Matokeo ya Bunge la Afrika Mashariki: Saba washinda, Mnyaa safi, Wagombea wa CHADEMA waangukia pua

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,189
2,970


Habari waungwana,

Leo unafanyika uchaguzi wa wabunge watakaotuwakilisha kwenye bunge la Afrika Mashariki lakini kabla ya hapo watajinadi kwa wabunge wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Mapema uliibuka mjadala mzito baada bunge kupokea majina kutoka kwa CUF A na CUF B.

MATOKEO YA UCHAGUZI WA WABUNGE WA AFRIKA MASHARIKI


KUNDI A: WANAWAKE

1. Ndg. Happiness Elias LUGIKO - KE - CCM - KURA 196

2. Ndg. Fancy Haji NKUHI - KE - CCM - KURA 197

3. Ndg. Happiness Ngoti MGALULA - KE - CCM - KURA 125

4. Ndg. Zainabu Rashidi Mfaume KAWAWA - KE - CCM - KURA 137

KUNDI B: ZANZIBAR

1. Ndg. Abdullah Hasnu MAKAME ME CCM - KURA 254

2. Ndg. Maryam Ussi YAHYA KE CCM - KURA 195

3. Ndg. Mohamed Yusuf NUH ME CCM - KURA 65

4. Ndg. Rabia Hamid MOHAMEDI KE CCM - KURA 142

KUNDI C: VYAMA VYA UPINZANI

CHADEMA

1. Ndg. Ezekia Dibogo WENJE - ME - CHADEMA - KURA ZA NDIYO 124 HAPANA 174

2. Ndg. Lawrence Kego MASHA - ME - CHADEMA - KURA ZA NDIO 126 HAPANA 198

CUF

1. Ndg. Habibu Mohamed MNYAA - ME - CUF KURA 188

2. Ndg. Sonia Jumaa MAGOGO - KE - CUF KURA 06

3. Ndg. Thomas D.C MALIMA - ME - CUF- ALIJIONDOA

4. Ndg. Twaha Issa TASLIMA - ME - CUF KURA 140

KUNDI D: TANZANIA BARA

1.Ndg. Adam Omai KIMBISA - ME - CCM 266

2. Ndg. Anamringi Issay MACHA - ME - CCM 23

3. Ndg. Charles Makongoro NYERERE - ME - CCM 81

4. Dkt. Ngwaru Jumanne MAGHEMBE - ME - CCM 287

Wabunge saba ndio wamechaguliwa na nafasi mbili za CHADEMA bado zipo wazi.

WALIOSHINDA NI;

1. Fancy Haji Nkuhi

2. Happiness Elias Lugiko

3. Abdallah Hasnu Makame

4. Maryam Ussi Yahya

5. Habibu Mohamed Mnyaa

6. Ngwaru Jumanne Magembe

7. Adam Omary Kimbisa
 
Kama chama kimoja kinaweza kuleta majina ya wagombea walioidhinishwa na makundi mawili tofauti ndani ya chama kimoja(factions) na wote wakawa halali na chombo cha kutunga sheria nacho kikaona kila kitu kiko sawa na hivyo ni halali kuendelea na uchaguzi,ni wazi nchi haina haja ya kuwa na katiba wala sheria bali tuongozwe na kauli na mitazamo ya watu wachache waliopewa dhamana.

Hivi kweli katibu wa Bunge anatamka kutambua CUF A na CUF B ndani ya chombo cha kutunga sheria na wabunge wakaridhika kupokea majina wa wagombe kutoka CUF A na CUF B?

CUF A na CUF B vyama hivi vimesajiliwa wapi na lini vilipata usajili wa kudumu?

Ni wazi tumebaki na mhimili mmoja tu unaonekana kuheshimu sheria na katiba ya nchi na hata swala hiki likipelekwa mahakamani ninahaki uchaguzi wote huu unaweza kutangaza kuwa ni null and void bila kujali tatizo ni la wagombe wa chama kimoja tu maana huenda mchakato mzima ukawa umeingia najisi.

Hii ni nchi ya ajabu sana.
 
Back
Top Bottom