maramia
JF-Expert Member
- Jul 17, 2015
- 2,030
- 1,345
Ama kweli sikio la kufa halisikii dawa! Sikutegemea kwa jinsi CCM ilivyobanwa mbavu kwenye uchaguzi wa mwaka jana kama ingetoa mwanya kwa Ukawa kung'aa tena katika siasa za Tanzania. Nilitegemea ingejisahihisha na kwa hiyo kuzivunja kabisa nguvu za akina Chadema na Ukawa.
Lakini mwendo wa utawala wa Magufuli ilioanza nao ni wa kuiweka serikali mbali na wananchi wale wale waliyoiweka madarakani.
Kwa mfano, sidhani kama vyama vya upinzani vitashindwa kuitumia mianya iliyoachwa wazi na serikali ili kujijenga na kujiimarisha kisiasa.
Naamini kwamba vitendo vya kuwabomolea wananchi nyumba zao katika hali ya unyama uliopindukia ubinadamu, sitisho la TBC kuwaonyesha live wananchi mijadala ya wabunge wao na ubakaji wa ushindi wa CUF na demokrasia huko Zanzibar vitawaimarisha sana kisiasa wapinzani na watarejea kwenye chati ambayo niliisha kata tamaa kama ingeweza kuwarejerea tena ndani ya muda mfupi huu.