Matatizo ya Tanesco, serikali yatupiwa lawama

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,792
287,994
Posted Date::11/23/2007
Matatizo ya Tanesco, serikali yatupiwa lawama
Ramadhan Semtawa na Patricia Kimelemeta
Mwananchi

UAMUZI wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kuomba kupandisha viwango vya matumizi ya umeme umepingwa vikali na wadau mbalimbali huku wakisema 'mchawi' wa shirika hilo ni serikali kwa kuingia mikataba mibovu ndani ya shirika hilo.

Licha ya kueleza bayana kwamba mchawi wa shirika ni serikali, pia wamekosoa mishahara ya watumishi kuongezeka kila mara huku makusanyo ya shirika ikiwemo madeni yakizidi kuporomoka mwaka hadi mwaka.

Tanesco imeomba kuongeza gharama za huduma za kwa asilimia 40 na za kuunganisha kwa kati ya asilimia 196 na 280.

Maoni ya wananchi hao kupinga mpango huo wa Tanesco, yametolewa jijijini Dar es Salaam jana katika mkutano wa wadau ulioandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) kujadili mapendekezo ya shirika hilo.

Kwa upande wake, Christina Kilundu, akitoa maoni yake, alihoji ongezeko la gharama za uendeshaji na mishahara ya wafanyakazi kuwa juu huku makusanyo ya madeni yakishuka.

Kilundu ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa CTI, alisema takwimu zinaonyesha kuwa kila mwaka kumekuwa na ongezeko la fedha za kulipa mishahara ya watumishi wa shirika na kutaka liangaliwe kwa makini.

Kwa upande wake mwananchi mwingine, Renatus Mkinga, alisema miundombinu yote ya kuzalisha umeme imejengwa tangu enzi za serikali ya awamu ya kwanza chini ya Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere, lakini viongozi wa sasa wameleta makampuni mizigo kama Richmond/Dowans na IPTL.

Mkinga alisema makampuni hayo ni mizigo kwa shirika hivyo haiwezekani gharama hizo zibebwe na wananchi bali serikali yenyewe badala ya kuwadanganya wananchi kuwa kuna mvua kutoka Thailand kitu ambacho hakipo.

"Hivi nyie mkoje, mabwawa yote ya kuzalisha umeme sijui Kidatu, Mtera, yote haya kajenga Nyerere, nyinyi mnaleta mambo ya Richmond, Dowans, sasa mikataba hii mibovu mnataka hasara yake ibebwe na wananchi," alisema Mkinga na kuacha ukumbi mzima kuzizima kwa kicheko.

Mkinga alisema shirika hilo limeshindwa kukusanya madeni yake ambayo ni mabilioni ya shilingi, ambayo sehemu kubwa yanadaiwa katika taasisi za serikali.

Alihoji na kutaka kufahamu deni la Zanzibar ambalo Tanesco inadai kama tayari limelipwa.

"Madeni hayalipwi na wadaiwa wakubwa ni serikali, tuambieni deni la Zanzibar limeishia wapi, limelipwa?" alihoji.

"Kuiba muibe ninyi halafu sisi mtubebeshe madeni, wizi wa nyaya za umeme unafanyika, kama watu wanaweza kununua Satelite kuangalia usalama kwanini msiweke teknolojia ambayo mtu akiiba waya tu anakufa papo hapo," alisisitiza.

Kwa upande wake mwananchi mwingine aliyejitambulisha kama mwakilishi wa taasisi ya familia ya mzee Gwao, (jina kamili Mujengi Gwao), alisema hivi sasa Tanesco inataka kutupa hasara yake kwa wananchi akahoji vipi serikali ikwepe jukumu hilo.

Gwao alisema wananchi hawawezi kubeba hasara ya Tanesco kwani tayari hivi sasa kila kitu kimekuwa ghali, ikiwemo kodi za nyumba, huduma za elimu na afya na bidhaa nyingine na kuongeza kwamba hata madafu yamepanda bei.

Baraza la Ushauri la Serikali, katika tamko lake limesema uamuzi huo wa Tanesco kutaka kuongeza gharama hizo unathibitisha halikutekeleza kikamilifu agizo la Ewura la Januari 10, mwaka huu.

Akisoma tamko hilo la baraza hilo, Mkurugenzi wa baraza hilo Juliana Lema, alisema matokeo ya kutotekeleza agizo hilo ni kukosekana kwa nyaraka muhimu ambazo zingesaidia katika kufanya tathimini ya maombi hayo ya Tanesco.

Lema alifafanua kwamba, hatua ya Tanesco kutoanisha manufaa na madhara ya kuongeza ada zake husunani katika mazingira kutasababisha watumiaji wa nishati ya umeme katika kupikia kuhamia katika matumizi ya mkaa hivyo kuongeza kasi ya uharibifu wa mazingira.

"Uharibifu huo utasababisha uhaba wa mvua ambao utasababisha ukosekanaji wa umeme wa maji na uliorahisi kwa wananchi," inasema sehemu tamko hilo.

Tamko hilo linaongeza kwamba, sekta ya viwanda ni eneo lingine ambalo baraza lingependa Tanesco iweke wazi iwapo ongezeko hilo halitaathiri uwezo wa ushindani wa viwanda vya nchini katika soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki na masoko mengine ya kimataifa.

Katika tamko hilo, baraza hilo la serikali linasema mengi ya matatizo ya Tanesco yamo ndani ya shirika na kutoa mfano wa wizi na kushindwa kukusanya vema mapato yao.

Lema akisoma tamko hilo, alitaja takwimu za kushuka kwa makusanyo kwamba, mwaka 2004 makusanyo yalifikia asilimia 108, 2005 asilimia 97, 2006 asilimia 87 na kuongeza kwamba mwelekeo huo unakinzana na matarajio ya Tanesco ya kufikia makusanyo ya asilimia 96 kwa miaka mitano ijayo (2007-2011).

"Kwa mfano wizi wa umeme wa watumiaji wakubwa wakishirikiana na wafanyakazi wa Tanesco, hili linanyima uwezo shirika kufikia malengo yaliyokusudiwa na wakati huo huo gharama za uzalishaji na usambazaji ziko pale pale," inasisitiza sehemu ya tamko.

Tamko hilo limeongeza kwamba, uamuzi wa kutaka kupandisha gharama za uunganishaji umeme kwa kati ya asilimia 196 na 280, utakuwa kikwazo kwa wananchi wengi wa kawaida kupata huduma za umeme hali ambayo itakwamisha mkakati wa Tanesco wa kupanua wigo wa wateja.

Akiwasilisha tamko la Shirikisho la Wenye Viwanda nchini (CTI) mwakilishi kutoka shirikisho hilo, Phocas Losway, alisema mpango wa shirika kupandisha kiwango hicho kwa muda mfupi si sahihi.

Losway alisema shirikisho linaamini kwamba, njia sahihi ni kupandisha gharama za matumizi ya huduma za umeme kwa viwango na nyakati tofauti.


Alisema mapendekezo ya CTI ni kupandisha umeme kwa asilimia kumi kwa miaka mitatu kwa kila mwaka asilimia 10.

Baraza la Watumiaji Huduma la Ewura (CCC), akisoma tamko hilo Makamu Mwenyekiti wake Said Mohamed, alisema Tanesco yenyewe haiko makini katika utoaji takwimu kwani inatoa takwimu zinazopingana.

Mohamed akisoma tamko hilo, alisema takwimu katika kundi lililopewa jina la gharama nyingine (Other Operating Expenses), zinapingana maradufu katika vipindi tofauti.

Katika tamko hilo, Mohamed alitoa mfano kwamba Agosti, 2007 gharama hizo ni sh 137,236 bilioni, 2008 zitakuwa sh 167,001 bilioni na mwaka 2009 sh 193,816 bilioni.

Aliongeza kwamba, Oktoba, 2007 gharama hizo ni sh 137,236 bilioni, 2008 ni sh 167,258 bilioni na 2009 ni sh 197,173 bilioni wakati Oktoba 29 ya mwaka huu pia, gharama ni sh 137,236, 2008 ni sh 239,648 na mwaka 2009 ni sh 279,014 bilioni.

"Licha ya takwimu kupingana, gharama ya bilioni hizi haziwezi kuwekwa kwenye kundi la Other Operating Expenses ( Gharama za matumizi mengine), bila kutoa mchanganuo, baraza limeshindwa kujiridhisha kuhusu uhalali wa takwimu hizi zinazo badilika badilika," inasema sehemu ya tamko.

Akisoma majumuisho ya mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu, alisema mamlaka itazingatia maoni ya wadau na itatoa maamuzi hivyo ambaye hataridhika ataka kuwa na uhuru wa kukata rufaa Tume ya Ushindani wa Kibiashara.

Masebu alisema maoni ya wadau yanaendelea kupokelewa kwa njia ya maandishi hadi mwisho Desemba ni saba na kusisitiza kwamba maoni hayo yataheshimiwa.

