Matembezi ya amani kutunisha mfuko wa M4C

FredKavishe

Verified Member
Joined
Dec 4, 2010
Messages
1,090
Points
1,195

FredKavishe

Verified Member
Joined Dec 4, 2010
1,090 1,195
For the record kwa jina naitwa fred kavishe wengi mnaweza msinijue.miaka 22.elimu bado nasoma.twende kwenye hoja moja kwa moja.

Jana nilitoa hoja wakati nachangia topic ya mzee mwanakijiji kuhusu m4c hoja yangu ilikua kuhusu matembezi ya amani kutunisha mfumko wa m4c inawezekana kabisa wengi hamkuona wengi mliisoma na kunipa like kuonesha kuikubali kuna wachache waliniambia wako tayari kwa matembezi na mmoja akaniambia atatoa 50000 lakini hatakuja kwenye matembezi.

Kwa kifupi lengo la haya matembezi itakuwa kuleta awareness kwa wananchi kujua lengo la m4c na madhumuni yetu.pia kukitangaza chama kwa njia nyingine.sasa mikutano mingi ya harambee imekua ikifanyika kwenye kumbi za ndani na kurushwa live kwenye tv na imekua ikichukua watu wa tabaka fulani lengo la haya matembezi ni kushirikisha kila mwananchi kuweza kuchangia haya mabadiliko chama kiweze kufika kwenye ngome ngumu kupenya.

Nikapendekeza tena tufanye haya matembezi mwezi wa 3 kwahiyo ina maana chama tukipe mwezi mmoja kituandalie ticketi,risiti na mfumo mzuri jinsi itakavyokua kuanzia mwezi wa kwanza tuanze kuzinunua hizo ticket na pia ingependeza kama wote tungekua kwenye sare za tshirt labda viongozi ndo wawe na combat.

Lengo la kiurudisha hii hoja hapa tena leo ni kuanza mchakato rasmi nitamuomba mkuu tumain makene aje aendeleze hii mada wale wanajf watakao kuwa tayari kwa matembezi haya mwezi watatu tutaanza kuchukua majina yenu na no zenu za simu kwa masiliano zaidi na ratiba zaidi.

Lengo la matembezi haya ni kukusanya bilioni 1-2 kwa ukanda huu wa dar es salaam mikoa mingine inawaza iga sasa tutafanyaje kuweza kupata hizo pesa.nilipendekeza ili kushiriki haya matembezi unaweza nunua ticket kwa sh 20000 tunahitaji watu sio chini 5000 ambapo mpaka hapo tutakua tumefikia lengo la 1 bilion.

Ni rahisi sana kujiwekea hii 20000 hata kwa sisi wanafunzi,wananchi wa kawaida kuna siku zaidi ya 90 zakujiandaa unaweza kujiwekea 200 ili ushiriki haya matembezi ya kutunisha mfuko wa m4c.

Lakini kama tutapata watu zaidi ya 5000 itapendeza zaidi na siku ya matembezi tutafungia pale jangwani wengine wanaweza kuongozea kiasi chao pale pale uwanjani harambee nyingine itaendelea.

Kutakua na misafara mbalimbali nikapendekeza pia mfano jimbo la ubungo tunaongozwa na mnyika si mbaya akaongoza msafara kutoka kimara mpaka eneo la jangwani,jimbo la kawe na mdee aongoze msafara hadi jangwani na wananchi wengine watakao changa hizo pesa.

Ieleweke tu kiwango cha chini kushiriki haya matembezi ni 20000 lakini unaweza toa zaidi kama wana jf mmoja alaiye nihaidi atatoa 50000 lakini hatashiriki sijui anaogopa nini.

Kwahiyo unaweza changia uwezavyo kushiriki haya matembezi naomba niseme mchakato utakua huru sana kwa wachangiaji ningekiomba chama kituandalie risiti ukilipa 20000 unapewa risiti na ticket ya kushiriki matembezi.

Unaweza ukawa hata nje ukavutia na haya matembezi ukatoa kiasi chochote cha pesa kwa uwezo wako upendavyo.

Matembezi haya yaendae na uzinduzi wa radio.
Tumekua tunatumia gharama kubwa kulipia airtime kwenye vituo vya radio na tv ili movement zetu zirushwe najua kwa sasa wazo la tv linahitaji pesa nyingi sana lakini hatushindwi kuanzisha radio.

Sasa radio inazinduliwa rasmi siku ya matembezi yetu ya amani kutununisha mfumko wa m4c nitawapa umuhimu mmoja tukipata radio yetu inakua rahisi sana kuna software moja inaitwa ozeki msg server hii ina control utumaji wa msg na upokeaji wa msg.

Mfano siku ya uzinduzi wa radio tukiwa na huu mtando vijana wetu wa IT wakipewa wataweza kutengeneza pesa kwa chama mfano kesho asubuhi mnyika atahojiwa chadema radio kwahiyo wale wenye maswali maoni wanaweza kutuma kwa njia ya msg kila msg inatozwa 500 labda 100 wanachukua mtandao wa simu 400 kichukue chama labda zikatumwa msg 1000 tushatengeza zaidi ya milioni 4.je kwa mwaka tunaweza tengeneza sh ngapi?

Faida nyingine ya hii software kipindi cha uchaguzi tunaweza wasiliana na wanachama wetu wote kwamba watatupigia kura kwa kuwatumia msg za kuwapa moyo na kutorudi nyuma kulinda shahada zao na kulinda kura.

