Matatizo ya Kampuni ya Zantel Tanzania

Matatizo ya Kampuni ya Zantel Tanzania

Matatizo lukuki yanayokumba ni pamoja na:


1.KIFURUSHI CHA BMP

Yaani kifurushi cha BONGA MPAKA BASI ndio mnakiona cha maana sana kuliko hata MB na SMS!
Yaani mtu aweke 3000 apate dakika 220 SMS 50 na MB 50.
Kwa kweli hapa mmefeli.


2.SPIDI YA INTANETI

Hapa kwenye spidi niseme kweli mpo vizuri
Kazeni kamba maana hata Vodacom Tanzania wapo vizuri kuliko mtandao wowote mkifuatia nyie Zantel.


3.KUSHINDWA KUSIKILIZA MAONI YA WATEJA.

Sijui mnakwama wapi? Yaani hata wateja wakiwapa maoni kuhusu maboresho ya vifurushi mnawapuuzia.
Hata huduma ya kuwasiliana na wateja kwa njia ya WhatsApp hamna?
Tena pale Makao Makuu yenu ya jirani na ubalozi wa USA, watoa huduma wana nyodo sana.
Yaani wanakujibu kama vile wanakusuta.


4.VIFURUSHI VYA USIKU

Hapa msinibishie kabisa, hamna kufurushi chochote kile cha intaneti cha usiku kuanzia saa 6 mpaka saa 12.
Wenzenu TTCL na Halotel hizi huduma wanazo na tunaenjoy sana usiku.
Fanyeni mpango mtupatie hata
>>> GB 1 kwa 500 saa 6 usiku hadi saa 12 asubuhi.
>>> GB 3 kwa 1000 saa 6 mpaka saa 12 asubuhi.


4.VIFURUSHI VYA CHUO

Ukipiga *148*05# kisha ukichagua Vyuo vya Bara
Aisee kama simu yako mnara unasoma 3G, H, H+ au 4G lazima igome kujiunga na kifurushi.
Mpaka uende kwenye setting useti mnara usome 2G kisha ujaribu kujiunga tena ndio itakubali ila kwa mbinde.


5.KERO YA SMS ZA OFA

Yaani nyie kwenye ustaarabu ni 0.3% yaani mnatuma SMS za ofa ovyo mpaka najifikiria kuwatukana.
Yaani kwa siku mnatuma SMS 12 yaani wastani wa kila saa mnatuma tu SMS.
Yaani hapa nilipo laini yenu nimeitoa kwenye simu ipo kwenye kabati sababu ya ujinga huu.


6.VIFURUSHI VYA SMS

>>Tsh 500 mnatoa SMS 150 saa 24
>>Tsh 1000 mnatupa SMS 500 wiki
>>Tsh 3000 mnipe SMS 2000 kwa mwezi!

Hapa mmefeli vibaya mno, yaani vibaya mno.
Nendeni mkajifunze hata kwa Vodacom Tanzania


7.VIFURUSHI VYA INTANETI HAVINUNULIKI

Ni bei mno jaribuni kukaa chini mshushe hiyo bei.
Waangalieni Halotel, TTCL na kidogo Airtel.
Nawapenda sana Zantel, tatizo mna vifurushi ghali sana.



Kwa staili hii mtapoteza wateja, mtafilisika na hatimaye mtarudi Visiwani kuimba Taarab na Kaswida kama sio kuuza urojo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, Zantel bado wako vizuri sana as long as vifurushi vyao vya chuo kila mteja wa bara anaweza kuvipata, suala la kujiunga ni network tu.
Vifurushi vya Internet ukitaka ufaidi jiunge vya wiki, Utafurahia sana na hakuna mtandao wa kushindana nao kwa kipande hicho.

Ila kwa kweli upande wa bando za usiku na SMS Daah, hasa kwa anaependa kuchat kwa SMS anaonewa na Zantel, wajirekebishe.
 
Mkuu, Zantel bado wako vizuri sana as long as vifurushi vyao vya chuo kila mteja wa bara anaweza kuvipata, suala la kujiunga ni network tu.
Vifurushi vya Internet ukitaka ufaidi jiunge vya wiki, Utafurahia sana na hakuna mtandao wa kushindana nao kwa kipande hicho.

Ila kwa kweli upande wa bando za usiku na SMS Daah, hasa kwa anaependa kuchat kwa SMS anaonewa na Zantel, wajirekebishe.
Shukrani sana mkuu.
Upande wa network wapo vizuri, ila upande wa SMS wanatuonea sana.

Ila vifurushi vya intaneti vy usiku ni muhimu sana.

Natamani siku moja nionane na Afisa Masoko wao nimchane laivu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shukrani sana mkuu.
Upande wa network wapo vizuri, ila upande wa SMS wanatuonea sana.

Ila vifurushi vya intaneti vy usiku ni muhimu sana.

Natamani siku moja nionane na Afisa Masoko wao nimchane laivu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, usijisumbue, Tigo tayar washa takeover, Zantel Kwa upande wa Bara ipo chini ya Tigo, management kuu inatoka Tigo.
Sijajua itafanyika Total Acquisition au Wataiacha ijitegemee.
 
Kwani tusi maanake nini ungesema TUU mapungufu ya Zantel ili warekebishe uliposema rudini Zanzibar ulukusudia nn kama si utudhalilisha kwamba mambo ya kupizi huwa yanakubalika Zanzibar na hayakubaliki Tanganyika hiyo ndio tafsir yake
Basi maalim umeshinda.

Maana sipendagi kubishana na watu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hapa umechapia, wanatoa
1000 Dk100 (55dk-Z to Z na 45dk all net) + 100sms +50mb
1000 1Gb + 20dk(5dk all net) + 50sms
Kuna shida ya shule uliyopitia naona aaah!!!

Umeshindwa kuelewa paragraph hii hapa...
"Sijui kama wana toa huduma kulingana na muda mteja aliokaa ila kwa upande wa bandle, sms au mins naona kawaida"
 
Natumia Zantel, kiukweli kwangu naona jamaa wako poa tu.

Menu ya *148*05# napata ofa ya vifurushi vya chuo 1500 GB 1.5, dk 160 mitandao yote na SMS 1000 kwa wiki.

Pia *149*15# napata ofa ya Bao Tanga 1000 GB 1 na dk 5 za mitandao yote siku 3
 
Back
Top Bottom