Matembezi ya amani kutunisha mfuko wa M4C

Bwana mdogo una mawazo mazuri,lakini hizo fedha hazitafikia malengo!Zitatumika kulipia mshahara wa Slaa na Mshumbuzi,pamoja na posho zao za kila siku!Pia baadhi ya hizo fedha anaweza kutumia mwenyekiti wetu kama nauli kufatilia maendeleo ya miradi yake Dubai.

Any way ucaha ngishe kwa ajili ya Hujenzi wa Hospitali au Shule.Ni mtazamo tu!

Ndo maana tumeomba matumizi ya vile fedha za kwanza zilipatika ni sh ngapi na zilitumikaje kama watashindwa kuonyesha matumizi mazuri nadhani kutakua hakuna haja
 
Chadema mnasema mnaitaji bilioni 3 Mwanza, lakini hawasemi matumizi yake...wapeni wananchi mchanganuo wa matumizi ya michango ya mwanzo.
 
Naona mkuu Ritz umeamua kumsaidia Invisible kujibu baadhi ya mapendekezo anayoombwa kuyafanya!

Sijui ni msukumo wa upendo au woga ndo umekutuma kuingilia majukum yasiyokua ya kwako!!
Binafsi nadhani ni woga.

Majukumu gani mkuu? hivi kwa akili yako unadhani JF ni mali ya Chadema?
 
Chadema mnasema mnaitaji bilioni 3 Mwanza, lakini hawasemi matumizi yake...wapeni wananchi mchanganuo wa matumizi ya michango ya mwanzo.

Ritz una jambo la msingi sana matumizi ya mwanzo ni muhimu
 
Shukurani kwa wakuu wote baadaye nitaongezea majina ya walikubali.

Pamoja tunaweza changia kubadilisha hii nchi
 
Shukurani wakuu tumefika watu zaidi ya 10 sasa endeleni kuhamasisha wengine tungefurahi kupata majina na no za simu iwe rahisi kukutafuta

Mkuu watu 5000 watapatikana tu wala haina shida cha msingi kama wewe umeamua kulibeba jambo hili usiliache njiani hakikisha limefika mwisho wake na mafanikio yake umeyaona na historia ya nchi hii itakukupumbuka kwa mchango wako wa kuleta mabadiliko yenye kuleta tumaini jipya la watoto wetu!

Mimi nashuri ushirikiane na uongozi wa chadema muunde kamati ya maandalizi ya haya matembezi ili ianze kuratibu.

Mimi niko tayari kutumia kiasi cha kipato changu kuchangia hizi harakati za mabadiliko zitakazo leta matumaini mapya kwa watoto wetu!

Chadema iko miyoni hivyo wala usihangaike kuchukua namba za simu tutatoa na kushiriki pia ili mradi yawe ni matembezi ya amani maana chadema ni chama cha amani sana!
Mkuu mie nitachangia zaidi ya 50k.
 
For the record kwa jina naitwa fred kavishe wengi mnaweza msinijue.miaka 22.elimu bado nasoma.twende kwenye hoja moja kwa moja.

Jana nilitoa hoja wakati nachangia topic ya mzee mwanakijiji kuhusu m4c hoja yangu ilikua kuhusu matembezi ya amani kutunisha mfumko wa m4c inawezekana kabisa wengi hamkuona wengi mliisoma na kunipa like kuonesha kuikubali kuna wachache waliniambia wako tayari kwa matembezi na mmoja akaniambia atatoa 50000 lakini hatakuja kwenye matembezi.

Kwa kifupi lengo la haya matembezi itakuwa kuleta awareness kwa wananchi kujua lengo la m4c na madhumuni yetu.pia kukitangaza chama kwa njia nyingine.sasa mikutano mingi ya harambee imekua ikifanyika kwenye kumbi za ndani na kurushwa live kwenye tv na imekua ikichukua watu wa tabaka fulani lengo la haya matembezi ni kushirikisha kila mwananchi kuweza kuchangia haya mabadiliko chama kiweze kufika kwenye ngome ngumu kupenya.

Nikapendekeza tena tufanye haya matembezi mwezi wa 3 kwahiyo ina maana chama tukipe mwezi mmoja kituandalie ticketi,risiti na mfumo mzuri jinsi itakavyokua kuanzia mwezi wa kwanza tuanze kuzinunua hizo ticket na pia ingependeza kama wote tungekua kwenye sare za tshirt labda viongozi ndo wawe na combat.

Lengo la kiurudisha hii hoja hapa tena leo ni kuanza mchakato rasmi nitamuomba mkuu tumain makene aje aendeleze hii mada wale wanajf watakao kuwa tayari kwa matembezi haya mwezi watatu tutaanza kuchukua majina yenu na no zenu za simu kwa masiliano zaidi na ratiba zaidi.

Lengo la matembezi haya ni kukusanya bilioni 1-2 kwa ukanda huu wa dar es salaam mikoa mingine inawaza iga sasa tutafanyaje kuweza kupata hizo pesa.nilipendekeza ili kushiriki haya matembezi unaweza nunua ticket kwa sh 20000 tunahitaji watu sio chini 5000 ambapo mpaka hapo tutakua tumefikia lengo la 1 bilion.

Ni rahisi sana kujiwekea hii 20000 hata kwa sisi wanafunzi,wananchi wa kawaida kuna siku zaidi ya 90 zakujiandaa unaweza kujiwekea 200 ili ushiriki haya matembezi ya kutunisha mfuko wa m4c.

