Maswali na majibu kuhusu nyoka

Maswali na majibu kuhusu nyoka

jsenyinah

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Posts
249
Reaction score
339
Kweli Mungu alimlaani nyoka na anaaniwe tu mpaka mwisho. Atembelee tumbo arambe vumbi na mikwaruzo yote hapa duniani.

1. Kwann nyoka humgonga mtu na kumsababishia maumivu na hatimae kifo? Kama angekuwa mla nyama sawa,anaonaje raha kuzamisha meno yake 4 na ambayo humletea uchungu yeye?

2. Kwann asitumie akili ya kumkimbia tu binadu badala ya kujiumiza?

3. Nyoka hula nn, kunywa nini?

4. Nyoka huishi miaka mingapi hadi kufa?

5. Nyoka ana masikio?

6. Nyoka ana faida gani hapa duniani?

7. Nini dawa ya nyoka?
 
Mi nawaza hapa, kwa nini iwe BIKOBA!?
 
Kwanza kabisa mkuu nyoka ana meno mawili makubwa yanayotoa sumu(fangs) na pia si nyoka wote wanaomtafuta binadamu wamdhuru bali ikitokea wamekutana na nyoka mwenyewe akajihisi yupo hatarini hapo anaweza kumgonga binadamu.. Lakini mara nyingi nyoka hukimbia bila hata kuonekana anapohisi au kukutana na binadamu... Kinachoweza kusababisha nyoka amgonge binadamu aidha ukimpiga, kumtishia, kumkanyaga, au kusogea kwenye mayai yake... Japo wapo baadhi ya nyoka wanaosemekana ni wakorofi sana hivyo hao ni hatari zaidi. Nilikuwa nakurekebisha kidogo tu mkuu waweza endelea
 
Namba 6.
Nyoka ni chakula km chakula kingine. Kuna siku niliangalia youtube jinsi watu wanavyoandaa supu ya nyoka. Duh nilishangaa sana
Watu wanashangilia kitoweo cha nyoka.
Usichokula ww, wengine wala.
 
Kwa nini nyoka huanzia kumeza mnyama kichwani na si miguuni/mkiani
 
Kwann ww ukimwona nyoka nyumbani kwako au hata mtaani lzm umpige magongo afe ..kumbe samaki akimla mtu inakuwa stori lkn kila siku samaki huliwa na wal a cyo story ..kwann mtu anampiga nyoka hata kama katulia zake ..defending Kama vile ww unavyojihami

Kila kitu duniani kina faida ,dunia hujaumbiwa ww tu ,

Nyoka hulisha wadudu mbali mbali ,kuna baadhi ya wadudu hupata mlo wao kupitia nyoka

Pia nyoka ni chakula kwa baadhi ya viumbe kama eagle,nyegere nk

Nyoka hula panya na wadudu wengine ambao huharibu mazao ,hvy husaidia kuepusha uharibifu wa mazao

Nyoka husaidia kupunguza idadi ya wanyama waharibifu kama panya nk
 
3.Hula chips kavu na hunywa mafuta ya transformer.

Mengine sijibu yamekaa kichochezzy.
 
Swali juu ya swali.

Eti nyoka akikugonga kuna kidubwasha kipo kama zile wanazosema dawa za mende, au sijui niseme za kufanya Chooni kunukie, unaweka pale ulipogongwa inaondoa sumu.

Mimi sifahamu chochote kuhusu hii.

Je kuna Mdau/Wadau watakaoweza kunisaidia kunipa majibu ili nipate kujifunza.

Kwa kweli nimesikia mara nyingi kutoka kwa Watu wakiwa wanaongelea hiyo kitu.

Msaada wenu, tafadhali
 
Kweli Mungu alimlaani nyoka na anaaniwe tu mpaka mwisho. Atembelee tumbo arambe vumbi na mikwaruzo yote hapa duniani.

1. Kwann nyoka humgonga mtu na kumsababishia maumivu na hatimae kifo? Kama angekuwa mla nyama sawa,anaonaje raha kuzamisha meno yake 4 na ambayo humletea uchungu yeye?

2. Kwann asitumie akili ya kumkimbia tu binadu badala ya kujiumiza?

3. Nyoka hula nn, kunywa nini?

4. Nyoka huishi miaka mingapi hadi kufa?

5. Nyoka ana masikio?

6. Nyoka ana faida gani hapa duniani?

7. Nini dawa ya nyoka?

Naomba nijibu swali namba 6. Tufanye (let's imagine) tuwatokomeze nyoka wote. Kitakachotokea (tuna-predict) panya (rodents), ambao ni chakula kikubwa cha nyoka, wataongezeka sana. Na hata wale wenzetu (watu fulani) wala panya hawataweza kuwamaliza. Matokeo yake panya hao, ili waweze kuishi na kuzaliana zaidi, watatafuta chakula, ambacho kwa kiasi kikubwa ni nafaka e.g., mtama, mahindi etc. wakishambulia hayo mazao watasababisha njaa sehemu husika. Hiyo inaweza pelekea watu wengi kufa kwa njaa. Vifo vya njaa vinaweza kuwa vingi kuliko kesi za watu wanaoweza kuuawa na nyoka kwa mwaka. Kwa hiyo uwepo wa nyoka kunasaidia kitu kinaitwa "ecological balance". Mtu wa mwanzo kuelezea hii filosofia ni bwana mmoja aliyeitwa Charles Darwin - refer biology F2
 
Chatu hana meno! Labda chatu wa mizimu ya kwenu!, pili, nyoka haoni anahisi, hili nimeshali practice sana patamela forest national reserve. Ukikutana na nyoka simama! Immediately!. Then anaondoka mwenyewe [HASHTAG]#elimukwenuwajingawajingakamawewe[/HASHTAG]!
 
