Matatizo ya figo yanakua kwa kasi Nchini Tanzania, sasa ni 6%

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Imeeleza kuwa matatizo ya magonjwa ya figo ni tatizo la Kidunia kwa kuwa takwimu za magonjw aya figo ni 10% wakati ndani ya Tanzania takwimu za nchi ni 6%

Serikali inajipanga katika mambo mengi, kwanza ni kutoa elimu ya afya mfano kula na mazoezi, pili kuna usalama wa chakula na usalama wa dawa.

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amesema hayo Bungeni leo Juni 21, 2022 ambapo ameshauri watu wote wanatakiwa kuwa wadau hasa katika suala la chakula.

Kuhusu elimu shuleni amesema wanashirina ana Wizara ya Kilimo na Elimu katika kutoa elimu kwa umma.
 
Wasiache kutoa elimu hata kwenye vilevi na jinsi vinavoweza kuchangia hilo tatizo.
 
hizo pombe kali tunakunywa huku uswazi tukiamini nikutoka kwa mabeberu na zimezingatia viwango, nyingi ni fake na zinatengenezwa uswazi kienyeji.

Walevi wenzangu wa pombe kali, tuchukue tahadhari sana, hizi J. Walker, Teachers, Black labbel, Jack Daniel Tennessee nyingi ni made Buguruni nk.
 
Serikali ipambane na pombe kali fake mitaani. Pia isambaze maji safi vijijini. Mtu anakunywa maji chafu (hard water) ya visimani maisha yake yote. Kula vizuri na mazoezi vs. BP
 
Chanzo kikuu..ni vinywaji vya viwandani mapombe makali ba hizi juisi kama energy na soda.

Pia matumizi hovyo ya madawa..self description of medicine nalo ni moja ya tatizo kubwa.

#MaendeleoHayanaChama
 
Imeeleza kuwa matatizo ya magonjwa ya figo ni tatizo la Kidunia kwa kuwa takwimu za magonjw aya figo ni 10% wakati ndani ya Tanzania takwimu za nchi ni 6%

Serikali inajipanga katika mambo mengi, kwanza ni kutoa elimu ya afya mfano kula na mazoezi, pili kuna usalama wa chakula na usalama wa dawa.

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amesema hayo Bungeni leo Juni 21, 2022 ambapo ameshauri watu wote wanatakiwa kuwa wadau hasa katika suala la chakula.

Kuhusu elimu shuleni amesema wanashirina ana Wizara ya Kilimo na Elimu katika kutoa elimu kwa umma.
Unakuta MTU anakunywa jagi zima la maji ya alovera ahhagh
 
Matatizo makuu ya figo chanzo ni maji tunayokunywa.

Tujiulize,haya maji ya chupa tunayokunywa,na maji ya DAWASCO hayo madawa wansyoweka yana usalama kiasi gani
 
Back
Top Bottom