Maswali ya alichokisema Roma! Inaonyesha hii ni movie ya kinajeria haina uhalisia

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Hii ni observation yangu baada ya kuangalia kile kilichoitwa press ya Roma leo. Nitamuongelea Roma tu na kujadili content ya yale aliyoongea. Sitagusa lolote kuhusu Mwakyembe kwa leo maana hakuwa mmoja wa waliotekwa. Japo uwepo wake, na jinsi alivyoshiriki kujibu maswali kumeibua mjadala mkubwa ambao sitaki tuujadili leo. Kwa Leo tumalizane na Roma kwanza;

1. Roma ameulizwa tukio hilo limetokana na muziki au mambo mengine? Anasema hajui na hawezi kubashiri. Lakini wakati huohuo anasema watekaji walikua wanawahoji huku wakiwapiga. Sasa walikua wakiwahoji nini? Hicho walichokua wakihojiwa na watekaji ndo kilichowafanya watekwe. Simple logic. Kama ni kuhusu mziki basi mziki ndo uliwafanya watekwe. Kama ni kuhusu siasa basi siasa ndo imewafanya watekwe. Sasa anasemaje hajui? Liars must have a good memory. Roma asituchezee akili.!!

2. Anasema walitupwa wakiwa wamefungwa mikono na miguu. Lakini aliweza kujifungua yeye then akawafungua na wenzie wakaanza kutembea. Huu ni uongo mtupu. Hili jambo linawezekana kwenye movie za Kinigeria tu. Tena zile za uchawi-uchawi. Yani mpigwe karibia kufa halafu mfungwe kamba mtupwe na muweze kujifungua? Walifungwa kamba au nyuzi za kushonea mawigi? Roma asituchezee akili.!!

3. Kwanini watupwe Ununio halafu akaripoti Oysterbay? Kuna vituo vingapgi vya polisi kutoka Ununio kabla ya Oysterbay? Kwanini hakuripoti kituo chochote cha polisi cha jirani usiku huohuo badala ya kwenda nyumbani kujiandaa na baadae kwenda Oysterbay? Roma asituchezee akili.!!

4. Anasema walitupwa Ununio lakini alitembea hadi nyumbani Mbezi Beach. Kwanini atembee kwenda nyumbani usiku wote huo? Katikati ya Ununio na Mbezi kuna chuo cha usalama na kuna kambi ya jeshi, kwanini hakujisalimisha huko? Kama haamini kambi ya jeshi, wala chuo cha usalama, kwanini hakwenda nyumba nyingine yoyote kuomba msaada badala ya kuamua kutembea kwa mguu hadi nyumbani? Hakua na hofu kwamba watekaji wanaweza kumfuata tena nyumbani? Roma asituchezee akili.!!

5. Anasema anaamini vyombo vya usalama vitachunguza kuwajua watekaji, lakini wakati huohuo anasema kwamba watekaji hao walikua na pingu. Kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, pingu haziwezi kumilikiwa na mtu asiye askari. Sasa Roma anatuambiaje anaviamini vyombo vya usalama wakati ameshasema watekaji walikua na pingu? Au siku hizi maproducer wa bongoflava nao wameanza kumiliki pingu? Roma asituchezee akili.!!

6. Roma anasema alipofika nyumbani aligonga hakufunguliwa so akavunja mlango. Je mkewe alikua wapi? Kwanini hakuwaamsha majirani badala ya kuvunja mlango? Hivi kuwaamsha majirani na kuvunja mlango kipi rahisi? Je hakuona kama kuvunja mlango usiku huo wa manane ni kujiweka kwenye risk zaidi? Maana majirani zake wanajua amepotea, so wapo kwenye taharuki. Ghafla wanasikia mlango unavunjwa usiku wa manane. Hakuona kwamba majirani wangeweza kureact na ikamgharimu? Halafu mtu aliyetekwa na kupigwa vibaya anapata wapi nguvu za kwenda nyumbani na kuvunja mlango? Roma asituchezee akili.!!

7. Roma anasema hawezi kusema yote kwa sababu ya usalama wake. Mbona Ruge alisema yote? Mbona Nape alisema yote? Ina maana wao hawapendi usalama wao? Roma asituchezee akili.!!

8. Anasema wamepigwa sana halafu anaonesha jeraha kwenye lips ambalo halizidi sentimita mbili. Kajeraha kanakolingana kabisa na mtu aliyejing'ata akitafuna bazoka. Roma anatuaminisha eti hilo ndo jeraha lililosababishwa na watekaji. Yani watekaji siku hizi hawang'oi meno wala kucha tena, bali wanakuchanja tu na wembe kwenye lips kajeraha kadogo ili ukila chakula cha moto uungue. Hiyo ni style mpya ya watekaji wa siku hizi. Roma asituchezee akili.!!

9. Anasema aliyofanyiwa anaweza kufanyiwa mtu mwingine yeyote, lakini hajasema amefanyiwa nini. Kama kweli ana nia ya kuwaepusha wengine na yaliyomkuta kwanini asiseme ukweli? Roma asituchezee akili.!!

10. Anasema suala liko polisi so hawezi kuongea sana ataharibu upelelezi. Hii inaonesha kuwa alikimbilia polisi kama defensive merchanism ili aje kujitetea kuwa hawezi kuongea coz suala lipo polisi. Roma asituchezee akili.!!

