UZUSHI Matiti ya mwanamke huanguka yanapoguswa guswa na viganja vya wanaume

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Kuna mwanamama aliwahi nipa ushuhuda kuwa matiti yake yalianza kuanguka akiwa na miaka 23 kutokana na mitomaso aliyokuwa anafanyiwa na mpenzi wake wa kwanza. Aliendelea kwa kusema kuwa, kabla ya kuanza michezo na wanaume alikuwa na chuchu dodo zilizosimama na kuchoma.

IMG_6646.jpeg

Hivi ni kweli kuwa matiti ya mwanamke yanapopapaswa na viganja vya mwanaume hupelekea kuanguka na kuwa ndala?
 
Tunachokijua
Binadamu kama walivyo wanyama wengine wanaopatikana kwenye Kundi la Mamalia huwa na sifa mbalimbali zinazowatenganisha na viumbe wengine. Baadhi yake ni;
  • Kuwa na manyoya
  • Kuwa na tezi za jasho
  • Huwa na tezi maalum za kuzalisha maziwa, maarufu kama mammary glands
  • Huwa na mifupa 3 kwenye sikio la kati
  • Uwepo wa eneo la Neocortex kwenye ubongo
  • Kuwa na meno yaliyotofautishwa muundo na muonekano
  • Moyo wenye vyumba 4 pia chembe nyekundu za damu zisizo na kiini (Nucleus) katikati
Kwa kurejea sifa hizi, mwanamke kama kiumbe kinachonyonyesha huwa na tezi kubwa zaidi za maziwa (Matiti) kuliko wanaume, pia huwa na homoni nyingi zaidi zinazosaidia uzalishwaji wa maziwa kuliko zile alizonazo mwanamme.

Kuanguka baada ya kushikwa na wanaume
JamiiForums imepokea madai haya na kufanyia kazi kwa kuzungumza na wataalam wa afya. Katika uchunguzi wetu, tumebaini mambo yafuatayo;
  1. Ukuaji wa matiti ya mwanamke huongozwa na mfumo wa taarifa za urithi (Genes) pamoja na mfumo wa vichocheo vya mwili (Homoni)
  2. Hakuna mfumo mmoja wa ukuaji wa matiti unaofanana kwa wasichana wote. Baadhi hukua mapema na baadhi huchelewa
  3. Kushikwa matiti na wanaume hakuwezi kusababisha kudondoka (kuanguka) kwa matiti, au hata kuongezeka ukubwa wake.
Ukiondoa Genes na Homoni, mambo mengine kama uzee, kani ya mvutano wa dunia (Gravity), uzito mkubwa, umri wa ukomo wa hedhi, kuzaa watoto wengi, kupoteza sana uzito wa mwili pamoja na uvutaji wa sigara husababisha kudondoka kwa matiti.

Pia, kwa mujibu wa Taasisi ya Nemours Teens Health, kuvaa au kutokuvaa sidiria hakuwezi kusababisha kukua, kudumaa au kudondoka (kuanguka) kwa matiti. Nadharia hizi ni uzushi usio na uhalisia kisayansi.
Kuna wanaojiuza lakin chuchu bado imesimama kama kamaliza darasa la saba mwaka huu hao unawaweka kind gan kwenye utafit wako
Ni kweli mkuu hata mimi naunga hoja kushikwa sio sababu matiti hukua kutokana na maumbile ya mwanamke , mbona wapo wanaoshikwa na wamechezea dyudyu mpaka basi lkn kifuani bado dede?

Ukiwasikiliza wao watakuambia kwamba kukua kwa matiti inatokana na maumbile na hata ukoo pia maana wapo hadi walio zalishwa lkn bado saa sita
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom