Maswi kachukua likizo ya kustaafu

Maswi kachukua likizo ya kustaafu

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
27,664
Reaction score
29,054
Habari za uhakika zilizopatikana kutoka Wizara ya Nishati na Madini ni kwamba Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakim Maswi, amechukua likizo ya kustaafu na kuna kila dalili kwamba huenda akastaafu rasmi utumishi wa umma kabla uchunguzi dhidi yake haujahitimika na kabla Profesa JK hajamchukulia hatua za kisheria na kinidhamu kwa kulipotezea taifa mabilioni ya shilingi ambazo zingetumika kuboresha huduma za jamii.

Naiona sinema ileile kutoka kwa Jairo, Werema na sasa Maswi. Ifike wakati itungwe sheria ya kumzuia mtumishi wa umma kustaafu pindi anapokuwa anachunguzwa kwa matumizi mabaya ya ofisi. Sote tunafahamu kwamba Jairo na Werema hawajachukuliwa hatua za kisheria kwa kisingizio cha kustaafu utumishi wa umma. Sasa imekuwa kama fasheni--kila fisadi akianza kuchunguzwa hukimbilia kuchukua likizo ya kustaafu ili kujinusuru na kibano kinachomkabili. Kwa staili hii, hakika hawa wezi wataifilisi nchi kwa kukwapua rasimali za nchi na ufisadi hautakoma kamwe! Tukubali kuliwa tu mpaka kiyama kitukute.

:israel:
 
''kama kafulila ni mwananume kweli ajitokeza uraiani aseme mimi ni mwizi aone kama sijamshughulikia, kwann wanakimbilia bungeni? Wao si wanaume waseme hadharani wanione'' Eliakim Maswi
 
Tuone kama ana huo ubavu wa kuyasema hayo baada kustaafu!!
 
Sasa anastaafu kwa nini wakati JK alisema ni pesa ya IPTL sio ya umma!!!
 
''kama kafulila ni mwananume kweli ajitokeza uraiani aseme mimi ni mwizi aone kama sijamshughulikia, kwann wanakimbilia bungeni? Wao si wanaume waseme hadharani wanione'' Eliakim Maswi

Karatasi za kufungia vitumbua.. Zimeanzia kumhengesha
 
Habari za uhakika zilizopatikana kutoka Wizara ya Nishati na Madini ni kwamba Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakim Maswi, amechukua likizo ya kustaafu na kuna kila dalili kwamba huenda akastaafu rasmi utumishi wa umma kabla uchunguzi dhidi yake haujahitimika na kabla Profesa JK hajamchukulia hatua za kisheria na kinidhamu kwa kulipotezea taifa mabilioni ya shilingi ambazo zingetumika kuboresha huduma za jamii.

Naiona sinema ileile kutoka kwa Jairo, Werema na sasa Maswi. Ifike wakati itungwe sheria ya kumzuia mtumishi wa umma kustaafu pindi anapokuwa anachunguzwa kwa matumizi mabaya ya ofisi. Sote tunafahamu kwamba Jairo na Werema hawajachukuliwa hatua za kisheria kwa kisingizio cha kustaafu utumishi wa umma. Sasa imekuwa kama fasheni--kila fisadi akianza kuchunguzwa hukimbilia kuchukua likizo ya kustaafu ili kujinusuru na kibano kinachomkabili. Kwa staili hii, hakika hawa wezi wataifilisi nchi kwa kukwapua rasimali za nchi na ufisadi hautakoma kamwe! Tukubali kuliwa tu mpaka kiyama kitukute.

:israel:

Hivi siku hizi umri wa kustaafu umeshushwa hadi miaka 45?
 
Alizaliwa lini?
 
Acheni uongo; kijana Kama Yule anastaafu vipi?

Tunajenga taifa la wambea, wazandiki ...why?
 
sidhani kama amefikisha umli wa kustaafu! hata hajakaribia!!
 
Hii nchi ccm imeharibu.....mbinu zote wizi na wezi wako ccm. Leo nimepita gate moja lina bendera ya ccm juu...kumbe umo ndani garage babu kubwa....si dhani kama TRA hutembelea maeneo kama hayo. Kweli ccm ukoo wa wezi.
 
Ukweli ni upi? Unasema si kweli wakati huna ukweli mbadala. Endelea kubisha huku wenzako wanakwapua rasilimali za nchi na kulala mbele. Mbona huulizi Jairo alikuwa na umri gani? Na mbona hujauliza Werema ana umri gani?
 
Sasa anastaafu kwa nini wakati JK alisema ni pesa ya IPTL sio ya umma!!!

Kama ni ya IPTL kwanini JK amemsimamisha kazi na kumchunguza? Anamchunguza ili iweje na kwanini mtuhumiwa amechukua uamuzi wa kuchukua likizo ya kustaafu kama kweli zile pesa walizokula sio za UMMA? Akili za kuambiwa, changanaya na za kwako....zile pesa ni za UMMA kwa 101% ila CCM wanafunika kombe mwanaharamu apite. Bado hujagundua hilo? Kalaghabhahho!
 
Back
Top Bottom