Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 50,462
- 21,334
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi amepiga marufuku kuweka barabarani matangazo ya biashara ya dawa za kuongeza nguvu za kiume.
Lukuvi amesema kufanya hivyo ni fedheha na kuwataka wanaotangaza biashara hizo, walipie katika mamlaka zinazohusika kama wana uhakika na dawa zao.
Marufuku yangu itafanikiwa endapo viongozi wa Manispaa watalisimamia hili kwa umakini kwa kuzingatia sheria za mazingira zilizowekwa maana wao ndio wachangiaji wakubwa wa hili kutokana na kutoshiriki kwa umakini katika kuusimamia usafi wa mazingira, alisema Lukuvi juzi katika kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa.
Aidha, uongozi wake umepiga marufuku matangazo yote ambayo huchafua mazingira yakiwemo ya vitambaa yanayodaiwa ni ya waganga wa jadi wanaotangaza kazi zao, ambayo hutundikwa pembeni mwa barabara badala yake imewataka wanaotaka kujitangaza kutumia vyombo vya habari.
Lukuvi alisema kitendo cha kutundika matangazo au kubandika mabango yenye kutangaza shughuli au bidhaa ni kukosa ustaarabu na ni uchafuzi wa mazingira.
Katika hatua nyingine, Lukuvi ambaye alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho, aliwataka Wakala wa Barabara (Tanroads) kuhakikisha wanafanya ukarabati na matengenezo katika barabara zilizoharibika kwa wakati badala ya kusubiri ziharibike sehemu kubwa ili kupunguza gharama na hasara kwa serikali.
Pia aliitaka Tanroads kuhakikisha inasimamia alama za barabarani na kupaka rangi katika michoro iliyofutika sanjari na kuweka matuta kila sehemu yanapohitajika ili kupunguza ajali zisizo za lazima.
Kwa upande mwingine, wajumbe wa kikao hicho walikubaliana kusimamia upandaji wa miti kando ya barabara inayoendana na hadhi ya barabara husika badala ya kupanda miti ya miarobaini ambayo haivutii katika barabara.