Matapeli wa mapenzi humu JF

Andrew123

JF-Expert Member
Jun 2, 2012
7,030
8,581
Wandugu!
Tafadhali Chukueni tahadhari na watu (wanawake kwa Wanaume) wanaotangaza kuwa eti wanataka wake au waume huku jamiiforums kumbe wana agenda ya siri nasema haya kwa sababu yamenikuta jana nilimpata mdada humu humu Jamiiforums tukawa tunawasiliana na jana mwanzoni tulikubaliana tukutane MLIMANI CITY baadae akabadilisha akasema tukutane pale MWENGE (Maryland Bar) mi nikakubali akaja kweli muda tuliokubaliana saa 10:30 jioni (Maryland Bar Mwenge ghafla nikavamiwa na group la vijana wapatao wa 4 wanadai ati kwa nini namsumbua kwa kumtongoza kila siku mke wake duuh! kilichonisaidia ni mbio zangu maana jamaa walishuhudia vumbi tu! labda walichofaidi ni bia niliyokuwa nimebakisha hapo mezani lakini kama ndo mpango wao wanipore wamenoa!! KWA HIYO TAFADHALINI kuweni makini,vinginevyo MTALIA SIKU MOJA
 
ahsante kwa tahadhari.mara kwa mara watu wanaonywa humu.ila mara nyingi malalamiko ni kwa wanawake wanatendwa na wanaume wa jf.sikutegemea kama kuna mwanamke angemtenda mwanamme jf.kisukari nitaishia kwenye screen tu,mengine akuu siyawezi.tena sitaki pm.wacha nikachungulie kulee
 
abdreaakalima ana hoja. Nitonye umemdandia bila kutaka hata kuhoji kama kuna upungufu kwenye madai yake. Kama alivamiwa anasingizia ili iweje wakati hakuna anayeshindana naye? Utapeli ni jambo la kawaida katika kila kitu. Uzuri ni kwamba hapa jamvini hatuonani kwa sura wala kujuana kwa majina ya kweli. Hivyo huyo unayeoona kama mke wa mtu au tapeli anaweza kutumia jamvi kufanya biashara yake. Huwa tuna tabia ya kuhofia wakenya na wanigeria kuhusiana na utapeli wakati mchezo huu mchafu umekua na uko kila mahali. Pole sana andreakalima mwanangu. Hata hivyo siamini kama unaweza kupata akufaaye kwa njia ya hatari na wasi wasi kama mtandao.
 
Hakuna vya bure ndugu...yaani a bunch of.PM's ndio zikupe mzigo...hiyo ni rahisi sana atiii
 
Father of All,

Upande wa Nitonye swala sio kudandia... Swala ni kwamba kitu gani ambacho mtoa mada kinamfanya afikirie kuwa watu wa JF wapo so special? Mkuu kupata mwanamke kwa njia ya kutangaza uchumba na sio kwamba mlizoeana mkajenga mazoea na kutaka kufahamiana inabidi lazima kama mwanaume uwe makini sana.

For tuwe wazi kuwa ni rahisi na salama zaidi kwa mwanaume kukutana na mwanamke ambaye hamfahamu na kukawa na usalama kuliko kwa mwanamke. Hivo mie kwa mtazamo wangu ukipata mwanamke ambaye umeahidiana bada ya makubaliano ya ndani ya siku moja inabidi ukimbie sana... na kama utataka kuonana nae na kuendeleza mahusiano mara nyingi mwanaume wa hivi ndio yule ambae kwa njia ya kama za fb kisha lala na wanawake kibao, na kwamba hata huyo hana niya nae zaidi tu ya kulalana na kusonga mbele. Kwa muktadha huo inakuwa kama 'he had it coming'..
 
Last edited by a moderator:
ina maana wengine humu mnataka kuonja?lakini ni tabia mbaya na ni utoto fulani,ujifanye single,halafu upange mpango wa kumuangamiza mwenzako.huwa unafikiria nini kabla ya kufanya yote hayo?na lengo lake ni nini?
 
acha uongo, pale maryland hamna wahuni wala wa kukufanyia fujo labda kama uliiba spanner za wale mafundi magari pale nje. Istoshe pale kuna ulinzi wa kutosha hata ukisahau simu kesho yake unaikuta. Ungesema Yenu bar ningekubali. Hata hivyo jf hamna mtu wa kukufanyia hivyo labda useme hii ni stori umetunga. Mia
 
Hahahahahahahahahahahahaha
mbio zako zime kuponya!
Hongera sanaaaaa!
 
Hahahahahahahahaha
kwa hiyo atakuwa aliiba spaner?
acha uongo, pale maryland hamna wahuni wala wa kukufanyia fujo labda kama uliiba spanner za wale mafundi magari pale nje. Istoshe pale kuna ulinzi wa kutosha hata ukisahau simu kesho yake unaikuta. Ungesema Yenu bar ningekubali. Hata hivyo jf hamna mtu wa kukufanyia hivyo labda useme hii ni stori umetunga. Mia
 
Wadau mimi nimetoa tu tahdhari na wala silazimishi mtu akubali au kukataa kilichonikuta mimi,kwa namana nilikimbia moaka neighbours walishtuka wakifikiri mi mwizi
 
chukua tahdhari unakwenda kukutana kwa mara ya kwanza na mtu usiemjua
 
ahsante kwa tahadhari.mara kwa mara watu wanaonywa humu.ila mara nyingi malalamiko ni kwa wanawake wanatendwa na wanaume wa jf.sikutegemea kama kuna mwanamke angemtenda mwanamme jf.kisukari nitaishia kwenye screen tu,mengine akuu siyawezi.tena sitaki pm.wacha nikachungulie kulee

hahahahahahah kwenye jukwaa lako pendwa!
 
Mods wakiiweka hii topic kama sticky inaweza saidia pia.. kama vile nakuona ulivochomoka na Rav2 yako! :lol:
 
hahahahaaa, unajua nilipokuwa nasoma huu uzi,nlikuwa namhurumia kweli ila hapo mwisho pakanivunja mbavu....
hilo ni fundisho bwana ukitaka kudate humu hakikisha una mbio za kutosha.....

chezeya JF alaaaa...............
Nambe, usikute ni wewe ume m-trap huyu jamaa yetu afu saivi unamchungulia kwa mbaaali, kama ivi: :behindsofa:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom