BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,832
- 287,782
Posted Date::11/23/2007
Matatizo ya Tanesco, serikali yatupiwa lawama
Ramadhan Semtawa na Patricia Kimelemeta
Mwananchi
UAMUZI wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kuomba kupandisha viwango vya matumizi ya umeme umepingwa vikali na wadau mbalimbali huku wakisema 'mchawi' wa shirika hilo ni serikali kwa kuingia mikataba mibovu ndani ya shirika hilo.
Licha ya kueleza bayana kwamba mchawi wa shirika ni serikali, pia wamekosoa mishahara ya watumishi kuongezeka kila mara huku makusanyo ya shirika ikiwemo madeni yakizidi kuporomoka mwaka hadi mwaka.
Tanesco imeomba kuongeza gharama za huduma za kwa asilimia 40 na za kuunganisha kwa kati ya asilimia 196 na 280.
Maoni ya wananchi hao kupinga mpango huo wa Tanesco, yametolewa jijijini Dar es Salaam jana katika mkutano wa wadau ulioandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) kujadili mapendekezo ya shirika hilo.
Kwa upande wake, Christina Kilundu, akitoa maoni yake, alihoji ongezeko la gharama za uendeshaji na mishahara ya wafanyakazi kuwa juu huku makusanyo ya madeni yakishuka.
Kilundu ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa CTI, alisema takwimu zinaonyesha kuwa kila mwaka kumekuwa na ongezeko la fedha za kulipa mishahara ya watumishi wa shirika na kutaka liangaliwe kwa makini.
Kwa upande wake mwananchi mwingine, Renatus Mkinga, alisema miundombinu yote ya kuzalisha umeme imejengwa tangu enzi za serikali ya awamu ya kwanza chini ya Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere, lakini viongozi wa sasa wameleta makampuni mizigo kama Richmond/Dowans na IPTL.
Mkinga alisema makampuni hayo ni mizigo kwa shirika hivyo haiwezekani gharama hizo zibebwe na wananchi bali serikali yenyewe badala ya kuwadanganya wananchi kuwa kuna mvua kutoka Thailand kitu ambacho hakipo.
"Hivi nyie mkoje, mabwawa yote ya kuzalisha umeme sijui Kidatu, Mtera, yote haya kajenga Nyerere, nyinyi mnaleta mambo ya Richmond, Dowans, sasa mikataba hii mibovu mnataka hasara yake ibebwe na wananchi," alisema Mkinga na kuacha ukumbi mzima kuzizima kwa kicheko.
Mkinga alisema shirika hilo limeshindwa kukusanya madeni yake ambayo ni mabilioni ya shilingi, ambayo sehemu kubwa yanadaiwa katika taasisi za serikali.
Alihoji na kutaka kufahamu deni la Zanzibar ambalo Tanesco inadai kama tayari limelipwa.
"Madeni hayalipwi na wadaiwa wakubwa ni serikali, tuambieni deni la Zanzibar limeishia wapi, limelipwa?" alihoji.
"Kuiba muibe ninyi halafu sisi mtubebeshe madeni, wizi wa nyaya za umeme unafanyika, kama watu wanaweza kununua Satelite kuangalia usalama kwanini msiweke teknolojia ambayo mtu akiiba waya tu anakufa papo hapo," alisisitiza.
Kwa upande wake mwananchi mwingine aliyejitambulisha kama mwakilishi wa taasisi ya familia ya mzee Gwao, (jina kamili Mujengi Gwao), alisema hivi sasa Tanesco inataka kutupa hasara yake kwa wananchi akahoji vipi serikali ikwepe jukumu hilo.
Gwao alisema wananchi hawawezi kubeba hasara ya Tanesco kwani tayari hivi sasa kila kitu kimekuwa ghali, ikiwemo kodi za nyumba, huduma za elimu na afya na bidhaa nyingine na kuongeza kwamba hata madafu yamepanda bei.
Baraza la Ushauri la Serikali, katika tamko lake limesema uamuzi huo wa Tanesco kutaka kuongeza gharama hizo unathibitisha halikutekeleza kikamilifu agizo la Ewura la Januari 10, mwaka huu.
Akisoma tamko hilo la baraza hilo, Mkurugenzi wa baraza hilo Juliana Lema, alisema matokeo ya kutotekeleza agizo hilo ni kukosekana kwa nyaraka muhimu ambazo zingesaidia katika kufanya tathimini ya maombi hayo ya Tanesco.
Lema alifafanua kwamba, hatua ya Tanesco kutoanisha manufaa na madhara ya kuongeza ada zake husunani katika mazingira kutasababisha watumiaji wa nishati ya umeme katika kupikia kuhamia katika matumizi ya mkaa hivyo kuongeza kasi ya uharibifu wa mazingira.