Shime wana chadema tutafute huu mtambo utakifanya chama kianze kujitegemea taratibu na kuacha utaratibu wa kutembeza bakuli kwa wananchi.

Kwa kumalizia namuomba tumain makene aje hapa achukue majina ya wana jf ambao watakua tayari kushiriki matembezi haya hatuwezi waachia kila kitu mbowe,slaa,mnyika,zitto wafanye sisi kama wanachadema tunaweza hamasishana na kuita viongozi wetu mwisho wa shughuli kupendezesha matembezi.

Faida ya matembezi
1:kutunisha mfuko wa m4C
2:kukitangaza chama
3:kuonyesha dunia tuko tayari kukiweka chadema ikulu 2015
4:kuvutia watu wengi wajiunge na chama

Zoezi naomba lianze sasa kukusanya majina ya washiriki wote tutoke nyuma ya keyboard mapambano yaanze rasmi.

Majina ya wana jf walikubali hoja
1.Gambas-50000 tsh
2.Aristides kasigwa-30000
3.Kurunzi
4.3squere
5.Dudus
6.Msenyela
7.Swrc
8.Ruttashobolwa
9.Magessi
10.Mr busta
11.Malunde
12.Cacico
13.Curriculum specialist
14.Matola
15.Okwi boban sunzu
16.Kajungu
17.Earthmover-100000
18.Sisimizi
19.Hakikwanza
20.Kanewi-20000
21.Magesi-20000
22.Yoweli-20000
23.Greenwich-20000
24.Bams

Fred kavishe
 

Matola

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2010
Messages
40,138
Points
2,000

Matola

JF-Expert Member
Joined Oct 18, 2010
40,138 2,000
Invisible tunakuomba uwatag wana JF hii thread bila kujari kwamba ni wa chama gani ili Member wengi zaidi ujumbe huu uwafikie. Nafahamu wako wana CCM wengi tu wanapenda kuchangia harakati za kuleta mabadiliko, maana wengine watoto wao ndio kwanza wapo Darasa la kwanza, wanajuwa fika Elimu bure inawezekana.
 
Last edited by a moderator:

Msenyele

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2012
Messages
334
Points
195

Msenyele

JF-Expert Member
Joined Feb 7, 2012
334 195
kjana una umri mdogo ila mawazo yako ni mazuri,hata mimi nilifiliria cdm tungekuwa na vyombo vya habari ingekuwa rahisi zaid kwa chama kujulikana hasa ikiwa na uwezo wa kurusha matangazo hadi vijijini ambako wengi wao pengne sio rahis kuktambua chama na ndo chanzo pekee cha kupata habari kwan ndio wanamudu kununua kuliko tv na magazeti. pia hlo likifanikiwa uwepo mpango wa kuanzisha kituo cha television ili magamba wawe na nafasi ya kujionea madudu yao.
 

kajunju

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2011
Messages
1,001
Points
1,250

kajunju

JF-Expert Member
Joined Jun 30, 2011
1,001 1,250
Wazo zuri kavishe,nafikiri baada ya kuanza harambee za ukumbini.hii ni next step ya kwako.viongozi wameona mwitikio wa wananchi wenye uwezo. Sisi walala hoi tunaweza anza changia mia 2,3, had elfu moja na pesa zitapatikana. Wazo lako nimelipenda
 

Ritz

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2011
Messages
42,258
Points
2,000

Ritz

JF-Expert Member
Joined Jan 1, 2011
42,258 2,000
Chadema kila siku mnasema Watanzania wana hali mbaya kiuchumi hawana pesa halafu leo tena mnataka kuwachangisha mabilioni.
 

Ritz

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2011
Messages
42,258
Points
2,000

Ritz

JF-Expert Member
Joined Jan 1, 2011
42,258 2,000
Invisible tunakuomba uwatag wana JF hii thread bila kujari kwamba ni wa chama gani ili Member wengi zaidi ujumbe huu uwafikie. Nafahamu wako wana CCM wengi tu wanapenda kuchangia harakati za kuleta mabadiliko, maana wengine watoto wao ndio kwanza wapo Darasa la kwanza, wanajuwa fika Elimu bure inawezekana.
Hakuna haja ya Invisible, kutag members wa JF kwa masuala ya Chadema, JF sio mali ya Chadema fanyeni hiyo kazi nyie Pro-Chadema JF.
 
Last edited by a moderator:

FredKavishe

Verified Member
Joined
Dec 4, 2010
Messages
1,090
Points
1,195

FredKavishe

Verified Member
Joined Dec 4, 2010
1,090 1,195
Nashukuru sana modes kwa kurudisha bandiko langu lisamame peke yake mpaka sasa tushapata watu 5 tunaendelea kupokea watu ambao watakua tayari kushiriki haya matembezi majino yao na no zao na kiasi watakacho toa.
 

FredKavishe

Verified Member
Joined
Dec 4, 2010
Messages
1,090
Points
1,195

FredKavishe

Verified Member
Joined Dec 4, 2010
1,090 1,195
Wazo zuri kavishe,nafikiri baada ya kuanza harambee za ukumbini.hii ni next step ya kwako.viongozi wameona mwitikio wa wananchi wenye uwezo. Sisi walala hoi tunaweza anza changia mia 2,3, had elfu moja na pesa zitapatikana. Wazo lako nimelipenda
Shukurani sana mkuu karibu kwa matembezi
 

Forum statistics

Threads 1,392,767
Members 528,684
Posts 34,117,601
Top