mpasta
JF-Expert Member
- Jan 17, 2011
- 919
- 2,007
Leo nimekumbuka Miaka ile ya 90's Nchini Tanzania kulibuuka utapeli wa ajabu sana mpaka mwanamuziki HEMEDI MANETI wa bendi ya CCM ya Vijana Jazz akatunga wimbo unaitwa "OGOPA MATAPELI".
Mwaka 1993 nikiwa mkoani nakumbuka kuna tapeli aliwaliza watu balaa. Timu ya SIMBA SC ilikuja Mkoani Mtwara kucheza na timu ya Bandari Mtwara. Sasa baada ya mechi usiku wake washabiki wa Simba wakaandaa hafla ya kuwapongeza Simba SC hasa ukichukulia mwaka huo Simba SC alikuwa anafanya vizuri kwenye mashindano ya CAF.
Tapeli mmoja mgeni machoni kwa watu nae akatinga kwenye sherehe na tracksuit zake nyekundu nadhifu, akajichanganya kwenye umati wa washabiki.
Dada mmoja mrembooo akajilengesha, maana alikuwa anamtafuta mchezaji wa SIMBA akiitwa DAMIAN KIMTI, alikuwa anampenda sana kwa uchezaji wake. Enzi zile hamna TV, hamna magazeti ya kutosha, Mastaa unawajua kwa jina tu kupitia Redio

.
Jamaa akamdanganya dada wa watu yeye ndio DAMIAN KIMTI akala uroda wa bure kwa dada yule. Kesho yake asubuhi na mapema jamaa akaibukia sokoni na makapu yake akiwa amevalia tracksuit zake nyekundu anatembea kwa machejo kama mchezaji mpira kweli. Watu wanaonyesha kwa vidole KIMTI yuleeee anapita KIMTI yuleee, basi sokoni anapewa tu mchele, maharage na bidhaa zinginezo bure kwa jina la KIMTI kumbe KIMTI feki.
Sasa balaa likaibuka, Simba wameshasafiri kurudi DSM kuendelea na mechi zao,KIMTI feki bado anaonekana mtaani hasafiri, ndipo dada wa watu uzalendo ukamshinda akamchana hadharani, "Nimekupa uroda nikijua ninampa uroda DAMIAN KIMTI kumbe mshenzi tapeli tu wewe"....

Kila zama na kitabu chake, zama hizi za Kidigitali matapeli wanakutapeli kwa njia za kidigitali mara nyingi wala huwaoni ila zama zile lazima muonane uso kwa uso hivyo walikuwa wanatumia akili nyingi sana....
Je umeshawahi kutapeliwa na wewe mpaka ukajiona ni mjinga??

Mwaka 1993 nikiwa mkoani nakumbuka kuna tapeli aliwaliza watu balaa. Timu ya SIMBA SC ilikuja Mkoani Mtwara kucheza na timu ya Bandari Mtwara. Sasa baada ya mechi usiku wake washabiki wa Simba wakaandaa hafla ya kuwapongeza Simba SC hasa ukichukulia mwaka huo Simba SC alikuwa anafanya vizuri kwenye mashindano ya CAF.
Tapeli mmoja mgeni machoni kwa watu nae akatinga kwenye sherehe na tracksuit zake nyekundu nadhifu, akajichanganya kwenye umati wa washabiki.
Dada mmoja mrembooo akajilengesha, maana alikuwa anamtafuta mchezaji wa SIMBA akiitwa DAMIAN KIMTI, alikuwa anampenda sana kwa uchezaji wake. Enzi zile hamna TV, hamna magazeti ya kutosha, Mastaa unawajua kwa jina tu kupitia Redio

.Jamaa akamdanganya dada wa watu yeye ndio DAMIAN KIMTI akala uroda wa bure kwa dada yule. Kesho yake asubuhi na mapema jamaa akaibukia sokoni na makapu yake akiwa amevalia tracksuit zake nyekundu anatembea kwa machejo kama mchezaji mpira kweli. Watu wanaonyesha kwa vidole KIMTI yuleeee anapita KIMTI yuleee, basi sokoni anapewa tu mchele, maharage na bidhaa zinginezo bure kwa jina la KIMTI kumbe KIMTI feki.