Matatani kwa kuwinda katika shamba la Mugabe

Matatani kwa kuwinda katika shamba la Mugabe

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,100
Reaction score
34,915
140701155155_mugabe_304x171_bbc_nocredit.jpg

Rais Robert Mugabe


Jirani yake Rais wa Zimbabwe Robert, ametozwa faini kwa kuwinda katika shamba la ras huyo.
Mahakama ilimuauru Michael Pazarangu, ambaye aliwapeleka Mbwa wake kuwinda mnyama
anayejulikana kama Mbawala au 'Deer' katika shamba la Mugabe, kulipa faini ya dola 50 au afungwe jela kwa siku thelathini.


Kwa mujibu wa gazeti la serikali la Herald, Bwana Pazarangu alituhumiwa kwa kuwaruhusu Mbwa wakali kuingia katika shamba binafsi la Rais Mubage, mjini Harare.


Mugabe ambaye ana umri wa miaka 90, amekuwa mamlakani tangu Zimbabwe kujitawala 1980.

Alichaguliwa tena mwaka jana na kumshinda hasimu wake wa jadi Morgan Tsvangirai.

Mtuhumiwa Pazarangu, alikiri kosa lake kinyume na alivyokuwa amesema hapo awali ambapo alikanusha madai hayo.


"kesi hii imewagusa watu wengi na imeniathiri sana,'' alinukuliwa akisema Bwana Pazarangu

Mahakama iliambiwa kuwa Mbwa wa mtuhumiwa walimuua Mbawala katika shamba la Mugabe mwezi Mei mwaka 2013 katika eneo la Borrowdale .

Mbwa hao walisemekana kuingia katika shamba la Mugabe kupitia ukuta unaogawanya nyumba za wawili hao.chanzo.Matatani kwa kuwinda katika shamba la Mugabe - BBC Swahili - Habari
 
inanikumbusha king"s deer kwenye robin hood.
 
Back
Top Bottom