Lakini kama tutapata watu zaidi ya 5000 itapendeza zaidi na siku ya matembezi tutafungia pale jangwani wengine wanaweza kuongozea kiasi chao pale pale uwanjani harambee nyingine itaendelea.

Kutakua na misafara mbalimbali nikapendekeza pia mfano jimbo la ubungo tunaongozwa na mnyika si mbaya akaongoza msafara kutoka kimara mpaka eneo la jangwani,jimbo la kawe na mdee aongoze msafara hadi jangwani na wananchi wengine watakao changa hizo pesa.

Ieleweke tu kiwango cha chini kushiriki haya matembezi ni 20000 lakini unaweza toa zaidi kama wana jf mmoja alaiye nihaidi atatoa 50000 lakini hatashiriki sijui anaogopa nini.

Kwahiyo unaweza changia uwezavyo kushiriki haya matembezi naomba niseme mchakato utakua huru sana kwa wachangiaji ningekiomba chama kituandalie risiti ukilipa 20000 unapewa risiti na ticket ya kushiriki matembezi.

Unaweza ukawa hata nje ukavutia na haya matembezi ukatoa kiasi chochote cha pesa kwa uwezo wako upendavyo.

Matembezi haya yaendae na uzinduzi wa radio.
Tumekua tunatumia gharama kubwa kulipia airtime kwenye vituo vya radio na tv ili movement zetu zirushwe najua kwa sasa wazo la tv linahitaji pesa nyingi sana lakini hatushindwi kuanzisha radio.

Sasa radio inazinduliwa rasmi siku ya matembezi yetu ya amani kutununisha mfumko wa m4c nitawapa umuhimu mmoja tukipata radio yetu inakua rahisi sana kuna software moja inaitwa ozeki msg server hii ina control utumaji wa msg na upokeaji wa msg.

Mfano siku ya uzinduzi wa radio tukiwa na huu mtando vijana wetu wa IT wakipewa wataweza kutengeneza pesa kwa chama mfano kesho asubuhi mnyika atahojiwa chadema radio kwahiyo wale wenye maswali maoni wanaweza kutuma kwa njia ya msg kila msg inatozwa 500 labda 100 wanachukua mtandao wa simu 400 kichukue chama labda zikatumwa msg 1000 tushatengeza zaidi ya milioni 4.je kwa mwaka tunaweza tengeneza sh ngapi?

Faida nyingine ya hii software kipindi cha uchaguzi tunaweza wasiliana na wanachama wetu wote kwamba watatupigia kura kwa kuwatumia msg za kuwapa moyo na kutorudi nyuma kulinda shahada zao na kulinda kura.

Shime wana chadema tutafute huu mtambo utakifanya chama kianze kujitegemea taratibu na kuacha utaratibu wa kutembeza bakuli kwa wananchi.

Kwa kumalizia namuomba tumain makene aje hapa achukue majina ya wana jf ambao watakua tayari kushiriki matembezi haya hatuwezi waachia kila kitu mbowe,slaa,mnyika,zitto wafanye sisi kama wanachadema tunaweza hamasishana na kuita viongozi wetu mwisho wa shughuli kupendezesha matembezi.

Faida ya matembezi
1:kutunisha mfuko wa m4C
2:kukitangaza chama
3:kuonyesha dunia tuko tayari kukiweka chadema ikulu 2015
4:kuvutia watu wengi wajiunge na chama

Zoezi naomba lianze sasa kukusanya majina ya washiriki wote tutoke nyuma ya keyboard mapambano yaanze rasmi.

Majina ya wana jf walikubali hoja
1.Gambas-50000 tsh
2.Aristides kasigwa-30000
3.Kurunzi
4.3squere
5.Dudus
6.Msenyela
7.Swrc
8.Ruttashobolwa
9.Magessi
10.Mr busta
11.Malunde
12.Cacico
13.Curriculum specialist
14.Matola
15.Okwi boban sunzu
16.Kajungu

Fred kavishe

big up mkuu. Naunga hoja na nitashiriki matembezi
 


Big Excellent!!... Kitaalamu inaitwa
Creativity….ukipenda itamke VISION .... KAMANDA NAKUPA MIA!! MAGAMBANI NI KITU ADIMU!!! Kazi yao kuiga na kuwatumia POLISI!!!
 
Pro-Chadema JF mna vituko sana mnashindwa kuchangia JF mtachangia Chadema kweli.
 
Wazo nzuri sana na mimi nitashiriki, lakini ujue itakuja ile tafsiri ya maandamano na uanaharakati ambao CCM wamekuwa wakiufanyia propaganda siku zote!

Kumsikiliza ccm ni sawa na mkristo kumsikiliza shetani.Hivyo ccm haimtakii mtu mema. Sisi inatupasa kusonga mbele.
 
Kwa wanachama wote wa CHADEMA, naomba tuungane katika kulifikisha jambo hili ambalo ni jema mno katika MATAWI yetu tuliyonayo ili tupime mwitikio wake pia.
 
Pro-Chadema JF mna vituko sana mnashindwa kuchangia JF mtachangia Chadema kweli.
Pimbi wewe unadhani kila anayechangia JF anahitaji hizo title za JF Gold Member au Tanzanite Member? Ur mentality slave.
 
Back
Top Bottom