Kwa mara ya mwisho Tanesco ilipandisha ankara za umeme kwa asilimia sita, hapo Februari mwaka huu lakini karibuni imepeleka maombi yake Ewura ikitaka kupandisha tena ili liweze kuweza kuhimili ushindani wa kibiashara.
 
Mchungaji adai sera ya umeme itamponza Rais

Habari Zinazoshabihiana
• Mchungaji aituhumu Serikali ya Kikwete 24.01.2007 [Soma]
*Shinyanga nao wamlilia, wamtaka aingilie kati
*Wasema kinachoendelea kinapingana na Ilani

Na Thompson Mpanji, Mbozi
Majira

KANISA la Tanzania Assemblies of God (TAG), Mlowo, wilayani hapa, limemtahadharisha Rais Jakaya Kikwete, kuwa endapo hatachukua hatua za haraka za kuleta mabadiliko ya sera ya sasa ya kuwa na shirika moja la umeme, itamharibia mwaka 2010.

Onyo hilo lilitolewa jana na Mchungaji wa Kanisa hilo, Bw. Daud Katule, alipozungumzia ombi la TANESCO kuongeza gharama za bili ya umeme kwa asilimia 40 na kuunganisha umeme kati ya asilimia 196 na 280.

Mchungaji huyo alisema hoja ya kufuta sera ya kuwa na shirika moja la umeme itamgharimu Rais Kikwete hasa wakati wa uchaguzi mkuu kutokana na vyama vya siasa vya upinzani kuitumia hoja hilo kama rungu la kummaliza kisiasa.

"Hili ni suala nyeti na linamgusa kila Mtanzania…Kikwete anakabiliana na majaribu (changamoto) makubwa, tangu achaguliwe gharama hizi ambazo hazijapandishwa hadi sasa Watanzania walio wengi hasa wa vijijini wameshindwa kumudu na kuendelea kuhaha kupata nishati hiyo, leo kabla hajafanikisha, unamwambia unapandisha gharama wataielewaje Serikali?," alihoji Bw. Katule.

"Lakini pia Kikwete awe makini na shirika hili, kwani ndilo linaweza kumhujumu katika uongozi wake…inawezekana ikawa hujuma, wanataka kuleta hali mbaya kwa wananchi wengi, haiwezekani makusanyo ya nchi nzima yakashindwa kuendesha shirika, kama wamefilisika ni bora waseme si kuwarundikia mzigo Watanzania,"alisisitiza.

Aliitaka Serikali iangalie uwezekano wa kukaribisha wawekezaji wengine wa kutoa huduma ya nishati kutoka nje ili kuleta ushindani na unafuu wa maisha.

"Kuna mashirika kama ya kijapani yapo mengi yana uwezo mkubwa wa kuendesha huduma hizi kwa ubora na ufanisi zaidi, kwa majaribio wapewe kama kanda moja ya Kusini waone utendaji wao na kwa maoni yangu TANESCO ina uwezo wa kutoa huduma katika mikoa miwili au mitatu," alisema.

Mchungaji huyo alitolea mfano wa Zambia ambayo ina kampuni zaidi ya moja za kutoa huduma ya umeme, "unapojenga pagale unakuta kampuni ya umeme imeshawahi kusogeza nguzo ya umeme, ukimaliza kujenga umeme unawashwa na imefikia mtu anaweza kuwa mteja wa zaidi ya kampuni moja, anafanya kama vile laini za simu, zote anajaza pesa ukizima ama ikiisha huku anatumia huku," alisema Mchungaji Katule.

Alifafanua, kuwa kupata huduma ya umeme hata kunufaika nao nchini ni kama mtu amepata maisha ya peponi na kuonekana ni kama jambo la muujiza ama neema fulani miongoni mwa jamii ya kitanzania.

"Watanzania hawatamwelewa Kikwete kuwa moto wake wa maisha bora kwa kila Mtanzania kasi yake imesishia wapi...TANESCO wamwache Kikwete atimize ndoto yake na kutilia mkazo wa kupitisha sheria ya kuwapo kampuni nyingi za umeme," alisema.

JK ingilia kati

Kutoka Shinyanga, Suleiman Abeid, anaripoti kwamba
sakata la kusudio la TANESCO kutaka kuongeza bei zake kwa viwango mbalimbali limezidi kupigiwa kelele na wananchi ambapo wakazi wa Shinyanga wamemwomba Rais Kikwete aingilie kati na kutoa tamko.

Wakizungumza na Majira mjini hapa kwa nyakati na maeneo tofauti, wakazi hao walisema baada ya kuwapo kila dalili ambazo zinaonesha wazi bei hizo zitapanda kama ilivyokusudiwa, ni vizuri Rais Kikwete akaingilia kati na kuizuia hali hiyo.

Walisema hawatamwelewa Rais wao iwapo hatazuia hali hiyo na kwamba bei zikipanda watakaa kimya na kumsubiri mwaka 2010, kwenye jukwaa la kuomba kura.

Mmoja wa wakazi hao, Bw. Fredy Akida, alisema ni bora mara 100 Rais asingezungumzia lolote kuhusiana na utata wa suala la Buzwagi, lakini akatoa tamko kwa hili la kupanda kwa bei ya umeme nchini.

"Mimi nafikiri kuwa hili suala la TANESCO linatugusa wengi, ni bora Rais asingetoa tamko lolote kuhusiana na suala la Buzwagi, lakini asimame kidete kuzuia janga hili, nasema ni janga kwa vile litatuumiza wananchi wenye kipato cha chini," alisema Bw. Akida.

Aliongeza: "Hawa TANESCO ni matapeli, ni vizuri Rais akaingilia kati na kuzuia kupanda kwa bei hizi, mwaka jana Februari, bei ziliongezwa kwa madai kuwa wanaboresha huduma, lakini hakuna tulichokiona, hali ni ile ile, sasa hii ni kutuumiza, nafikiri wanachotafuta si uboreshaji, bali ni kuongeza maslahi ya wakubwa ndani ya TANESCO," alieleza Bw. Akida.

Wakazi hao walihoji sababu za msingi za shirika hilo kutaka kupandisha bei za huduma zake wakati halioneshi juhudi zozote za kukusanya madeni, kutoka kwa wadeni wake na kwamba baadhi ya kumbukumbu za madeni zimepitwa na wakati na zinaidanyaga Serikali.

"TANESCO wanashangaza, laiti wangejipanga vizuri, wangekusanya fedha nyingi sana kutoka kwa wateja wao, leo wanaendelea kukumbatia kumbukumbu za madeni ya watu waliokufa, huku wakikataa kuwaunganishia umeme watu wanaoishi katika nyumba za marehemu hao kwa vile wanadaiwa na TANESCO," alieleza Bw. Shija Mathias.

Bw. Mathias alisema iwapo TANESCO itafuta madeni yote ya miaka ya nyuma na kuwaunganishia umeme wateja wapya katika nyumba zilizokatiwa huduma miaka mingi, ni wazi itakusanya fedha nyingi zitakazokidhi kuendeshea huduma mbalimbali ndani ya shirika.

"Mimi ingawa si mtaalamu wa mahesabu, lakini huwa nasikia kuna kitu kinaitwa ‘madeni mabaya' haya hufutwa pale njia zote za kulipwa kwake zinaposhindikana, lakini hawa wenzetu mpaka leo wameendelea kuwadai marehemu, itawezekana hilo?," alihoji Bw. Mathias.

Naye kada maarufu wa CCM mjini hapa ambaye hakupenda kutajwa jina, alisema suala la umeme limo ndani ya Ilani ya Chama chao ambapo iliahidiwa kuwa Serikali ya Awamu ya Nne itajitahidi kuwapatia wananchi wake huduma nafuu za umeme.

Kwa kuthibitisha kauli yake, kada huyo alinukuu ibara ya 43 ndani ya Ilani ya uchaguzi ya CCM isemayo: "Aidha, umeme unaopatikana hivi sasa ni wa gharama kubwa, katika kipindi kijacho, hatua zifuatazo zitachukuliwa zenye lengo la kuongeza nishati hasa ya umeme, ili uwafikie wananchi wengi zaidi."

Alisema moja ya hatua hizo iliyoainishwa katika ibara hiyo kifungu (f) inaeleza wazi kuwa, "kuweka mkakati wa uzalishaji umeme wa kutosha na wa gharama nafuu zaidi kwa lengo la kuongeza ufanisi viwandani."

Kada huyo alisema ili CCM wasionekane waongo na kusutwa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu nchini mwaka 2010, ni vizuri Rais Kikwete akasimama kidete na kuzuia hali hiyo kwa vile itawaumiza wananchi wengi na gharama za maisha zitapanda maradufu.

Aidha, mkazi wa mtaa wa Buzuka, Bw. Rashidi Mhango, alisema kimefika kipindi hivi sasa Serikali kupitia upya mikataba ya IPTL, Songas, Dowans na mradi wa makaa ya mawe wa Kiwira, ambao inahisiwa nao umejiunga katika kulipwa fedha na TANESCO, kwa ajili ya kuizuia umeme.

