Matokeo niliyoyaona jana usiku Simba SC 🆚 Rs Berkane

Kekule Wa Benzene Ring

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2019
Posts
277
Reaction score
1,178
Jana mnamo saa Nane Usiku niliota ndoto ya Matokeo ya fainali kombe la shirikisho Afrika mkondo wa pili kati ya SIMBA SC ya TANZANIA dhidi ya RS BERKANE kutoka Morocco.

Mechi ilianza Kwa Kasi sana na Simba mnamo dk ya 15 walipata mkwaju wa penalty na Steven Mukwala akaweza kukwamisha mpira kambani.

Dk ya 42 Simba wakapata Goli Tena Kupitia ELI MPANZU baada ya kupewa pasi ya mwisho na Jean Charles AHOUA.

Kipindi cha pili RS BERKANE walipata Goli dk ya 68 na kuufanya mchezo Kuwa 2-1 Lakini Goli lilikataliwa na VAR Kuwa kulikuwa na foul kabla ya goli

Dk ya 88 Simba wakapata Goli na kuua Mechi Kupitia Fabrice Luamba Ngoma.

FT: SIMBA 3 🆚 RS BERKANE 0
 
Jana mnamo saa Nane Usiku niliota ndoto ya Matokeo ya fainali kombe la shirikisho Afrika mkondo wa pili kati ya SIMBA SC ya TANZANIA dhidi ya RS BERKANE kutoka Morocco.

Mechi ilianza Kwa Kasi sana na Simba mnamo dk ya 15 walipata mkwaju wa penalty na Steven Mukwala akaweza kukwamisha mpira kambani.

Dk ya 42 Simba wakapata Goli Tena Kupitia ELI MPANZU baada ya kupewa pasi ya mwisho na Jean Charles AHOUA.

Kipindi cha pili RS BERKANE walipata Goli dk ya 68 na kuufanya mchezo Kuwa 2-1.

Dk ya 88 Simba wakapata Goli na kuua Mechi Kupitia Fabrice Luamba Ngoma.

FT: SIMBA 3 🆚 RS BERKANE 1
Bado haikutosha simba kubeba kombe
 
Hayo ni kwenye ndoto tu Mkuu, usijaribu kuyapa uzito ukidhani yanawezekana maana utaumia zaidi mambo yatakapokuwa vice versa (na ndivyo itakavyokuwa)

Simba kumfunga Berkane ni kwenye ndoto pekee.
 
ndoto zina mambo inaweza vilevile ikawa kinyume.unaweza kuota ndoto lakin ukashindwa kuftasiri
 
Hayo ni kwenye ndoto tu Mkuu, usijaribu kuyapa uzito ukidhani yanawezekana maana utaumia zaidi mambo yatakapokuwa vice versa (na ndivyo itakavyokuwa)

Simba kumfunga Berkane ni kwenye ndoto pekee.
Kwa nini iwe kwenye ndoto na wewe umejuaje kama na wewe pia haupo ndotoni ? Thibitisha kwa hoja tatu.
 
Back
Top Bottom