Matatizo ya Kampuni ya Zantel Tanzania

Matatizo ya Kampuni ya Zantel Tanzania

Ferruccio Lamborghini

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2020
Posts
1,667
Reaction score
2,625
Matatizo lukuki yanayokumba ni pamoja na:


1. KIFURUSHI CHA BMP
Yaani kifurushi cha BONGA MPAKA BASI ndio mnakiona cha maana sana kuliko hata MB na SMS!
Yaani mtu aweke 3000 apate dakika 220 SMS 50 na MB 50.
Kwa kweli hapa mmefeli.


2. SPIDI YA INTANETI
Hapa kwenye spidi niseme kweli mpo vizuri
Kazeni kamba maana hata Vodacom Tanzania wapo vizuri kuliko mtandao wowote mkifuatia nyie Zantel.

3. KUSHINDWA KUSIKILIZA MAONI YA WATEJA
Sijui mnakwama wapi? Yaani hata wateja wakiwapa maoni kuhusu maboresho ya vifurushi mnawapuuzia.
Hata huduma ya kuwasiliana na wateja kwa njia ya WhatsApp hamna?
Tena pale Makao Makuu yenu ya jirani na ubalozi wa USA, watoa huduma wana nyodo sana.
Yaani wanakujibu kama vile wanakusuta.

4. VIFURUSHI VYA USIKU
Hapa msinibishie kabisa, hamna kufurushi chochote kile cha intaneti cha usiku kuanzia saa 6 mpaka saa 12.
Wenzenu TTCL na Halotel hizi huduma wanazo na tunaenjoy sana usiku.
Fanyeni mpango mtupatie hata
>>> GB 1 kwa 500 saa 6 usiku hadi saa 12 asubuhi.
>>> GB 3 kwa 1000 saa 6 mpaka saa 12 asubuhi.

4. VIFURUSHI VYA CHUO
Ukipiga *148*05# kisha ukichagua Vyuo vya Bara
Aisee kama simu yako mnara unasoma 3G, H, H+ au 4G lazima igome kujiunga na kifurushi.
Mpaka uende kwenye setting useti mnara usome 2G kisha ujaribu kujiunga tena ndio itakubali ila kwa mbinde.

5. KERO YA SMS ZA OFA
Yaani nyie kwenye ustaarabu ni 0.3% yaani mnatuma SMS za ofa ovyo mpaka najifikiria kuwatukana.
Yaani kwa siku mnatuma SMS 12 yaani wastani wa kila saa mnatuma tu SMS.
Yaani hapa nilipo laini yenu nimeitoa kwenye simu ipo kwenye kabati sababu ya ujinga huu.

6. VIFURUSHI VYA SMS
>>Tsh 500 mnatoa SMS 150 saa 24
>>Tsh 1000 mnatupa SMS 500 wiki
>>Tsh 3000 mnipe SMS 2000 kwa mwezi!

Hapa mmefeli vibaya mno, yaani vibaya mno.
Nendeni mkajifunze hata kwa Vodacom Tanzania

7. VIFURUSHI VYA INTANETI HAVINUNULIKI
Ni bei mno jaribuni kukaa chini mshushe hiyo bei.
Waangalieni Halotel, TTCL na kidogo Airtel.
Nawapenda sana Zantel, tatizo mna vifurushi ghali sana.

Kwa staili hii mtapoteza wateja, mtafilisika na hatimaye mtarudi Visiwani kuimba Taarab na Kaswida kama sio kuuza urojo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Suala la vifurushi limekuwa mtihani, hawa airtel wana kifurushi cha bei poa lakini ukijiunga hiyo netweki itakufanya uishie njiani uende "ukapigwe" tu na voda kwa vifurushi vya sh 2000, na pesa uliyoweka kule airtel ndio hivyo imeenda.
 
Suala la vifurushi limekuwa mtihani, hawa airtel wana kifurushi cha bei poa lakini ukijiunga hiyo netweki itakufanya uishie njiani uende "ukapigwe" tu na voda kwa vifurushi vya sh 2000, na pesa uliyoweka kule airtel ndio hivyo imeenda.
Watu wanaongelea zantel ww unaibuka na mada yako ya voda na airtel....totally OP
 
Back
Top Bottom