Habari za uhakika zilizopatikana kutoka Wizara ya Nishati na Madini ni kwamba Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakim Maswi, amechukua likizo ya kustaafu na kuna kila dalili kwamba huenda akastaafu rasmi utumishi wa umma kabla uchunguzi dhidi yake haujahitimika na kabla Profesa JK hajamchukulia hatua za kisheria na kinidhamu kwa kulipotezea taifa mabilioni ya shilingi ambazo zingetumika kuboresha huduma za jamii.
Naiona sinema ileile kutoka kwa Jairo, Werema na sasa Maswi. Ifike wakati itungwe sheria ya kumzuia mtumishi wa umma kustaafu pindi anapokuwa anachunguzwa kwa matumizi mabaya ya ofisi. Sote tunafahamu kwamba Jairo na Werema hawajachukuliwa hatua za kisheria kwa kisingizio cha kustaafu utumishi wa umma. Sasa imekuwa kama fasheni--kila fisadi akianza kuchunguzwa hukimbilia kuchukua likizo ya kustaafu ili kujinusuru na kibano kinachomkabili. Kwa staili hii, hakika hawa wezi wataifilisi nchi kwa kukwapua rasimali za nchi na ufisadi hautakoma kamwe! Tukubali kuliwa tu mpaka kiyama kitukute.
:israel: