Matatizo ya kifamilia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matatizo ya kifamilia

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Che Kalizozele, Sep 19, 2008.

 1. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2008
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Jamaa wawili walikutana kwenye kituo cha basi wakafanya mazungumzo. Mmoja aling'ang'nia kuzungumzia kero za familia yake hatimaye mwenzake akasema " Unadhani familia yako ina matatizo?"

  Basi sikiliza kisa hiki.

  "Miaka michache iliyopita nilikutana na mwanamke mjane aliyekua na binti mkubwa tu na tukaamua kuoana. Baadaye baba yangu akamuoa binti yangu wa kambo hivyo huyo binti yangu wa kambo akawa mama yangu wa kambo na Baba yangu akawa mtoto wangu wa kambo wa kiume ambapo mke wangu akawa mama mkwe wa mkwe wake.

  Baadaye binti ya mke wangu yaani binti yangu wa kambo alipata mtoto wa kiume. mtoto huyo wa kiume alikua ndugu yangu kwa sababu tulichangia baba mmoja. lakini kwa vile alikua ni mtoto wabinti wa mke wangu papo hapo akawa mjukuu wa mke wangu na mimi nikawa babu yake mdogo wangu.

  Lakini hayo yote yalikua si kitu mpaka mimi na mke wangu tulipopata mtoto wa kiume. Sasa msichana ambaye ni ndugu wa mtoto wangu huyo wa kiume kwa kuchangia mama yao mmoja, akawa pia bibi yake. Hali hiyo ilimfanya pia baba yangu kua shemeji wa mtoto wangu ambaye ndugu yake wa kike kwa upande wa mama yao ndie mke wake baba yangu.Tatizo ni pale tunapokutana,unatumia jina gani au cheo kipi.

  SWALI.

  Je, unadhani mpaka hapo wewe una matatizo ya kifamilia? Acha kulalamika
   
 2. africa6666

  africa6666 JF-Expert Member

  #2
  Sep 19, 2008
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 281
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hiyo si rahisi kutokea ktk familia za kiafrika kwa sababu ktk kuja kutoa posa ya kumuoa binti yako wa kambo, wewe ndo unatoa ridhaa ya kuolewa kwa niaba ya mkeo. sasa iweje baba yako aje atake kumuoa binti yako halafu wewe umkubalie??

  Labda kama walikutana huko mitaani na kuamua kuishi bila ridhaa yako, na kwa mtindo huo hamtakuwa na mahusiano mema, so it resolves
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Jun 5, 2017
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,154
  Trophy Points: 280
  .......
   
Loading...