VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Kikao cha kupitisha Viwango Vipya vya Ufaulu vilivyotumika kwa Kidato cha Nne kilihusisha Wizara ya Elimu na Ufundi,NECTA na TCU. Nyaraka za kikao hicho kilichofanyika Disemba mwaka jana,zinaonesha kuwa kikao husika kilikuwa chini ya Uenyekiti wa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dr.Shukuru Kawambwa na Katibu wa Kikao alikuwa Naibu wake Bwana Phillipo Mulugo.
Kwa upande wa NECTA,waliwasilishwa na Mwenyekiti wake Prof.Rwekaza Mukandala na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo,Dr.Joyce Ndalichako.Pia alikuwepo Mjumbe kutoka Mamlaka ya Vyuo Vikuu nchini-TCU ambaye alikuwa ni Prof. Sifuni Ernest Mchome (ambaye baadaye akawa Mwenyekiti wa Tume ya Kuchunguza Ufaulu wa Kidato cha Nne!)
Kikao hicho kiliidhinisha kutumika kwa viwango hivyo vipyakwa kidato cha nne na cha sita. Wajumbe wote wa Mkutano walikubaliana na viwango vipya na matumizi yake kwa kidato cha nne 2012.
Habari zaidi zimeripotiwa katika Mwananchi la leo
Je, kuchunguza na kutaka kubadili matokeo haya si dharau zilizopitiliza kwa watanzania? Je, ni halali kwa Prof.Mchome kuhudhuria kikao na halafu kuongoza Tume ya Kuchunguza? Watanzania tumedharauliwa,sasa tuchukue hatua gani? Nani mtanzania muungwana atawaamini watu hawa kwasasa?