Hello JF! Kwa anayejua shule inayohitaji mwalimu wa hesabu, O level na hata A level anipe mchongo. Shule ikiwa Dar, itakuwa vizuri zaidi, lakini hata mikoani si neno.
ANGALIZO:
Sijasomea ualimu, nimesoma Bachelor of Science in Mathematics (Bsc. Maths), na nimeshafundisha shule tatu mpaka sasa.
Licha ya kutosomea ualimu, napenda kufundisha. Hiyo kozi yenyewe niliyosoma (Bsc. Maths), niliichagua nikijua ni kozi ya ualimu (kuwa mwanakijiji wa kwanza kusoma chuo ni shughuli), nilipofika chuoni, ndipo nikajua siyo ualimu.
Lakini haiba ya ualimu nimeshaipata kwa kukaa na walimu (si unajua tena, ukikaa kwenye waridi utanukia uaridi).
Kwa kutambua wanaohitaji nafasi hiyo ni wengi, nafasi hiyo itupie hapa hapa kwenye uzi, ili watakaotaka kupeleka maombi, wapeleke.
Natanguliza shukrani. Ndimi
Graph Theory