matapeli wa mapenzi tanzania

Smile

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
15,347
11,610
mabinti mabinti mabinti hii ni kutoka kwa wadada wafanyakazi tanzania(wwt)
kunawimbi la vijana especially wa chuo wanapenda kushobokea wadada wanaofanya kazi.inakuwa ni kazi kwako kumlipia ada,akae kwako.umlishe umvishe na mapenzi umpe.akimaliza chuo mapenzi kwishney
nimeshuhudia wadada watatu wapo kwenye huu mtego.vijana wenyewe hawajatulia wala nini.kuna mdada wa kwake kampa na gari kabisa,.asubuhi wanaondoka wote hme kwa mdada anamwacha mdada job anampitia demu wake wa chuo haooo chuo kwa raha zao
na katika tafiti zilizofanywa hapa mjini wanaume wanaopenda kulelewa ni wa iringa,songea,sumbawanga na singida. matapeli wa mapenzi.
mimi wachaga,wapare ,wasukuma,wagita.wahaya pamoja saaaana na nyie wakuu. mimi na nyie damdam huko sumbawanga aku babu
ila ushauri wangu kwa wanawake wenzangu
msipende kufanya maisha kuwa magumu,sio kwamba mtafute watu wenye kipato la maisha ni popote
msiwe na pupa kutafuta wapenzi usipanic by the way sio lazima.ishi maisha yako jinsi utakavo na sio watu watakavo. maisha ni haya haya furahia maisha
hv utaakaaje na mtu akupi furaha moyoni?
unaishi na mwanaume nyumbani kwako hana hata future na wewe ,kwanza anakupatia aibu kwa ndugu zako,mwenyewe si mkaaji kesho anaondoka utaweka wapi sura yako
mimi namshukuru sana mungu kwa busara alionijalia mimi siwezi kuishi na mwanaume kinyumba iwe kwangu au kwake
kama mwanaume ana malengo na wewe afate taratibu .huu ulimbukeni jamani unawacosti wanawake.
mimi mwenyewe nilishawai kuwa na mpenzi loh namshukuru mungu kunitoa huko.yaani very iresponsible lakini mimi nilikuwa naona sawa tu as long tunapendana.kumbe nilikuwa najidanganya.usikae na mtu kwa kujidanganya
take this example unavaa kiatu no 9 ukaenda shop ukakuta kiatu no 7 kizuuuri sio saizi yako kinakubana ukakichukua.nini kitatokea?
dunia ni kubwa hii wanaume wapo kibao tulia muombe mungu.
always mungu anajibu nothing bad comes from heaven
have a nice wkend
bye
 
Haha, kwa kifupi watu wa kaskazini wanajishughulisha eh?! Saaafi..

By the way, mkuki kwa nguruwe. Sitaki kusema ni mara ngapi lakini jinsia KE ndio inaongoza kwa kuwatumia ME ili kutimiza matakwa yao. Iwe chuoni, makazini au mtaani! Wote tuna matatizo (ME + KE)
 
Watu wengine wake kwa waume wanapenda kulea au kutumiwa kwahiyo acha tu waendelee maana hapo ndipo furaha yao ilipo.
 
Mkuu Smile tapeli kazi yake ni kukuteka akili, so wewe umeleta tahadhari hii lakini watch out kama watakuja kwako watakuja kwa style nyingine, na possibly wa kukutapeli hawatakua wanachuo kwa sababu hao tayari ushawa earmark ikifika zamu yako kutapeliwa wala hutajua, kiulaini tu utaingia mtegoni, si ndio maana ikaitwa utapeli. Wakati huo wewe wadhani uko katika deep love naye kwamba huyu ndio nlikua natamtafuta kwa muda mrefu yeye atakuwa anasema kimoyomoyo kudadadadeki mida ikifika tu nasepa
 
Yakinikuta ujue nimependa kufanya hivyo. . . hamna nnachofanya kwa lazima linapokuja swala la mahusiano.
mungu akusaidie iwe hvo lizzy yaani wadada wanateseka jamani namshukuru mungu kwa kunitoa huko
 
viwango vinatofautiana hii yenu ni too much mkuu

Ah wapi! Ni case ya mtu kuumwa na mbwa it is not news ila mtu akimuuma mbwa ....

Thread yako yenyewe inaashiria kuwa wewe ni subscriber wa falsafa ya ME kugharamia kila kitu. Alijiimbia wa jina langu "ni lini kina dada nao watatoboka" (kama wimbo huo huufahamu m-PM Preta).
 
sio lazima kuwa na mwanaume maishani mkuu thats my principle

Unamaanisha nini? Kwamba sio lazima kuolewa/kuoa ama kuwa na mpenzi tu? Naona hayo ni mawili tofauti! Na la pili hapo ndio utapoingizwa mkenge coz la pili ni ngumu kuliepuka
 
kweli binadamu tunatofautiana, yaani hivi hivi namuhanga mwanaume gari?
nampa pesa ya matumizi?
uwiiiiiiiiiiii labda nampangia nyuma? ahahahahahahahahah

mambo ya kujifanya nimependa sana sitaki mie........ na nilivyo mbahili hao vijana hawatonipata ng'oooo loh.......
 
Ah wapi! Ni case ya mtu kuumwa na mbwa it is not news ila mtu akimuuma mbwa ....

Thread yako yenyewe inaashiria kuwa wewe ni subscriber wa falsafa ya ME kugharamia kila kitu. Alijiimbia wa jina langu "ni lini kina dada nao watatoboka" (kama wimbo huo huufahamu m-PM Preta).
sipo unavodhani mkuu na ningekuwa hvo nisingekuwa hapa nilipo nisingekuwa naamka saa kumi usiku.am living my life on my own
 
Haha, kwa kifupi watu wa kaskazini wanajishughulisha eh?! Saaafi..

By the way, mkuki kwa nguruwe. Sitaki kusema ni mara ngapi lakini jinsia KE ndio inaongoza kwa kuwatumia ME ili kutimiza matakwa yao. Iwe chuoni, makazini au mtaani! Wote tuna matatizo (ME + KE)
fafanua mkuu
 
kweli binadamu tunatofautiana, yaani hivi hivi namuhanga mwanaume gari?
nampa pesa ya matumizi?
uwiiiiiiiiiiii labda nampangia nyuma? ahahahahahahahahah

mambo ya kujifanya nimependa sana sitaki mie........ na nilivyo mbahili hao vijana hawatonipata ng'oooo loh.......
just imagine shosti
 
Back
Top Bottom