Mbwana Samatta na App ya SamaPay - Haya ni mapungufu niliyoyaona

southern boy

Member
Jan 12, 2016
43
125
Habari za humu!!

Kipindi cha siku mbili zilizopita nimeona matangazo na baadhi ya video za youtube zikielezea kuhusu hii app ya SamaPay ambayo imeanzishwa na mchezaji wa mpira wa miguu Mbwana Ali Samatta.


Kwanza ningependa kutoa hongera kwa uamuzi wake huo wa kufikiria na kufanya kitu ambacho kidogo kipo utofauti na jambo lililomletea umaarufu (mpira).

Mimi pia ni android App Developer ila huwa na fanya kama hobby. Haya chini ni baadhi ya mapungufu ambayo nimeyaona kwenye app hiyo na mengine ni mawazo yangu.

Mara nyingi kabla sijadownlaoad app yoyote huwa naangalia reviews pia nikiona kama app ina stars less than 4.0 mara nyingi huwa siidownload. Lakini app hii (samapay ) imekua rated na watu 9 tu (mpaka mda huu naandika hii post). Na katika hao tisa wametoa reviewes mbaya mpaka kupelekea app ikawa na 2.3 stars (mpaka mda naadika hii post).

Pia nikikuta app ambayo imekuadeveloped au imeanzishwa na Mtanzania huwa lazima niipakue ili kuunga mkono na pia kuona Watz tunafanya nini. Twende moja kwa moja kwenye mawazo yangu kuhusu SamaPay.

App sio 'user friendly' kwa upande Phone number. Jambo hili ndio limepelekea mpaka baadhi ya watu kushindwa ku-sign up (according to reviews) pamoja na mimi pia nimeshindwa. Developer angeweka tu simple sign up ya phone number kama kwenye names.

WhatsApp Image 2020-09-12 at 14.16.31.jpeg

Kwenye phone number haijulikani mtu aanze na 255714***** au 0714******. Ingawa nilijaribu kwa options zote pia imeshindikana ku-sign up.

Yaani pia hata ukiweka '111' inasema tu 'verification code sent ...' bila hata kuangalia kama phone number ipo sahihi au lah. Nimeandika 111 phone kisha verification code '123456' inasema verification has been confirmed ila imeshindikana kuendelea mbele.

Pia mtu akijaza kila kitu alafu akabofya 'Verification' inasema tu 'agreement' kidogo ingeatoa maelezo kwamba may be 'You have to agree on terms of service and privacy above' ili moja kwa moja mtu ajue nini cha kufanya.

Hizo terms of service na privancy zipo kwa lugha ya Kikorea. Nikazifanyia mpango nizi translate into English nikakuta ni Terms na privacy policy za KSnet Co. Ltd (nahisi huyu atakua ndio developer) na sio terms na privacy za SamaPay.

Data ikiwa off halafu ukaingia kwenye app inakuletea vitu ambayo sio vzuri kwa mtumiaji kuviona.


WhatsApp Image 2020-09-12 at 14.30.54.jpeg

Huyo developer naweza sema amefanya kitu ambacho ni very beginner in apps development. Mimi pia nishawahi kutumia 'Webview' katika baadhi ya app nilizotengeneza. Data ikiwa off haikutakiwa kuletewa kitu kama hicho (angali picha juu ) kwa mtumiaji kama ilikua haina jinsi kwa developer kutumia webview (kuingiza page ya website kwenye android app). Labda sababu hakutaka kuunganisha firebase database which is a very best option (kwangu mimi) na kuachana na webview kwa upande wa siging up.

Halafu kwangu sio kitu kizuri kwa developer kukupa sub-domain (samapay.kspoint.co.kr/). Kwa kiasi cha chini ya 200,000 (laki mbili) ungeweza kupata domain nzuri kwa ajili ya project ya samapay mfano samapaytz.com, samapayafrica.com, au pia ungechukua samapay.com (jina hili nimelicheki ili kulipata kidogo ni ghali may be milioni 2).

Nyongeza 1. Kabla ku-lunch app ni kuhakikisha inatestiwa kwenye android version zote ambazo developer alikubali. Nikiongea Ki- Android App development ni kuwa kama minimum sdk aliweka android 5.0 (Lolipop) basi app itestiwe kwenye devices tofauti kuanzia android 5, 6, 7, 8, 9 ,10 ,11 na 12 (kama imetoka). Ingawa kwa upande wangu 9 mpaka 11 hazisumbuagi ila 8 na 6 zinazingua sometimes.

Nyongeza 2. Iyo atcivity ya sign up kipindi inaload bas hata angeweka kitu kuonyesha app inload kitu sio unaona white blank.

Nyongeza 3. Baadhi ya makosa ya developers wengi kipindi wanadevelop app na kui-test, huwa wantest kama developer na sio kama mtumiaji. Just try all scenarios kama mtumiaji.

Sijaweza kuifanyia review zaidi sababu nimeshindwa ku-sign up na kuingia ndani zaidi sabab kila mda inaleta sign up.

Ni hayo tu.
 

racka98

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
245
250
Ishatupa NullPointException. Sema sijui hata phone number ya nini kma ukibonyeza verify inasema ingiza 12356.

Ila kweli User Experience ni mbovu sana. Kuna sehem zingine kuna kijapan. Na inaonekana kma vile app bado ipo kwenye testing.

Screenshot_20200912-173731_SamaPay.jpg
 

de carter jr

Senior Member
Aug 27, 2014
130
250
Mi mwenyewe nilijaribu kuitest hii app lakini nimeona ina mapungufu mengi sana na sijui kwa nn ameiachia wakati huu kwanza huwezi kuilink na kadi yyte ya bank au mobile money hzi mpesa nk.....
kwenye sehemu ya kuscan ulipie kwa kuscan Qr code hamna kile ki camera cha kuscan
ki ufupi app haieleweki nahisi kwakua hajui mambo ya technology ndio maana hajaelewa kilicho fanyika alafu ina stack kwl
IMG-20200910-WA0060.jpg

IMG-20200910-WA0055.jpg
IMG-20200910-WA0057.jpg
IMG-20200910-WA0056.jpg
 

southern boy

Member
Jan 12, 2016
43
125
Ishatupa NullPointException. Sema sijui hata phone number ya nini kma ukibonyeza verify inasema ingiza 12356.

Ila kweli User Experience ni mbovu sana. Kuna sehem zingine kuna kijapan. Na inaonekana kma vile app bado ipo kwenye testing.


Kweli ipo kwnye testing lakin hakutakiwa kuitangaza kiasi kile. Angewapa tu baadhi ya watu privately waitest. Sabab kaitangaza hotel ya Hyatt kama sijakosea
 

Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
3,124
2,000
Kweli ipo kwnye testing lakin hakutakiwa kuitangaza kiasi kile. Angewapa tu baadhi ya watu privately waitest. Sabab kaitangaza hotel ya Hyatt kama sijakosea
Hii inawea mpotezea watumiaji maana mtu akiidownload ikamlet down atakuwa tayari ashakuwa na bad experience na hii app hatoitumia tena
 

Stefano Mtangoo

Verified Member
Oct 25, 2012
4,165
2,000
Sometimes bongo huwa hatufikiri user experience na first impressions
Itakuwa shida ya Consultant aliyempata ndio amemuangusha. Maana sidhani kama ana utaalam binafsi na haya mambo. Lazima atakuwa anatumia jamaa au third party consultant.

Whoever amepewa kazi hii hakumtendea haki. Haswa ukiangalia brand ya jina lake ambayo katumia jasho jingi kuijenga. Hope wata fix na kuja na kitu Pro!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom