Maswali ya wanawake..

Maswali ya wanawake..

Asiipoongea na wewe utalalamika anakisirani, akiongea na wewe unaona kero... ndiyo maana wengine wanaamua kuwa busy na smartphones zao na kuchat na watu wanaowasikiliza...
 
Mwenyewe napendaga kweli maswali huwa natamani niulize tu nijibiwe huwa nafurahia kwa kweli.
Eti bae leo umerudi nyumbani saa ngapi
 
Hahaha mmetisha sana kwenye hiyo ndoa. Inaonyesha jamaa unakausha sana mpaka missus anatafuta convo kwenye matangazo ya biashara. Natamani kusikia majibu yako kwa maswali kama hayo.
 
Subiri hivyo hivyo siku akutane na wapiga debe na wazee wa swaga waanze kupiga mashine kisha uje hapa kulalamika unapigiwa ...[emoji224][emoji224][emoji224]
 
Habari wanaMMU

Bila kupoteza muda naomba kufahamu hasa kutoka kwa wanaume waliooa kama hii hali inatokea na kwako.

Hivi na ninyi huwa mnaulizwa maswali mfulululizo kama mimi kutoka kwa wake zenu?

Vipi na nyie wake za wanaume wwnzangu huwa mnawauliza maswali mengi muwapo na waume zenu kama mimi navoulizwa?

Ninaposema maswali sijalenga upande mmoja ila namaanisha ile hulka ya kuulizauliza hata kitu kidogo.

Mfano anaona tangazo kwenye tv tumepunguza bei ya bidhaa zetu kwa 50% bado atakuuliza eti wamepunguza kwa 50%? wakati anaona na anasikia

Anaelimu ya kutosha kuelewa na kumudu lugha ya kimombo lakini bado anataka umfanyie ukalimani kwenye series za kichina na kikorea kupitia Eng Subtitle?

Si kwamba nachoshwa na maswali ya mke wangu ila ningependa kujua hata nyie ni hivo
Ndio hivyo mkuu, tuwazoee. Na ukiwa unamjibu wanafarijika sana anajua unamsikiliza.
 
Back
Top Bottom