Maswali ya Sensa 8 tu? why | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maswali ya Sensa 8 tu? why

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Duduwasha, Aug 27, 2012.

 1. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #1
  Aug 27, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,177
  Trophy Points: 280
  Mbona Watu wa Mjini Tuliambiwa tutaulizwa maswali mengi zaidi ya 63 lakini mimi nimeulizwa maswali Nane tu oi au Wamechukua vilaza kuwahesabu watu so wameshindwa kusoma vipengele vingi...

  1. Jina lako? Duduwasha

  2.Umri wako?Old Enough

  3.Una Mke? Sijaoa Kwa nini Bahati bado haiafika akacheka! Mdada huyo...

  4.Mpo wangapi kwenye kaya yako? Mmoja

  5.Una Ulemavu wowote? Sina

  6.Unasoma Elimu yako? Chuo nimemaliza! - Nakumbuka Kikwete amesema akimaliza uraisi ataanza kusoma tena? Sijui atasomea wapi au Nje! USA kama sumaye! Tutakimbiwa

  7.Upo kwenye mfuko wowote wa Jamii? Ndiyo NSSF Ila wafikishie ujumbe nataka niache kazi niendeleze biashara mafao yangu nayataka yote

  8.Una mtu yeyeto aliyesafiri nje ya Nchi? Mdogo wangu amesharejea na ataondoka tena karibuni

  Nikawauliza una Yameisha? Wakasema Ndiyo? Nikashangaa! Manake walisema kutakuwa na maswali zaidi ya 60
   
 2. C

  CDK Member

  #2
  Aug 27, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 45
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 15
  Mi yaliongezeka mawili
  Unajishushugulisha na kilimo au ufugaji
  Upo kwenye bima ya afya
  BAADA YA HAPO WAKATOKA MBIO
   
 3. n

  ngonani JF-Expert Member

  #3
  Aug 27, 2012
  Joined: Aug 27, 2012
  Messages: 1,371
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Sensa na maajabu yake:mimi niliulizwa maswali mengi mfano:una pasi ya mkaa,una pasi ya umeme,friji je,simu ya mkononi,kompyuta?kuna mlemavu?etc kwa ujumla nilishangaa kidogo na nilipommuliza alinieleza kuwa kuna dodoso fupi na refu na kwamba mimi ameniuliza kwa dodoso refu,then nikamuuliza mnatumia vigezo gani kuhoji wengine kwa dodoso fupi na wengine kwa dodoso refu akasema makarani wamegawanywa kundi la dodoso fupi na kundi la dodoso refu,hivyo inategemea ni karani yupi amewahi kufika kwako.Mimi sielewi ni kwanini maswali yawe tofauti katika sensa ile ile,wnegine waulizwe dodso fupi ya maswali tisa na wengine dodoso refu la maswali 54,tafadhali mwenye ufahamu wa mambo haya ya sensa anieleweshe logic ya hii kitu maana niko gizani.
   
 4. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #4
  Aug 27, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Hii sensa moja ya nchi moja? Mbona maswali tofauti?

  Au mzaha huu?
   
 5. Observer2010

  Observer2010 Senior Member

  #5
  Aug 27, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 198
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Maswali mengine yaliyopo kwenye dodoso yanahitaji just observartion ya karani na si lazima akuulize vitu vyote. Kwa mfano, kujua nyumba imeezekwa bati au nyasi or kujua kama nyumba yako ina umeme au haina, kujua unapata huduma ya maji safi au la si lazima akuulize, akifika tu nyumbani kwako anaona. So ukiona umeulizwa maswali machache ujue the rest ameyaobserve mwenyewe na kuyajaza.
   
 6. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #6
  Aug 27, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  questionnaire and observation sheet ni vitu viwili tofauti. Hapa mtoa mada anauliza kuhusu questionnaire!
   
 7. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #7
  Aug 27, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Hata wanaotoa majibu kama wewe hamsikilizi maswali vizuri; hivi jibu la 'una mke?' ni 'sijaoa?'. Mfuko wa jamii au mfuko wa hifadhi ya jamii?
   
 8. Observer2010

  Observer2010 Senior Member

  #8
  Aug 27, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 198
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Vyovyote utakavyoweza kuiita ila wao wameita dodoso, sasa sijui kiingereza chake km ni questionnaire au ni observation sheet, ila fahamu kuwa hilo dodoso anakuwa nalo yeye na anapokuuliza anajaza yeye, not like common questionnaires ambazo unapewa, unasoma maswali then unajibu na kujaza accordingly. Muulize mtoa mada kama alikabidhiwa hilo dodoso halafu akasoma na kuona kama lina maswali hayo machache. Nadhani umenielewa. I hope bado haujahesabiwa mkuu.
   
