Matatizo ya CHADEMA haya hapa

Matatizo ya CHADEMA haya hapa

CCM safii ...haina matatizo kabisa....ccm inajenga nchi...safi sana
 
Mkuu uelewa wako ni mdogo sana hata kuandika hujui.. Hapo lumumba wamekupa bei gani? Acha umbulula.. Kakojoe ukalale... Hapa ni mziki mkubwa...
Habari wa JF.
Naomba nitaje matatizo ambayo yako CHADEMA.

1. Kupeana Ubunge kwa kujuana, e.g viti maalumu
Ndesamburo vs Lucy Owenya
Mbowe vs Grace Kihwelu
Lissu vs J.Lissu(Dada yake tumbo moja)
Zitto vs mtoto wa shangazi yake

2. Ukiwa mchaga ni rahisi kupewa Cheo au Jimbo la uchaguzi tena bila hata kura za maoni.


3. Kudhani kila wakati ndio chama kikuu cha upinzani wakati kuna vyama vingine. Na hata
nccr mageuzi ya Mrema ilikuwa hivyo hivyo.

4. Kila wakati wanadhani wanaonewa hata kwenye mambo yasio ya msingi au yasiyo na maslai
kwa taifa hili.

NAOMBA MBADILIKE.


NB: SIASA CI SULUHISHO SAHIHI LA MATATIZO YETU.
 
Du! Kweli chadema ni noma!kimewashika mpaka ndani ya matumbo yenu!
 
Vita kawawa na Dada yake Zainabu kawawa..Samweli Sita na Mke wake!
Ungetoa ufafanuzi ili tukuelewe ndugu (Hili ni Jukwaa la 'Greater Thinkers') jinsi hao wanavyopeana hayo madaraka si kufanya ulinganisho tu, mfano Lissu VS dada yake. Mbona vyama vingi hizo 'VS' zipo? Mfano Makamba Sr VS Makamba Jr. Onyesha nawe ni miongoni mwa 'GT'
 
hawa member waliojiunga june 2013 si bure , wapo humu kwa kazi maalumu kutoka kitengo maalumu cha watu maalumu wenye maslahi maalumu kwa Taifa hili na kundi fulani maalumu humu Jukwaani. Tuwaogope kama ukoma kwani Tusipoangalia tutakuwa tunacheza ngoma zao maalumu ,kututoa katika mambo muhimu na ya msingi humu.
 
Umekuwa msemaji wa CCM kwamba walikwambia walitaka kutumia mfumo wa CDM. Lakini hebu nisaidie mimi mbumbumbu, ilikuwaje habari hii ya CCM kutamani mfumo wa CDM hukuiweka hadharani ahdi leo unapigwa dongo ndio unaitoa? au ndio huku kumwaga mchuzi na ugali?
Baadhi ya wajumbe wa kamati kuu walitamka wazi katika vikao vya chama walipokuwa Dodoma katika vikao vyao. Ukitaka chukua, kama hutaki acha.
 
Back
Top Bottom