Bw. Mhango alisema anaamini ongezeko la gharama zinazoombwa na TANESCO hivi sasa, si kwa ajili ya kuboresha huduma, bali ni kuwaongezea malipo watu wenye kampuni binafsi wanaoiuzia umeme.

"Hapa bwana hakuna namna, ni lazima Kikwete aingilie kati, hawa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) hawana kitu, hapa Shinyanga tulikataa mbele yao bei za maji kupanda, mpaka huduma ziboreshwe, lakini bei zimepandishwa kimyakimya na kwa TANESCO itakuwa hivyo hivyo," alieleza Bi Beldina Charles.

Safari ya Dkt Rashidi

Naye Hemed Kivuyo, anaripoti kutoka Arusha, kwamba
hatua ya kujiuzulu kwa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Dkt. Idrisa Rashidi, ilianza kuonekana mkoani hapa katika mkutano ulioshirikisha wananchi kutoa maoni yao juu ya kupanda kwa bei ya umeme, Majira imefahamishwa.

Dkt. Rashidi alifanya mkutano katika ukumbi wa Benki Kuu mjini hapa na kukumbana na wakati mgumu baada ya wananchi waliofika kutoa maoni yao walipomtaka ajiuzulu yeye na baadhi ya viongozi wa Serikali kuliko kupandisha bei ya umeme.

Kabla ya wananchi hao kutoa maoni yao, Dkt. Rashidi alitoa sababu za kutaka kupandisha bei ya umeme kwa asilimia 40 na kutaja sababu kadhaa ikiwa ni pamoja na kusitishwa kwa ruzuku waliyokuwa wakipewa na Serikali .

Baada ya kumaliza, ilifuatia EWURA ambayo ilitoa sababu kadhaa za kukataa kupanda kwa bei ya umeme, huku wananchi wakiunga mkono kwa kupiga makofi.

Ulipofika wakati wa wananchi kutoa maoni yao, Mkurugenzi alijikuta katika wakati mgumu baada ya kila mwananchi aliyesimama, kudai kuwa hakuna mantiki ya shirika hilo kupandisha bei ya umeme.

Wananchi hao walidai kuwa kutokupewa ruzuku kwa shirika hilo ni sababu ambazo haziwahusu na mikataba mibovu iliyoingia ni sababu za shirika hilo kupandisha bei ya umeme na kufanya hivyo ni kumwonea mwananchi wa kawaida.

Nao wamiliki wa kampuni mbalimbali waliofika kutoa maoni yao walidai kuwa katika shirika hilo, kumejaa ufisadi na madeni ya miaka mingi na kupandisha bei kwa mwananchi ni kumwonea na kuongeza kuwa kama bei hiyo itapanda nao watapunguza wafanyakazi.

Baadhi ya wananchi waliotoa maoni yao walidai kuwa ni vyema viongozi wa shirika hilo wakajiuzulu mmoja mmoja na kuwaachia kazi hiyo watu wengine, kuliko bei hiyo kupanda kila wakati.

Akizungumza na Majira mmoja wa waliotoa maoni hayo Bw. Amos Alex (55) mkazi wa Ngulelo, alisema wao wateja, hawaitaji kupanda kwa bei ya umeme na walikuwa wakitaka Mkurugenzi huyo ajiuzulu na baadhi ya viongozi wa Serikali walioshiriki kuweka mikataba isiyo na manufaa kwa wananchi.

"Ni afadhali amejiuzulu, kwa sababu mikataba waliyoiweka miaka ya nyuma wao na baadhi ya viongozi wa Serikali ndiyo madhara yake yameanza kuonekana hivi sasa, sio ajiuzulu peke yake na hata baadhi ya viongozi wa Serikali," alisema Bw. Amos.

Kitendo cha wananchi hao kumtolea maneno hayo Mkurugenzi huyo kilimfanya akune kichwa kila wakati na hata alipoinuka kwa mara ya pili, hakuwa na la kusema zaidi ya kukiri upungufu ndani ya shirika hilo na kuonekana kukubaliana na maoni ya wananchi hao.
 
Wakati TANESCO iko hoi bin taabani waliowaleta makaburu wa Net Group Problems wamekaa kimya wanakula kuku! bila kuwasahau wale waliosaini mikataba bomu kati ya Richmond, IPTL, Kiwira Coal Mining na Dowans. TANESCO wanalipa mabilioni ya fedha kwa huduma ambazo labda wasingezihitaji au wangezipata kwa bei ya chini.
 
Kama serikali ndio imeleta matatizo TANESCO, basi ni serikali hiyo hiyo ndiyo itakayoyatatua. Ukipewa kazi ya kuendesha shirika kama hilo, sikiliza serikali inachosema. Na ukitaka kufanya uamuzi wowote peleka hukohuko serikalini kwanza. Na nitashangaa sana kama serikali itaruhusu wananchi wanyanyaswe na shirika ambalo serikali yenyewe ina mamlaka nalo. Wananchi wameiweka serikali hii madarakani ili iwaondolee kero zao ikiwamo hii ya umeme. Litakuwa jambo la kushangaza sana kama serikali itaruhusu kero ya umeme iongezeke badala ya kupungua.
 
Ati unakataa kumuunganishia umeme mteja kwa vile unayemdai amekufa au amehama!!! Mkataba unakuwa na nyumba na sio mtu? Badala ya kuunganisha ukusanye mapato na uendelee kumfuatilia mdeni wako,unamkataa mteja mpya!Iko kazi.
 
DAILY NEWS Reporter
Daily News On Saturday; Saturday,November 24, 2007 @00:02

THE resignation of Tanzania Electric Supply Company (Tanesco) Managing Director, Dr Idris Rashid, has been linked to meddling by his minister and board chairman in his decision to disconnect power at Tanga Cement Factory (TCC) early this week.

Reliable sources close to the board of directors and within Tanesco said that Dr Rashid resigned because the Board Chairman, Ambassador Fulgence Kazaura, ordered restoration of power at TCC some hours after it was disconnected on Tuesday. Other highly placed sources further said that Dr Rashid's resignation was likely to be rejected and he would be required to continue with his post.

"The bottom-line is he will continue to be the chief executive officer of Tanesco", said one source. When reached for comment, the Minister for Energy and Minerals, Mr Nazir Karamagi, admitted that Tanesco still needs the services of Dr Rashid. "I doubt if the TCC power issue is what prompted his decision to resign. There could be some other issues…but I cannot know for sure. Find out more", said Mr Karamagi.

Sources, however, said that trouble started brewing at the power utility company since Dr Rashid was appointed and after he started introducing changes. Shortly after his appointment, Tanesco withdrew the vehicle that was being used by the chairman on a daily basis. The company also moved the chairman from a posh office that he was using at the former headquarters of the company.

The office, sources say, is now being occupied by the Tanesco Ilala Regional Manager. As for the TCC saga, sources said that Dr Rashid ordered power to be disconnected at the factory after getting an official report that TCC's meter was tampered with and the company ignored Tanesco's letter asking for settlement of an outstanding bill of 47m/-.

A few hours after the factory was halted, the Minister for Energy and Minerals, Mr Nazir Karamagi, called Dr Rashid and wanted power to be restored after explaining to him economic, political and social implications of such a move. Dr Rashid did not agree to rescind his decision and moments later Ambassador Kazaura called him and a conversion similar to that of Minister Karamagi followed but the MD, then, maintained his position.

Sources said, "Ambassador Kazaura called the Tanga Manager and ordered him to restore power. The manager did so immediately. When Dr Rashid got information that power was restored at TCC, he called the manager to disconnect power immediately and he obeyed." Dr Rashid received the calls of Mr Karamagi and Ambassador Kazaura when he was in Arusha on Tuesday where public hearing session on the proposed 40 per cent tariff increase and 100 per cent up on connection charges was held.

Sources said: "Soon after arrival from Arusha on Wednesday he presented his resignation letter to the board chairman who convened an emergency meeting which endorsed it. "Dr Rashid told the members that he took the decision because the minister and the board chairman were interfering with operational issues of the company. Their role in relation to Tanesco is on policy issues and not operations."

Minister Karamagi said he contacted Dr Rashid over the TCC power disconnection matter. He did so after getting a call from fellow minister for Industries, Trade and Marketing inquiring about the move taken by Tanesco. "I shared his concern over the repercussions in the light of the prevailing shortage of cement which forced the government to allow importation and following that decision the price of cement has started to go down.

"I contacted Dr Rashid because it was procedural. I also contacted the board chairman and directed him to deal with the matter. So who else could he have contacted if not Dr Rashid," he quipped.
 
Posted Date::11/24/2007
Dk Rashidi aeleza kwa nini alitaka kujiuzulu
*Asema alikerwa na tabia ya kuingiliwa katika kazi
*Ni katika suala la kiwanda cha Saruiji Tanga

*Adai alibadili msimamo baada ya kushauriwa

Na Joyce Mmasi
Mwananchi

MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco), Dk Idris Rashidi ametaja sababu za kujiuzulu na hatimaye kuondoa kusudio lake baada ya kushauriana na watu mbalimbali.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili kwa njia ya simu jana, Dk Rashidi alisema alichukua uamuzi wa kujiuzulu kutokana na kuingiliwa katika kazi zake na baadhi ya watu na hasa suala la kukikatia umeme Kiwanda cha Saruji cha Tanga.

