Matarijio ya wengi ni Samatta achangie zaidi kama Ronaldo na Messi

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,310
12,606
Sio kwamba Samatta hatoi mchango kwa taifa lakini mchango wake hautoshi kabisa. Kule Ulaya anaitwa Samagoal lakini Taifa stars anaitwa Samaassist. Hiki ndicho watu wasichokitaka. Mafanikio ya Ronaldo na Messi ni pamoja na kupachika magoli kwenye mataifa Yao na kuamua matokeo.

Tumuombee Samatta afanye zaidi kuliko anavyofabya Sasa. Maana yeye ndio kaka yetu mkuu uwanjani kutokana na mafanikio aliyoyapata. Anatakiwa aweke rekodi yake kwenye timu ya Taifa ambayo itadumu kwa muda mrefu bila kivunjwaa.
 
Sammata sifa zilizidi hapo nyuma na akaanza kujikuta level yake ni kubwa sana hadi kwenye timu ya Taifa, akawa hajitumi sana

Simon Msuva akachukua jukumu la kustruggle ili stars ipate matokeo kwa kila mechi hukumu samatta akibaki kuwa mzungukaji tu uwanjani

Now ndio ameanza kushtuka baada wabongo kuanza kumsagia kunguni sana, ndio effort unaanza kuziona uwanjani tena anatumia energy kubwa sana

Ila tofauti na hapo aache kujiona special sana kwa timu ya Taifa
 
Anachezea na wachezaji wa aina gani
Sio kweli timu inatengeneza nafasi ambazo hazitumii. Wachezaji anaocheza wanamtengenezea nafasi za wazi ambazo yeye hazigeuzi kuwa magoli. Unataka acheze na wachezaji wa kumfanyia nini.
 
Acha uongo nafasi gan ya wazi katengenezewa hv karibuni
 
Ingia kacheze wewe..mijitu ya vyeti feki bhana!
Dua mbaya za wananchi zinampanda kichwani. Yeye anatunza miguu yake isivunjie taifa stars ili ikavunjikie huko kwa wakoloni wetu. Huu ni ulimbukeni wa hali ya juu.
 
Naamini kwamba tatizo kubwa la Samatta ni mafanikio yake aliyoyapata katika mchezo huu na naweza kulieleza hilo katika namna mbili. Kwanza kwa kutumia mfano ambao washabiki wa soka wa Tanzania wanaweza kuuelewa vizuri zaidi na pili mfano ambao unaweza usieleweke vizuri.

Mfano wa kwanza unamhusu mchezaji Simon Msuva. Kwa bahati nzuri mimi ni mpenzi wa masuala ya mbinu na mikakati ya uwanjani na nilikuwa nikisikiliza sana mawaidha ya makocha wa Simba katika mechi zote ambazo ilikuwa inacheza na Yanga.

Karibu makocha wote wa Simba walikuwa wanasisitiza namna ya kuwazuia Haruna Niyonzima na Simon Msuva wasiwe na madhara.

Ilikuwa inajulikana kwamba endapo timu itaruhusu Msuva na Niyonzima watawale mechi, hali itakuwa mbaya. Matokeo yake yakawa kwamba katika mechi dhidi ya Simba, Msuva akawa hatambi sana. Yakaanza maneno kwamba yeye ni shabiki wa Simba na ndiyo huwa hachezi vema dhidi ya Simba.

Washabiki hawa hawakuwa wakijua kwamba Simba na makocha wake ndiyo wamemfanya Msuva na wakati mwingine Niyonzima washindwe kucheza. ili pia ndilo jambo ambalo limekuwa likimkuta Samatta katika miaka ya karibuni. Mbwana huyu wa leo si yule wa miaka sita hadi minne iliyopita ambaye timu zilikuwa hazimjui.

Leo hii, kila timu inayocheza na Stars inajua ina mchezaji anayeitwa Samatta. Wakati wote wa kujiandaa na mechi zetu, huwa wanakuwa na mikakati ya kuhakikisha nyota wetu huyu anakuwa na athari kidogo kwenye mechi. Kila kocha anakuwa na maelekezo yake kuhusu ni kwa vipi watamdhibiti.

Bado hawajajua sana kumhusu Msuva, Ditram Nchimbi au Iddi Nado. Lakini sasa wanajua kila kitu kuhusu Samatta na ni jambo la akili kwa washabiki na wachambuzi wa soka kufahamu kwamba hiki ni kitu kitakachokuwa endelevu katika miaka inayofuata mpaka nyota huyu wa Genk atakapoamua kutundika daluga zake.

Kwa hiyo hiyo ni sababu ya kwanza na ambayo kwangu ni ya msingi zaidi. Umaarufu wa Samatta utasababisha achungwe zaidi lakini hiyo sasa itatoa fursa kwa akina Msuva kuchomoza. Siku ambayo Msuva naye atakuwa maarufu, tutarajie kumwona akiwa tofauti na alivyo sasa; kama vile Simba na timu za Tanzania zilivyokuwa zikimchunga akiwa Yanga.

Sababu ya pili inahusu sana staili ya uchezaji na tabia ya Samatta. Wengi wa washabiki wa soka bado wanaamini kwamba nahodha ni mtu anayetakiwa kuwa mpambanaji, mlalamishi uwanjani na mtu anayezungumza na kusukuma timu mbele kila wakati. Bahati mbaya ni kwamba Samatta si wa aina hiyo.

Yeye huongoza timu kwa uwezo wake tu uwanjani. Wakati wa mechi dhidi ya Guinea ya Ikweta, Erasto Nyoni alikuwa akizungumza zaidi na waamuzi na kupiga kelele kuliko Samatta ambaye wakati mwingine alikuwa akionekana kujiinamia. Lakini utulivu na ukimya wa Samatta ndiyo imekuwa tabia yake miaka yote tuliyomfahamu. Yeye huacha miguu na kichwa chake vizungumze uwanjani.

Na Samatta, kama walivyo wachezaji wengi wenye vipaji halisi; si aina ya wachezaji wa kukimbizana na kugongana na wenzake uwanjani. Hawa vijana wa Kizaramo na Kindengereko wanaojua mpira wanapenda kucheza mpira tu na si kufanya kazi nyingine za kutumia nguvunguvu.

Hilo wanawaachia akina Elias Maguli, Ditram Nchimbi, Thomas Ulimwengu na wengine ambao Mungu hajawapa kipaji halisi cha kusakata mpira lakini kawapa moyo na mapafu ya kupunguza kile wanachokikosa kwenye uwezo halisi wa kusakata soka.

Kwa hiyo, kumhukumu Samatta kwa sababu hakimbii sana au kupambana huku na kule ni kumwonea. Yeye ana jukumu lake na sehemu kubwa ya jukumu lake liko katika eneo la hatari la wapinzani. Ni sawa na leo mtu aanze kumhukumu Lionel Messi kwamba hakabi anapokuwa uwanjani. Hilo si jambo analoliweza sana uwanjani.

Kwa hiyo tatizo kubwa la Samatta ni mafanikio yake mwenyewe yanayosababisha awekewe mikakati ya kukabwa na timu pinzani na pia kwa washabiki kutegemea makubwa zaidi kutoka kwake kwa sababu sasa wanajua kuwa wana nyota wa kiwango cha juu.

Ni changamoto ambayo Mbwana Ally Samatta anatakiwa kuipokea na kuibeba kwa mikono yake miwili. Wanasema tembo anaponzwa na mkonga wake.
 
Unapokuwa unachungwa sana na timu pinzani ndio hapo unapotakIwa kuonyesha umahiri wako kuwa wewe ni mchezaji mkubwa sawa na walivyomchukulia. Yule mchezaji wa Benin aliyetufunga hapa BAO 1 alilifunga lile BAO kutokana na uwezo wake mkubwa kwakuwa alikuwa amekabwa na wachezaji wetu 3. Msuva kule Benin alilifunga lile BAO kama yeye kutokana na uwezo wake mkubwa.

Hata akina Messi, Ronaldo, Beckham, Drogba, na wengine wanakamiwa pia na timu pinzani lakini wanazisaidia timu zao kuamua matokeo kama timu na kama wao. Huyu wa kwetu anacheza uwanjani huku anafikiria timu yake. Hivyo anaogopa kuumia au kupata kadi.
 
Unapokuwa unachungwa sana na timu pinzani ndio hapo unapotakuwa kuonyesha umahiri wako. Yule mchezaji wa Benin aliyetufunga hapa BAO 1 alilifunga lile BAO kutokana na uwezo wake mkubwa kwakuwa alikuwa amekabwa na wachezaji wetu 3. Msuva kule Benin alilifunga lile BAO kama yeye kutokana na uwezo wake mkubwa.

Hata akina Messi, Ronaldo, Beckham, Drogba, na wengine wanakamiwa pia na timu pinzani lakini wanazisaidia timu zao kuamua matokeo kama timu na kama wao. Huyu wa kwetu anaocheza uwanjani huku anafikiria timu yake. Hivyo anaogopa kuumia na kupata kadi.
Sahihi mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom