa scenario yetu idadi ya wanawake inaweza kuzidi theluthi, na kuzidi si dhambi kwa kuwa sheria inasema ANGALAO na haifungi wakiongezeka, kwa hiyo jambo sio kutafuta mahesabu ya 1/3 ya 9 ni kiasi gani, bali kutazama uwezeshaji wa vyama kufikia hiyo ANGALAO mbapo inaweza kuzidi..
One-third of the elected members should reflect either gender.Ni ngumu kuielewa hii?Wangeleta wanawake watupu ndo wangekuwa wametimizaje sasa hiyo kanuni.Muwe mnasoma na kuelewa vitu kabla hamjajigeuza walimu
 
Siasa za Tanzania hazina tija yoyote sasa kuna tofauti gani na kuahirisha uchaguzi,maana wabunge walipendekeza kutokana na mgongano uchaguzi usogezwe ili wajipange lakini AG akashauri zege isilale.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Yaani unategemea uwe mpinzani wa CCM halafu wakupigie kura? Au Upinzani wanaweza kuwapigia kura CCM? Unalowaza haliwezi kutokea isipokuwa tu, siasa za wanaogombea zikiwa ni siasa zisizo na takataka ambazo angalau zina apreciate pale mpinzani anapofanya vyema na kukosoa pale panapostahili... Angalia ACT unaweza kuelewa.... tatizo siasa za Kitanzania ni chafu sana, ukwia upinzani hujengi hoja, umaarufu wako ni kumtukana au kumkashifu mpinzani mwenzako... Mauaji ya Kimbarii na ubaguzi vilianza hivyo hivyo kwa siasa za kijinga na ndio maana hakuna kupigiana kura...
Upinzani wanaweza kupiga kura kwa CCM,ukiangalia matokeo ya Dr Maghembe utagundua amepata kura kwa pande zote.Jamaa yuko vizuri atasaidia sana hata alivyokuwa anajieleza mimi nikasema huyu lazima awe mwakilishi
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Kweli hivi watu na akili zao wanaacha kumchagua Twaha Taslima kutuwakilisha bunge LA Afrika Mashariki na kumchagua Mnyaa kwa vile wanamkomoa Maalim Seif? Hivi hapo kakomolewa Seif au Tanzania?
Wanapiga kura za hapana kwa Masha na Wenje wakati watu wabishi na makini kama hao ndio tunawataka kwenda kupambana na Wakenya na Wanyarwanda? Kweli naona maneno ya Makonda kuhusu Bunge letu in ya kweli kabisa. Watu hawana utaifa wala umakini bali ushabiki wa kijinga pekee.
Acha Kenya na Uganda wawe wanatukebehi in sawa tuu kama wawakilishi wenyewe ndio hawa.
 
Kwa hiyo sababu bunge la Uingereza wanapiga kelele kama masokwe basi na sisi tuige kwa kuwa ni Waingereza wanafanya hivyo basi nenda beach kaogelee na mama yako mkiwa mumevaa chupi pamoja na dada zako kwa kuwa hizo ndio tabia za Waingereza nawe iga.
Sheria za mabunge ya jumuia ya madola zinafanana hivyo hata tabia lazima ziendane. Hiyo ya kwenda beach niwaige kwa kanuni IPI?
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Tukivuta kumbukumbu tutaona ni jinsi gani chadema imewahi kulalamikiwa sana na wanachama wake pamoja na jammii juu ya teuzi zakke zisizo na demokrasia. Tujikumbushe baadhi tu ya teuzi zake zilizolalamikiwa kutofuata misingi ya demokrasia................ Uteuzi wa lowassa kuwa mgombea urais kupitia chadema. Uteuzi wa mwenyekiti wa chama bilakupigiwa kura au kutoa fursa ya wanachama wengine kuomba nafasi hiyo. Uteuzi wa wabunge wa viti maalum ambapo wengi wao walisemekana ni ndugu au wake wa viongozi. Uteuzi wa viongozi wa kanda mbalimbali za kichama. Hivi karibuni uteuzi wa wagombea wa EalA. Hiii inamaanisha kuwa ndani ya chadema kuna udikteta na kutofuatwa kwa kanuni na misingi ya kidemokrasia. Kama demokrasia ingefuatwa nisingetegemea kumuona mtu kama Masha ambaye ni mwanachama mpya kabisa akiwazidi wavuja jasho ndani ya chadema kwa miaka zaidi ya 20 wakikosa japo fursa tu ya kugombea nafasi hiyo ndani ya chama. Zaidi.......Ni hawa hawa chadema wanaolilia siku zote kuwa bunge haliwezi kufanywa muhuri....leo hiii wanalitega bunge na kutaka kulitumia kama ngazi ya kutokkea shimoni waliponasia.polleni wanachadema lakini bunge limetumia haki yake kuwarudishia akili iliyowapotea yaani akili ya ,kuhoji maamuzi ya mwenyekiti na kuachana na hulka ya yule mnyama aitwaye.........anayepatika serengeti na masaimara.............kabla sijamaliza nakumbushwa hapa kuwa hata katibu wenu mlipata kwa figisufigisu na sio kidemokrasia ndio maana hawezi kufuata lolote zaidi ya takwa la mwenyekiti........Ciao kwa leo . nnn n mimi jingalao ni,iwasaidia bavicha
 
Kweli hili linashangaza sana, wabunge wetu wanaacha watu makini, kweli mizuka na chuki ndo zinawamaliza wabunge wetu. Hapa kilichokuwa kinatakiwa ni Utanzania kwanza mengine ya siasa baadae. Wanautani sana na tz yang juu ya EAC.
 
Back
Top Bottom