Matata ya mbu! Anajuaje hili ndio sikio?

Matata ya mbu! Anajuaje hili ndio sikio?

Pia mm haka kamdudu mbu huwa kananiacha hoi. Unaweza kuwa serious na mambo yako, mfano mm huwa nakesha mara kwa mara, sasa ataganda sikioni au usoni (mtazamane),unaingiwa na hasira unaanza kupiga makofi, mwisho wa siku unaonekana mpumbavu kwenye nyumba ya watu kupiga piga makofi usiku wa manane...kwahyo njia nzuri ni kuwasha feni, ila cha maana feni kali ndo humfukuza na pia mwanga, sasa imagine usiku kuchwa upo kwenye mfeni mwanga mkali wa taa...kwakifupi huyu kiumbe kaumbwa kutukomoa. hana faida na hana hasara (meaning anaweza kukusaidia uwe macho ufanye mambo yako)
 
Ukitaka uepuke usumbufu wa Mbu sikioni lala karibu na soksi zako chafu ulizovaa siku nzima,hakika utakuwa salama...
Kuna mbu wana tabia za mende ujue kama binadamu tu
In fact kuna mbu hupendelea zaidi damu ya kalio kwa wale walala utupu[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
hofu kuu ya mkubwa ni kuchekwa!!! jsmbo ambalo hawezi kulikubali

Amuondoe mbu ili mmcheke! never!!!

licha ya madudu anayofanya ataendelea kumkumbatia ili msije mkamcheka
 
Sasa tufanyeje Mshana, maana tushajipiga makofi hadi tumezirai na wengine kufa kabisa, kinachotuudhi ni ile sauti yake inatusumbua, sasa tutumie yale mambo yako ya vilingeni, au tuendelee na mfungo?
 
Unaweza kumuita ndio kiumbe msumbufu zaidi akiamua kukukosesha usingizi... Nafahamu una kiroboto na kunguni pia... Duniani wawili wawili.. Lakini mbu ni kiboko, atakujia toka atokako direct mpaka kichwani halafu sikioni? Na udogo wake wote huo sijui werevu huu kaupata wapi.. Anajuaje hili ni sikio? Aje avumie hapo na kisauti chake chembamba kikali?
Ukistuka ukarusha kofi utaishia kujipiga mwenyewe... Yeye huyoo krshasepa kitambo

Pamoja na wepesi wake wa kukwepa makofi yanayoweza kumletea umauti wa hapohapo.. Waswahili wanasema bila hata kuomba maji, na werevu wake wa kujua pa kupigia kelele lakini anaweza pia kuwa kiumbe **** mpumbavu zaidi.,. Akikupigia kelele sikioni isiporusha mkono ama kustuka anajua wazi huyu kalala fofofo... Hivyo hujichagulia artery nene iliyojaa vizuri damu na kutumbukiza mrija wake hapo.... Ujuha wake unakuja hapa hatafyonza kiasi cha kushiba tu ili abaki na wepesi wake wa kubaki na kasi ya kukwepa shambulio... Atajisahau na kufyonza mpaka kitumbo kiwe ndindindi... Atafyonza mpaka avimbiwe kabisa na kushindwa kuruka hata pima moja ama akiweza ni kizembe mno na kwa kasi ndogo kabisa....
Mtoto mtukutu kawa kama mbu... Mbu akishavimbiwa hata kuvuma hawezi tena! kupayuka kumepungua kabisa, miruko ya huku na kule huisikii tena... Zile kelele za kila usiku kama kule mawingu haziko tena!
Kala kavimbiwa... Wepesi na ujasiri wa kuruka tena haupo! kifuatacho kinajulikana

By the way (hii ni nje ya mada) hivi kuna mbu chapombe? Kamwe hamwendei ambaye sio mlevi.... Starehe yake ni damu ya mtu aliyetoa lock[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Cha kuongezea mbu ndio kiumbe hatari kuliko wote Duniani


ila nimekuelewa hapo mwisho, ngoja tuone kofi litakalompata huyu "mbu" kama litamuua
 
Sasa tufanyeje Mshana, maana tushajipiga makofi hadi tumezirai na wengine kufa kabisa, kinachotuudhi ni ile sauti yake inatusumbua, sasa tutumie yale mambo yako ya vilingeni, au tuendelee na mfungo?
Ngoja mfungo uishe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom