Matembezi ya amani kutunisha mfuko wa M4C

Habari za asubuhi list inaendelea kuongezeka tunakaribia watu 25.mpaka sasa kiongozi yoyote wa chama hajapita hapa ombi langu wenye nia ya kweli kufanikisha hili jambo tupeleke makao makuu halafu tuone kama watalichukulia hatua zaidi.
 
Katika mtandao wa twitter mpaka sasa tumepata wapambanaji 20 amabao wako tayari kushiriki.

Mapambano yanaendelea
 
Ni kweli kuwa Watanzania walio wengi ni maskini sana lakini ili kuondokana na umaskini ni lazima maskini waunganishe nguvu zao kwa kuchanga kidogo kidogo ili kuwa na uwezo wa kuwaondoa mafisadi wachache wenye hela wanaotumia nguvu zao za kifedha na dola. Mafisadi wana pesa nyingi lakini wana mioyo na vichwa vichache, maskini wana hela kidogo, wana uzalendo, wana mioyo na vichwa vingi, wanahitaji nguvu ndogo tu ya hela ili kuwashinda mafisadi matajiri wachache wa CCM wanaowatumia maskini dhaifu wenye upeo duni ili kuendelea kutawala na kuiba.

Chadema kila siku mnasema Watanzania wana hali mbaya kiuchumi hawana pesa halafu leo tena mnataka kuwachangisha mabilioni.
 
Hakuna haja ya Invisible, kutag members wa JF kwa masuala ya Chadema, JF sio mali ya Chadema fanyeni hiyo kazi nyie Pro-Chadema JF.

Unahangaika sana....take a break, or join Kinana in his famous trips of shame to wana CCM.
 
Last edited by a moderator:
Tunafikia watu karibu 50 sasa napenda kutoa taarifa huu ni mchakato kama mambo yakienda vizuri makao makuu wakaukubali ticket zitaanza kuuzwa kuanzia january kwa ajili ya hayo matembezi no za simu muhimu ili upewe taarifa mbalimbali wapi pa kuja kuchukua ticket yako.
 
Da mipango mizuri!

nitaungana pamoja nanyi wana wa dar kwa harakati hizi za ukombozi mimi niko chuo iringa nitachangia pesa kiasi cha elfu ishirini na nitashiriki matembezi hayo kama yatafanyika mwez huo wa tatu kwani tutakuwa likizo.wazo zuri sana na hii ni dalili ya kwenda ikulu
 
nitaungana pamoja nanyi wana wa dar kwa harakati hizi za ukombozi mimi niko chuo iringa nitachangia pesa kiasi cha elfu ishirini na nitashiriki matembezi hayo kama yatafanyika mwez huo wa tatu kwani tutakuwa likizo.wazo zuri sana na hii ni dalili ya kwenda ikulu

Karibu sana mkuu ungetupatia no yako ili ticket zikianza kutoka kupeane taarifa
 
Unahangaika sana....take a break, or join Kinana in his famous trips of shame to wana CCM.

Mie tena naangaika? Nyie ndio mnaangaika kila sehemu mnataka kuchangia pesa njoo home uchukuwe mchango.
 
KAMANDA!!!

usihofu mchango wangu LIVE...Makao makuu CHADEMA ARUSHA.....before 22 December 2012!!!
 
Fred

Hongera kwa wazo zuri, ingawa bado linahitaji maboresho ya hapa na pale, but generally hongera sana kwa kutimiza wajibu wako kwa kuhakikisha CHADEMA na mapambano kwa ujumla yanatimiza lengo la kutoa utumishi bora kwa umma, lengo ambalo ili litimie, historia ya nchi hii inapaswa kuongezwa kurasa kadhaa zitakazosema kuwa CCM kiliwahi kutawala mwaka fulani mpaka mwaka fulani...

Kutokana na majukumu kadhaa yaliyonibana kwelikweli sikuwahi ku comment mapema ingawa niliona kilichoandikwa mapema sana na kufuatilia mjadala baadae kwa kina. Kwa ajili ya kuangalia tunasonga namna gani mbele, hasa kwa ku-incorporate wazo hili katika plans zinazofanana na hiki kitu ili sasa viwe under same umbrella kwa ajili ya efficiency na effectiveness, nitaku PM wewe na wengine ambao nimefuatilia mchango wao hata kama ni kwa kuweka alama ya 'like', hata wale waliopinga au kuponda pia.

Lakini pia ili kurahisisha mambo, fanya hivi 0688 595831, hata kama ni usiku wa manane.

Tutalizungusha hili gurudumu na kulifikisha tunakofikiria na kuona kwenye ndoto zetu mchana na usiku, iwapo tu kila mmoja wetu atatimiza wajibu wake kama ulivyofanya Kamanda Fred na kama wanavyofanya wengine kwa namna mbalimbali, ikiwemo critiques and constructive criticism.

Kila mmoja wetu anacho cha kuchangia katika mapambano haya na mchango wa kila mmoja wetu utathminiwa kadri inavyotakiwa, kama si leo basi kesho au keshokutwa kwenye kurasa za historia ambayo inaendelea kuandikwa kila kila sekunde inayopita. Baadae nitaweza kujadili kwa kina baadhi ya mambo ambayo si lazima sana kupelekeana PM.
 
Back
Top Bottom