 9. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #9
  Aug 27, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,077
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  sasa hapo kwenye red alikuwa anatania au alikuwa anamaanisha?
   
 10. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #10
  Aug 27, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  MKUU NA MIMI NIMEULIZWA HILI REFU AAAH MPAKA KERO DAAh!
   
 11. K

  Kelvin Mndeme New Member

  #11
  Aug 27, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanza naomba nikusahihishe, dodoso fupi lina maswali 37 na refu lina maswali 62, na pia Wamefanya hivyo sababu ya maeneo ya kuhesabia watu yaani EA(Enumeration Area) kuna zingine ni kubwa na zingine ni ndogo,kwa hiyo wale wa dodoso fupi wamepewa EA ndogo compared na wa dodoso refu,pia makarani wa dodoso refu huwa wawili ktk EA moja!!
   
 12. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #12
  Aug 27, 2012
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Yeah, kuna dodoso fupi (maswali 37) na dodoso refu (maswali 62). Kuna maswali mengine anatumia tu uzoefu na common sense. Kwa mfano, akiuliza elimu yako na ukamjibu first degree, haoni sababu ya kukuuliza "unajua kusoma na kuandika?". Lakini kwenye dodoso, elimu yako niswali moja na kujua kusoma & kuandika ni swali jingine.
   
 13. Gedeli

  Gedeli JF Gold Member

  #13
  Aug 27, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 452
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  hapo nikuniwekea maneno mdomoni Je kama nina bomba lakini kutokana na ukata wa maisha walishakata umeme na maji si atanijibia ndio
   
 14. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #14
  Aug 27, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Sensa wakifanya kawaida inagawika sehemu mbili

  Moja inakuwa ya kujua idadi ya watu na nyengine wanaita Household Budget Survey

  Hii ya HBS inakuwa na masuala mengi yanayohusiana na income, matumizi na ownership of appliances kwenye kaya.

  Sio watu wote wanaoulizwa hii ya HBS maana masuala ni mengi mno

  Mfano wa masuala hayo ni pamoja na
  1. Unatumia kiasi gani cha mapato yako kwa nishati?
  2. Unatumia kiasi gani cha mapato yako kwa chakula?
  3. Unatumia kiasi gani cha mapato kwa usafiri?
   
 15. Gedeli

  Gedeli JF Gold Member

  #15
  Aug 27, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 452
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45

  ninawasubili kwa hamu lakini sitakuwa na mda wa kuwapa waniulze maswali 62 nitawaomba waondoke hii itakuwa kero tena
   
 16. RGforever

  RGforever JF-Expert Member

  #16
  Aug 27, 2012
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 6,187
  Likes Received: 1,908
  Trophy Points: 280
  ULIMUULIZA KWANINI?

  1. Hawezi kukuuliza kama wewe ni albino wakati anakuona siyo

  2. Kama ni Mwanafunzi wa chuo huwezi kuulizwa unamifugo mingapi


  Maswali Mengine hawezi kukuuliza kutokana na mazingira yako. Na uwe unamuuliza ili akufafanulie siyo kuja Kulalamika JF
   
 17. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #17
  Aug 27, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  KUna mtu kaulizwa jinsi yake!
   
 18. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #18
  Aug 27, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,177
  Trophy Points: 280
  Sasa wenyewe wapo Busy unataka niwaulize eeh! na mimi pia nilikuwa mbio mbio... Nilimuuliza Hapo ndio mwisho wa maswali akasema Ndio... Wewe ulitaka niendelee au nimbishie?? wewe RGforever hujaacha kunywa Wanzuki! tu

  Jinsi unavyoonekana Mlevi Unasema Mwanafunzi huwezi kumuuliza ana mifugo Mingapi? unadhania kuitwa mwanafunzi ni ulofa? watu wanarithi mali Jirani yangu kuna Mwanafunzi anamiliki Nyumba na mali kadhaa alizoachiwa na Wazazi wake Marehemu, kama karani mjinga kama wewe hatauliza ni kosa kubwa kwa kazi aliyopewa.

  naona Hangover za Jumapili hazijakuisha! kuna kitu unakitafuta!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #19
  Aug 27, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,177
  Trophy Points: 280
  oi Nadhani alisuuzika tu
   
 20. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #20
  Aug 27, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,177
  Trophy Points: 280
  Kwahiyo ningesikiliza Vizuri ningepata nini? na hapo sikuweka tu sahihi alisoma kwenye karatasi zake una mke? kisha akasema uomeoa? nikajibu Sijaoa.
  na kuhusu huo Mfuko ndivo alivyotamka tena akatoa hadi mfano kabisa NSSF? Ndio Nikajibu wewe lipi Utakalo.. Watu Wengine Hupenda Ligi za Kijinga!
   
Loading...