Alisema kuna watu ambao hata hivyo alikataa kuwataja majina, walijaribu kumuingilia katika suala la kiwanda hicho, ndipo alipoona njia sahihi ni kukaa pembeni, hivyo akaamua kuandika barua ya kujiuzulu.

Akizungumzia sababu za kuamua kuandika barua nyingine ya kuondoa ile ya kwanza ya kujiuzulu, alisema alifanya hivyo baada ya kukaa na kuzungumza na watu.

Hata hivyo, vile vile alikataa kuwataja watu waliomshauri kuondoa uamuzi wake wa kujiuzulu.

Dk Rashidi alisema baada ya tukio la Kiwanda cha Saruji Tanga kuwekwa hadharani kila Mtanzania ameelewa kile kilichokuwa kinafanyika, na watu wote wanajua kwamba hata katika kazi, kila mtu ana mipaka.

Alisema hapendi kuingiliwa katika kazi zake na kuwa hata yeye hajawahi kumuingilia mfanyakazi yeyote wa shirika hilo katika kutekeleza maamuzi yake katika eneo lake la kazi.

Mameneja wangu mikoani wanafanya maamuzi yao huko bila kuingiliwa na yeyote, kama kuna mtu amekamatwa akiwa amelihujumu shirika kwa utaratibu wowote anaadhibiwa papo hapo kwa kukatiwa umeme, sijawahi kumuingiliwa mtu, lakini iweje mimi niingiliwe katika hili la Tanga Cement?� alihoji Dk Rashidi na kuongeza:

Mbaya zaidi ni kuwa hawa Tanga Cement tuliwapa muda wa kutosha kushughulikia matatizo yao, wakashindwa kurekebisha, tulipowachukulia hatua kunatokea kuingiliwa, Ni vizuri kila mtu afuate taratibu alizopewa katika kazi zake.

Akizungumzia madeni ya shirika hilo na madai ya vyombo vya habari kwamba Rais Jakaya Kikwete amempa rungu la kukusanya madeni na kuwakatia umeme wote wanaodaiwa, Dk Rashidi alisema, Mimi sijaenda Ikulu wala sijazungumza na Rais ama na Waziri Mkuu.

Kuhusu mikakati ya kukusanya madeni yao,alisema tayari walishaanza na kuwa wanachofanya sasa ni kuendelea na zoezi bila kumuonea mtu yeyote haya awe serikali, taasisi au mtu binafsi.

Kukusanya madeni ni kazi ya Tanesco, tulishaanza na hatuwezi kumsamehe mtu katika hili, iwe serikali, taasisi au mtu binafsi wote wanapaswa kulipa madeni wanayodaiwa na shirika,� alisema.


Alipoulizwa juu ya deni la Zanzibar lililodaiwa na wadau wa shirika hilo kuwa ni kubwa, Dk Rashid alisema, Tanesco haiidai Zanzibar kiasi chochote cha fedha na kuwa kwa muda wote wa yeye kuwa katika shirika hilo, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuwa ikilipa madeni yake kwa wakati.

Hatuidai serikali ya Zanzibar hata shilingi moja, kwa muda wote nilipokuwa Tanesco, Zanzibar imekuwa ikilipa madeni yake kwa wakati, alisema na kufafanua kuwa bei ya umeme kwa Zanzibar ni sawa na kwa mashirika na makampuni mengine na kuwa utaratibu wa kulipa nao ni ule ule.

Alisema anachojua yeye ni kuwa serikali ya Zanzibar inao utaratibu wa kutoa ruzuku katika suala la umeme ili kuwapa urahisi wa kulipa ankara wananchi wake.

Alhamisi iliyopita Tanesco iliikatia Kampuni ya Saruji ya Tanga, hatua iliyosababisha kampuni hiyo kukifunga kiwanda kwa muda, kabla ya kurudishiwa umeme siku hiyo hiyo, ambayo pia Dk Rashidi alitangaza kujiuzulu wadhifa wake.

Uamuzi wa kujiuzulu kwake, awali ulitawaliwa na kiwingu na kauli tofauti, hadi ulipothibitishwa kwa nyakati tofauti na Dk Rashidi mwenyewe, Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco, Balozi Fulgensi Kazaura na Waziri wa Nishati na Madini Nazir Karamagi siku iliyofuata.