Nyoka anaona! Ila haoni rangi (can not discriminate btn different colors). Kwamba ukisimama hafanyi kitu huenda ikawa sahihi kwa sababu nyoka wengi huwa wanakuwa stimulated/irritated na "moving object". Ila ndugu hii ni nadharia tu! Ukikutana na koboko (black mamba) au swira (e.g., spitting cobra), hiyo inaweza kuwa habari nyingine.
 
Nyoka kumgonga mtu kama njia ya self defence na kujikinga na athari atazoweza kupata na hatari ya huwepo wako eneo husika , mara nyingi usipo mwona yeye hana hata habari na wew husepa kimya kimya. Unapishana na nyoka sana maporin bila wew kujua, ingawa kuna nyoka wengine wao ni wakorofi wakikuona wanatana kukudhuru tu, mfano koboko.

( nyoka anagonga hata wanyam wengine sio binadamu likija suala la hatari)

Kujiumiza sio kupenda, ni sawa na binadamu anampiga mtu ngumi , japo na yeye anaumia lakini anaondoa tatzio na kulinda uhai ambalo ni thamani kuliko maumivu ya muda mfupi.

Uhai na maisha ya nyoka inategemea na mazingira anayoishia (kama ni hatar sana kwake) pia na specie ya nyoka huyo


Nyoka hana masikio, ila taarifa zote kuhusu mabidiliko ya nje anapata kupitia ulimi wake anaotoa toa nje kila mara

Nyoka, anafaida nyingi, kiuchumi huingiza kipato, hutengenezewa bidhaaaa nyingi, sumu yake hutumika kwa kazi nyingi, watfiti huwa tumia, wana sayansi,

Kijamii, ni kiburudsh watu hulipa hela kwenda kuwaona hawa nyoka, kuna watu wanaabudu ambazo ibada zao hukamilika akiwepo nyoka.
Kwenye ECO SYSTEM nyoka hubalance nature kwa kupungiza viumbe wengine, n kutoa chakula kwa wengine pia faida zipo nyingi


Dawa nyoka ukimaanisha kama tiba ya alie umwa na nyoka, zipo za hospital na jadi ila inategemea aina ya nyoka na ukali wa sumu na uharaka wa kupata tiba hiyo.

Ila ukimwaga mafuta nyoka hakai eneo hilo.
 
Chatu hana meno! Labda chatu wa mizimu ya kwenu!, pili, nyoka haoni anahisi, hili nimeshali practice sana patamela forest national reserve. Ukikutana na nyoka simama! Immediately!. Then anaondoka mwenyewe [HASHTAG]#elimukwenuwajingawajingakamawewe[/HASHTAG]!
Chatu meno anayo pemben kwa chini fulani , yanayo muwezesha kuvuta mzoga wake, stage kwa stage katika kumeza
 
Kweli Mungu alimlaani nyoka na anaaniwe tu mpaka mwisho. Atembelee tumbo arambe vumbi na mikwaruzo yote hapa duniani.

1. Kwann nyoka humgonga mtu na kumsababishia maumivu na hatimae kifo? Kama angekuwa mla nyama sawa,anaonaje raha kuzamisha meno yake 4 na ambayo humletea uchungu yeye?

2. Kwann asitumie akili ya kumkimbia tu binadu badala ya kujiumiza?

3. Nyoka hula nn, kunywa nini?

4. Nyoka huishi miaka mingapi hadi kufa?

5. Nyoka ana masikio?

6. Nyoka ana faida gani hapa duniani?

7. Nini dawa ya nyoka?

Naomba niongezee kujibu swali namba 7: nini dawa ya nyoka?
Nitaeleza mara mbili, 1) matibabu ya nyoka baada ya kuumwa 2) jinsi gani ya kujikinga kupunguza uwezekano wa kugongwa na nyoka.

DAWA
Hapa nitatoa maelezo ya dawa rasmi za nyoka zinazotumika hospitali. Dawa ya nyoka huitwa antivenon (=antivenin). Dawa hii hutengenezwa kutokana na sumu ya nyoka mwenyewe. Kwa mfano jamiii ya nyoka ya cobras na mamba (koboko) hutoa sumu iitwayo neurotoxin ambayo huathiri mfumo wa fahamu (nervous system). Sumu ya neurotoxin hukamuliwa toka kwa nyoka hao kutengeneza antivenin ya sumu ya cobras. Hali kadhalika sumu ya nyoka vifutu (puff adders au gaboon viper) wana sumu tofauti (cytotoxin) inayoathiri mfumo wa damu na pia cardiotoxin inayoathiri moyo. Antivenin ya vifutu hutengenezwa kutokana na sumu yao hiyo hiyo. Kwa hiyo unapoumwa na nyoka ni vema utambue ni nyoka gani huyo na ana sumu ipo. Good thing ndugu zangu ni asilimia haizidi 20% ya nyoka wenye sumu, Wengine aidha hawana sumu kabisa e.g., chatu au sumu yao haidhuru mwanadamu mtui mzima. Vile vile kwa kuwa dhumuni la sumu ya nyoka ni kujipatia chakula chake, anapomgonga mnyama mkubwa kama binadamu dhumuni lake ni defense. Kwa sababu hiyo si ajabu nyoka Mwenye sumu anaweza kukugonga na asikuachie sumu - hii huitwa dry bite. Kwa hiyo ndugu zangu ukiiumwa na nyoka don't panic! Watu wengi wamemkufa kwa ajili ya effect ya hofu rather than sumu yenyewe.
 
Back
Top Bottom