Mataifa ya Kiarabu yaombwa kuiwekea vikwazo Marekani

ze kokuyo

JF-Expert Member
Jan 24, 2014
7,418
9,599
Waziri wa mambo ya nje wa Lebanon ameyaomba mataifa ya Kiarabu kuiwekea vikwazo vya kiuchumi Marekani kama njia ya kulipiza kisasi kwa kitendo cha Rais wa nchi hiyo Donald Trump kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel,huku akiahidi kuuhamisha ubalozi wa nchi yake kwenye mji huo (Jerusalem).

Waziri wa mambo ya nje wa Lebanon Gebran Bassil,ameyasema hayo katika kikao cha dharula huko Cairo nchini Misri.
Bwana Bassil ameyataka mataifa ya mashariki ya Kati kuiwekea vikwazo vya kisiasa,kiuchumi na kifedha Marekani.

RT

Huku hayo yakiendelea kuna taarifa zinaeleza kwamba jeshi la Malaysia limesema kwamba lipo tayari kuiingilia kijeshi na kuikomboa Jerusalem.

YAhoo Singapore News
 
Duh! Ha ha ha! Naona kundi la mapaka-shume 20 wakiungana kupambana na simba. May be this time watafanikiwa ukizingatia Kiduku naye kishatoa neno kulaani; Iran naye na sera yake ya kuifuta Israel katika uso wa dunia. Sie akina panya tukae tu mkao wa "kuliwa" tuangalie upepo unavyovuma; whether is in our favor or against.
 
Tatizo mataifa hayo manafiki sana kwani hayana hata kiwanda cha risasi yanapewa na Marekani huku yakiwa yamekabizi kila kitu kwq USA!!

Mataifa haya yamechonganishwa na Mmarekani kwa kigezo cha suni na Shia na wao kuonana maadui kuwa kila kiongozi yuko hatarini kupinduliwa na USA ndio mshirika wao anaewaunga mkono.

Rejea mgogoro wa hivi karibuni wa Qatar na waarabu wenzie ambapo Marekani alijifanya ahusiki wakati yeye ndio aliwachochea wengine kuwa Qatar anaunga mkono magaidi huku waarabu wakiitwanga vikwazo hadi vya ndege za Qatar kutua ila USA akasaini deal la kuwauzia ndege za abiria!!!
 
Ili wale mafuta yao au wajikaangie
Sio ndio hapo kiongozi. Kwanini kwa mfano, kuonesha mshikamano mashirika yote ya ndege ya kiarabu - Emirates, Etihad, Qatar, Oman Air, Egypt Air, Saud Air, etc. etc. wasisitishe safari zao zote kuingia US? Hawawezi; kwanini? Ndio route yenye faida nono zaidi na mhimili wa hayo mashirika. Wamebaki kupiga makelele yasizo na kichwa wala miguu.
 
Wanaitegemea kiuchumi na kiulinzi pia Waarabu ni mbwa koko bora Waajemi kule Irani wanakoroma
 
Wanaitegemea kiuchumi na kiulinzi pia Waarabu ni mbwa koko bora Waajemi kule Irani wanakoroma
Angalau kwa mujibu wa hiyo habari naona jeshi la Malaysia kidogo limetamka kitu chenye mashiko; liko tayari kuingilia kijeshi kuukomboa Jerusalem. Hawa angalau nimewaelwa sio hao wengine debe tupu.
 
Wanaitegemea kiuchumi na kiulinzi pia Waarabu ni mbwa koko bora Waajemi kule Irani wanakoroma
Hata wao ni muda tuu. Obama aliwabeba hao na nyuklia deal ila trump ni kivuruge atawachachafya mpka wakome. Na urafiki was trump na Israel umeipa jeuri Israel hapo tegemea ubabe kama huwezi pigana au huna silaha za kisasa unapigwa tuu
 
Ahahha!!! Dah.... hapo ni sawa na kusema watanzania waishio viijijini wagomea kununua bidhaa za Azam,

Ni vigumu sana kumwekea Marekani vikwazo vya kiuchumi, sababu mataifa mengi sana wanaitengemea Marekani, labla mataifa yote tuungane tuwawekee vikwazo

Bei ya mafuta ikishuka dhamani kutakuwa na mtafutano
 
Ni sawa na Zanzibar kuiwekea Vikwazo Tanzania!

Au Msondo ngoma kuiwekea Vikwazo Basata
Wewe ni kichaa, kwani Zanzibar siyo Tanzania?

Hapa duniani ni Watanganyika peke yao wasiojuwa Tanzania ni nchi gani na Tanganyika ni ipi, Wazanzibar wanajitambuwa vyema.

Ukienda United Kungdom, England wanajitambuwa, Ireland wanajitambuwa, Wiles wanajitambuwa na Scotland wanajitambuwa.

Ccm ni laana kwa Watanzania.
 
Nchi zenyew za kiarab zenye nguv zmebak ngap jamen?maana zote ziliharibiwa kwa vita,.nadhan itakua imebak 1.maana usitegeme saudia au UAE wamgomee US hata sku1,labda kina iraq na afghanistan,hahaha
 
Ahahha!!! Dah.... hapo ni sawa na kusema watanzania waishio viijijini wagomea kununua bidhaa za Azam,

Ni vigumu sana kumwekea Marekani vikwazo vya kiuchumi, sababu mataifa mengi sana wanaitengemea Marekani, labla mataifa yote tuungane tuwawekee vikwazo

Bei ya mafuta ikishuka dhamani kutakuwa na mtafutano
Vijijini hawamuhitaji Azam hata kidogo na wanaeza ishii toa mifano ya maana
 
Back
Top Bottom