"Uharibifu huo utasababisha uhaba wa mvua ambao utasababisha ukosekanaji wa umeme wa maji na uliorahisi kwa wananchi," inasema sehemu tamko hilo.
Tamko hilo linaongeza kwamba, sekta ya viwanda ni eneo lingine ambalo baraza lingependa Tanesco iweke wazi iwapo ongezeko hilo halitaathiri uwezo wa ushindani wa viwanda vya nchini katika soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki na masoko mengine ya kimataifa.
Katika tamko hilo, baraza hilo la serikali linasema mengi ya matatizo ya Tanesco yamo ndani ya shirika na kutoa mfano wa wizi na kushindwa kukusanya vema mapato yao.
Lema akisoma tamko hilo, alitaja takwimu za kushuka kwa makusanyo kwamba, mwaka 2004 makusanyo yalifikia asilimia 108, 2005 asilimia 97, 2006 asilimia 87 na kuongeza kwamba mwelekeo huo unakinzana na matarajio ya Tanesco ya kufikia makusanyo ya asilimia 96 kwa miaka mitano ijayo (2007-2011).
"Kwa mfano wizi wa umeme wa watumiaji wakubwa wakishirikiana na wafanyakazi wa Tanesco, hili linanyima uwezo shirika kufikia malengo yaliyokusudiwa na wakati huo huo gharama za uzalishaji na usambazaji ziko pale pale," inasisitiza sehemu ya tamko.
Tamko hilo limeongeza kwamba, uamuzi wa kutaka kupandisha gharama za uunganishaji umeme kwa kati ya asilimia 196 na 280, utakuwa kikwazo kwa wananchi wengi wa kawaida kupata huduma za umeme hali ambayo itakwamisha mkakati wa Tanesco wa kupanua wigo wa wateja.
Akiwasilisha tamko la Shirikisho la Wenye Viwanda nchini (CTI) mwakilishi kutoka shirikisho hilo, Phocas Losway, alisema mpango wa shirika kupandisha kiwango hicho kwa muda mfupi si sahihi.
Losway alisema shirikisho linaamini kwamba, njia sahihi ni kupandisha gharama za matumizi ya huduma za umeme kwa viwango na nyakati tofauti.
Alisema mapendekezo ya CTI ni kupandisha umeme kwa asilimia kumi kwa miaka mitatu kwa kila mwaka asilimia 10.
Baraza la Watumiaji Huduma la Ewura (CCC), akisoma tamko hilo Makamu Mwenyekiti wake Said Mohamed, alisema Tanesco yenyewe haiko makini katika utoaji takwimu kwani inatoa takwimu zinazopingana.
Mohamed akisoma tamko hilo, alisema takwimu katika kundi lililopewa jina la gharama nyingine (Other Operating Expenses), zinapingana maradufu katika vipindi tofauti.
Katika tamko hilo, Mohamed alitoa mfano kwamba Agosti, 2007 gharama hizo ni sh 137,236 bilioni, 2008 zitakuwa sh 167,001 bilioni na mwaka 2009 sh 193,816 bilioni.
Aliongeza kwamba, Oktoba, 2007 gharama hizo ni sh 137,236 bilioni, 2008 ni sh 167,258 bilioni na 2009 ni sh 197,173 bilioni wakati Oktoba 29 ya mwaka huu pia, gharama ni sh 137,236, 2008 ni sh 239,648 na mwaka 2009 ni sh 279,014 bilioni.
"Licha ya takwimu kupingana, gharama ya bilioni hizi haziwezi kuwekwa kwenye kundi la Other Operating Expenses ( Gharama za matumizi mengine), bila kutoa mchanganuo, baraza limeshindwa kujiridhisha kuhusu uhalali wa takwimu hizi zinazo badilika badilika," inasema sehemu ya tamko.
Akisoma majumuisho ya mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu, alisema mamlaka itazingatia maoni ya wadau na itatoa maamuzi hivyo ambaye hataridhika ataka kuwa na uhuru wa kukata rufaa Tume ya Ushindani wa Kibiashara.
Masebu alisema maoni ya wadau yanaendelea kupokelewa kwa njia ya maandishi hadi mwisho Desemba ni saba na kusisitiza kwamba maoni hayo yataheshimiwa.
Kwa mara ya mwisho Tanesco ilipandisha ankara za umeme kwa asilimia sita, hapo Februari mwaka huu lakini karibuni imepeleka maombi yake Ewura ikitaka kupandisha tena ili liweze kuweza kuhimili ushindani wa kibiashara.