Wakati hayo yanatokea, shirika hilo lilikuwa katikati ya mjadala mkali kuhusu ombi lake la kutaka kupandisha bei na gharama za uunganishaji umeme ambapo wadau waliokutana katika mkutano ulioandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) walipinga vikali mpango huo.

Mchakato wa ukusanyaji wa maoni ya wadau kuhusiana na suala hilo utachukua siku 84 unaendelea, kwani baada ya mjadala wa wazi juzi, maoni wadau yanapokelewa kwa maandishi hadi Desemba 7, mwaka huu saa 11 jioni.

Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu alisema juzi kuwa baada ya hatua niyo, Ewura itatoa maamuzi yake na kuyachapisha katika gazeti la serikali na kwenye magazeti mengine ya kawaida.

"Endapo kuna upande hautaridhika na maamuzi ya mamlaka hiyo, rufaa inaweza kukatwa kwenye Baraza la Ushindani wa Haki katika Biashara," alisema.

Akichangia mjadala huo wa wazi, Mkurugenzi Mtendaji wa CTI, Christina Kilundu, alihoji sababu za kushuka kwa ukusanyaji wa madeni Ilhali kuna ongezeko la gharama za uendeshaji na mishahara ya wafanyakazi.

Kilundu alisema takwimu zinaonyesha kuwa kila mwaka kumekuwa na ongezeko la fedha za kulipa mishahara ya watumishi wa shirika na kutaka hilo liangaliwe kwa makini.

Mdau mwingine, Renatus Mkinga, alisema miundombinu yote ya kuzalisha umeme imejengwa tangu enzi za serikali ya awamu ya kwanza chini ya Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere, lakini viongozi wa sasa wameleta makampuni ambayo ni mzigo kwa wananchi kama vile Richmond/Dowans na IPTL.

"Hivi nyie mkoje, mabwawa yote ya kuzalisha umeme sijui Kidatu, Mtera, yote haya kajenga Nyerere, nyinyi mnaleta mambo ya Richmond, Dowans, sasa mikataba hii mibovu mnataka hasara yake ibebwe na wananchi," alihoji Mkinga na kuacha ukumbi mzima kutawaliwa na kicheko.

Alisema shirika hilo limeshindwa kukusanya madeni yake ambayo ni mabilioni ya shilingi, ambayo sehemu kubwa yanadaiwa katika taasisi za serikali, na akataka kufahamu deni la Zanzibar kama limelipwa.

"Madeni hayalipwi na wadaiwa wakubwa ni serikali, tuambieni deni la Zanzibar limeishia wapi, limelipwa?" alihoji.

Mwananchi mwingine Mujengi Gwao, alisema hivi sasa Tanesco inataka kutupa hasara yake kwa wananchi na kuhoji vipi serikali ikwepe jukumu hilo.

Gwao alisema wananchi hawawezi kubeba hasara ya Tanesco kwani tayari hivi sasa kila kitu kimekuwa ghali, ikiwemo kodi za nyumba, huduma za elimu, afya na bidhaa nyingine hadi madafu.

Mkurugenzi wa Baraza la Ushauri la Serikali, baraza hilo Juliana Lema, alisema uamuzi huo wa Tanesco kutaka kuongeza gharama unathibitisha kuwa haikutekeleza kikamilifu agizo la Ewura la Januari 10, mwaka huu, la kuitaka kuwa na nyaraka muhimu ambazo zingesaidia katika kufanya tathimini ya maombi hayo ya Tanesco.

Akiwasilisha tamko la Shirikisho la Wenye Viwanda nchini (CTI), Phocas Losway, alisema mpango wa shirika kupandisha kiwango hicho kwa muda mfupi si sahihi.

Losway alisema shirikisho linaamini kwamba, njia sahihi ni kupandisha gharama za matumizi ya huduma za umeme kwa viwango na nyakati tofauti.

Akisoma majumuisho ya mkutano huo, Masebu, alisema mamlaka itazingatia maoni ya wadau na itatoa maamuzi hivyo ambaye hataridhika atakuwa na uhuru wa kukata rufaa Tume ya Ushindani wa Kibiashara.

Kwa mara ya mwisho, Tanesco ilipandisha ankara za umeme kwa asilimia sita, Februari mwaka huu na karibuni imepeleka maombi mengine Ewura ikitaka kupandisha tena kwa asilimia 40 kwa watumiaji na kati ya asilimia 196 na 280 kwa waunganishaji wa umeme ili liweze kuweza kujiendesha na kufanya kazi kibiashara.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom