Umekuwa msemaji wa CCM kwamba walikwambia walitaka kutumia mfumo wa CDM. Lakini hebu nisaidie mimi mbumbumbu, ilikuwaje habari hii ya CCM kutamani mfumo wa CDM hukuiweka hadharani ahdi leo unapigwa dongo ndio unaitoa? au ndio huku kumwaga mchuzi na ugali?
Uteuzi wa wabunge wa viti maalumu ulifanywa na CHADEMA? Acha porojo zako wewe kama hufahamu uliza ujibiwe. Kwa taarifa yako mfumo uliotumiwa na CHADEMA kupata wabunge wa viti maalumu hata ccm wanatamani kuutumia ila tatizo ni chama chao kumilikiwa na fikra za mwenyekiti wao "zidumu fikra za mwenyekiti".
CHADEMA walikabidhi kazi ya uteuzi wa wabunge wa viti maalum kwa jopo la maprofesa wa chuo kikuu. Wao walichofanya ni kuainisha sifa za wabunge wanaowahitaji tu.
Kama CHADEMA wangefanya uteuzi kwa upendeleo kama unavyotaka kutuaminisha, hata wengine waliotaka kupata nafasi hizo wangelalamika sana. Mfano mzuri ni pale alipofarike Regia Mtema nafasi yake ilizibwaje? Uliza ujibiwe acha kubwabwaja tu ili mradi uiingize buku saba. Tumbo litakuponza.
CCM wenyewe wanatambua utaratibu uliotumika kuwapata wabunge wa CHADEMA ndio maana wanakaa kimya na walishawahi kushauriana kutumia mfumo kama huo tatizo ni kwamba viongozi wanatumia nafasi ya viti maalum kuwapatia wapenzi wao ulaji.