#NB:
Kwa ujmla Roma amejiharibia sana baada ya press ya leo. Ni bora angeamua kukaa kimya tu kama Dr.Ulimboka. Kukaa kimya ni jibu zuri kuliko kuongea utumbo kama wa Roma.

Kuna watu wanamtetea Roma kuwa eti amefanya vizuri kutokueleza yote maana ana familia na watoto hajui hatma yake. Mimi nasema huo ni UBINAFSI wa ajabu mno. Akina Nyerere wakati wanatafuta uhuru wa nchi hii wangekuwa wanawaza hatma ya familia zao tungekua bado tupo kwenye ukoloni.

Sisemi familia sio muhimu, ila nasema kuwa taifa ni muhimu zaidi. Kitendo cha Roma kuficha ukweli kinaweza kuisaidia familia yake kwa muda tu, lakini kitawaweka watanzania wengi kitanzini (ikiwemo familia yake) hapo baadae. Wapo watanzania ambao watatekwa, watajeruhiwa, na wengine watauawa kwa sababu tu Roma amekataa kusema ukweli leo. Lakini angesema ukweli angeokoa watanzania wengi sana ambao wametekwa au wako kwenye mpango wa kutekwa.

Kuficha ukweli wa yaliyomkuta hakumfanyi awe salama hata kidogo. Ila kunamfanya awe kwenye hatari zaidi. Hii ni kwa sababu siri inabaki kuwa kati yake yeye na watekaji. So watekaji wanaweza kutumia mwanya huo kummalizia kabisa ili kupoteza ushahidi. Lakini angekua mkweli akawataja hadharani angewapunguza nguvu watekaji hao, so angekuwa salama zaidi.

Faida ya kumtaja adui yako hadharani ni kwamba unammaliza nguvu. Moja ya principle za espionage ni kwamba ukimtaja adui yako hadharani anageuka kuwa mlinzi wako namba moja. Maana yake ni kwamba atahakikisha baya lolote halikupati, maana ukipatwa na baya (hata kupitia kwa watu wengine) atahusishwa yeye. Waswahili husema mchawi mpe mwanao akulelee.

Lakini ukimtunzia siri adui yako, atatumia nafasi hiyo kukumaliza kirahisi kwa sababu ana uhakika siri ni yenu wawili tu. So Roma asijione yuko salama kwa kuficha ukweli, ila ajione kuwa kajiweka kwenye hatari zaidi. Kuficha ukweli ni kuamua kukaa upande wa adui.

Askofu Desmond Tutu aliwahi kusema "If you are silent in situations of injustice, you have chosen the side of oppressor." Maana yake ni kwamba ukiamua kukaa kimya (kuficha taarifa) mahali penye uonevu, umechagua kuwa upande wa yule anayeonea wengine (oppressor). Bahati mbaya Roma kachagua kuwa upande wa oppressor kwa kuwafichia taarifa.!

Malisa GJ
 
Kama Roma ana zaidi ya ukweli kuliko uongo huu labda tutajua baadaye. Labda kama alitakiwa aeleze hivyo lakini akaharibu, hawakumfundisha ipasavyo. Utumbo mtupu!!!
 
Ukweli upi nyie nyumbu?

Furaha yenu ilikua kutajwa Makonda sio.
Acheni upuuzi, kaeleza ya moyoni.
Tengenezeni picha nyingine.

Malisa wakala wa mafisadi acha kujifanya unajua kila kitu
Hivi mmetumia muda japo kidogo kusoma hayo maswali na kutafakari japo kwa sekunde chache ?

Hivi Lumumba ni hizo buku saba tu mnapewa au kuna kitu mnasokomezewa pia ?
 
Malisa asiwe na wasiwasi na yeye siku yake ya kutekwa inakuja, atakuwa ana muda mzuri wa kufanya Press yake na kutoa maelezo yake.
... lazima asindikizwe na mtu mzito ili asipotoshe maelekezo ya maelezo!!!

Ndio maana Roma akijitahidi kuchanganya maelekezo na maelezo yake!! Hapo kwenye "pingu" nilienda mpaka "nyumbani" kuvipita vituo vya usalama! kujifungua kamba nk! kuna dots zaidi ya hizo ndio maana mkewe Roma alimtazama jicho la kukata akimaanisha Roma hajasema uhalisia!
Iko siku ukweli utajulikana
 
Umewahi kupita toka mahaba beach hadi kambi ya jeshi?uliona vituo vingapi Vya police? Kilichopo hapo karibu na TAYOWA kina kufulu mlangoni ni mwaka sasa .Pili hebu tuombe Mungu na wewe utekwe japo kwa siku moja tuone utakavyotoka ukiwataja watekaji wako haswa unapokuwa umejua ni system sio majambazi tu wakawaida .Acheni kabisa kufanya mambo magumu marahisi Mimi hadi sasa namsupport Roma maana amejitahidi kutuambia ukweli bila kuhatarisha maisha take mwenye akili ameshajua who is behind this give the guy time to heal and gain is confidence instead ya kulaumu mgeenda kwenye Vyombo Vya haki za binadamu huko international level mfungue madai sijui kesi ili wajue kuna kitu si chakawaida Tz Mpoki kumsakama Roma ambae kiukweli ametekwa hadi sasa tena ni Mbaya zaidi maana yuko kwenye utumwa mkali wa kuzuiwa kusema ukweli
 
Back
Top Bottom