Wandugu!
Tafadhali Chukueni tahadhari na watu (wanawake kwa Wanaume) wanaotangaza kuwa eti wanataka wake au waume huku jamiiforums kumbe wana agenda ya siri nasema haya kwa sababu yamenikuta jana nilimpata mdada humu humu Jamiiforums tukawa tunawasiliana na jana mwanzoni tulikubaliana tukutane MLIMANI CITY baadae akabadilisha akasema tukutane pale MWENGE (Maryland Bar) mi nikakubali akaja kweli muda tuliokubaliana saa 10:30 jioni (Maryland Bar Mwenge ghafla nikavamiwa na group la vijana wapatao wa 4 wanadai ati kwa nini namsumbua kwa kumtongoza kila siku mke wake duuh! kilichonisaidia ni mbio zangu maana jamaa walishuhudia vumbi tu! labda walichofaidi ni bia niliyokuwa nimebakisha hapo mezani lakini kama ndo mpango wao wanipore wamenoa!! KWA HIYO TAFADHALINI kuweni makini,vinginevyo MTALIA SIKU MOJA
Na je hii umepata kuisikia?
Kuna kijana mpevu wa Kitanzania kaenda New York. Yupo katika kijiziara cha muda mfupi watu wanamplia gharama zake full board. Hivyo anakaa katika Hoteli moja bomba.
Huyu kijana kazoea moja moto moja Baridi maeneo ya Getaways. Sijui kama msomaji ulikuwapo wakati Getaways inawika pale makutano ya Mtaa wa Uhuru na Bibi Titi Mohamed. Huyu kijana mpevu hajui afanyeje jioni hii pale New York na yeye ana kiu aina mbili. Ana kiu ya Bia na kiu ya ile sehemu. Kiingereza anajua, kwa hiyo hakuna tatizo la mawasiliano. Kuuliza uliza kaelekezwa sehemu panauzwa bia, na wale binadamu wenye ile sehemu wapo.
Mtoto wa kitanzania katoka taratibu hadi kwenye ile jointi. Pale kakutana na wanywaji wenzake, akiwapo mdada mmoya wa kinyu yok. Katia leather shoes zake safi, rangi ya ngozi ni mweusi yeye utazani wa Zinza Mori. Kijana toka Bongo hakupoteza muda. Kamuongelesha binti yule kwa kiingereza wakaelewana wataondoka wote--lakini kwanza wanywe.
Usiku ukiwa unakaribia kuwa mkuu, kijana wa kitanzania akamwomba sasa huyu mtoto wa kinegro watoke kuelekea kwenye ile hoteli ya kifahari alikofikia. Mtoto kakataa: "No I don't sleep in hotels." (Tafsiri? Mi silali mahotelini, akasema). Kijana akaanza kujisikia hovyo. Nadhani unajua inakuwaje unapokuwa umejiandaa kumpa mtu kitu kisawasawa halafu picha inakuwa kama inaharibika.
Ila pakawa na bahati kidogo kumbe. Yule binti akamwambiaje? We kama una hiyo kiu? Twende kwangu. Eti huyu kiijana wa Kitanzania kakubali baada ya kuambiwa si mbali sana kutoka bale baa. Yule binti kaanza kuongoza njia kuelekea kwene uchochoro fulani una kijigiza hivi. Mara zikatokea njemba. Mijibaba minne. Kijana kakwidwa.
"Search him fast," njemba mmoja anaamuru apekuliwe mifukoni haraka. Kwa bahati mbaya fedha zote alizotembea nazo zikawa zimeishia baa. akawa kabakisha dola moja tu. Yule alokuwa anampekua akahamaki: Unataka binti wa New York kwa dola moja? Una akili wewe? Katika majibizano lafudhi ikaonesha huyu kijana si Mwamerika.
"Where you from?" Njemba moja likauliza.
"Tanzania," kijana akajibu.
"Where is that?" Njemba jingine likauliza kwa kutokujua Tanzania ndo wapi.
Maelezo yakaonesha huyu kijana katoka Afrika.
Wakamzaba kofi na kuamuru, "get lost...." Nasikia na ile dola moja haikurudishwa.