Maswali na majibu kuhusu Biblia (bible): Tukutane hapa

Ukiangalia mstari wa 14 Unaweza pata mwanzo wa huu mtiririko,,ili upate kujua kwamba Suleiman ametumika kama kalamu tu kuwasilisha mambo yenye chanzo kilicho zaidi ya Suleiman.
 
Methali 8

1 Je! Hekima halii?Ufahamu hatoi sauti yake?

2 Juu ya mahali palipoinuka karibu na njia,Penye njia panda, ndipo asimamapo.

3 Karibu na malango, mahali pa kuingia mjini,Mahali pa kuyaingilia malango anapiga kelele.

4 Enyi watu, nawaita ninyi;Na sauti yangu ni kwa wanadamu.

5 Enyi wajinga, fahamuni werevu,Nanyi wapumbavu, mpate moyo wa kufahamu.

6 Sikieni, maana nitasema yaliyo mazuri,Na kufumbua midomo yangu kutakuwa maadili.

7 Maana kinywa changu kitasema kweli,Na uovu ni chukizo kwa midomo yangu.

8 Maneno yote ya kinywa changu yana haki;Hapana hata neno lililopotoka au la ukaidi.

9 Yote humwelea yule afahamuye,Yote huelekea mbele yao waliopata maarifa.

10 Pokea mafundisho yangu, wala si fedha,Na maarifa kuliko dhahabu safi.

11 Maana hekima ni bora kuliko marijani;Wala vyote vinavyotamanika havilingani nayo.

12 Mimi, hekima, nimefanya werevu kuwa kao langu;Natafuta maarifa na busara.

13 Kumcha BWANA ni kuchukia uovu;Kiburi na majivuno, na njia mbovu,Na kinywa cha ukaidi pia nakichukia.

14 Shauri ni langu, na maarifa yaliyo sahihi;Mimi ni ufahamu, mimi nina nguvu.

15 Kwa msaada wangu wafalme humiliki,Na wakuu wanahukumu haki.

16 Kwa msaada wangu wakuu hutawala,Na waungwana, naam, waamuzi wote wa dunia.

17 Nawapenda wale wanipendao,Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.

18 Utajiri na heshima ziko kwangu,Naam, utajiri udumuo, na haki pia.

19 Matunda yangu hupita dhahabu, naam, dhahabu safi,Na faida yangu hupita fedha iliyo teule.

20 Natembea katika njia ya haki,Katikati ya mapito ya hukumu.

21 Niwarithishe mali wale wanipendao,Tena nipate kuzijaza hazina zao.Sehemu ya Busara katika Uumbaji

22 BWANA alikuwa nami katika mwanzo wa njia yake,Kabla ya matendo yake ya kale.

23 Nalitukuka tokea milele, tangu awali,Kabla haijawako dunia.

24 Wakati visipokuwako vilindi nalizaliwa,Wakati zisipokuwako chemchemi zilizojaa maji.

25 Kabla milima haijawekwa imara,Kabla ya vilima nalizaliwa.

26 Alipokuwa hajaiumba dunia, wala makonde Wala chanzo cha mavumbi ya dunia;

27 Alipozithibitisha mbingu nalikuwako;Alipopiga duara katika uso wa bahari;

28 Alipofanya imara mawingu yaliyo juu;Chemchemi za bahari zilipopata nguvu;

29 Alipoipa bahari mpaka wake,Kwamba maji yake yasiasi amri yake;Alipoiagiza misingi ya nchi;

30 Ndipo nilipokuwa pamoja naye, kama stadi wa kazi;Nikawa furaha yake kila siku;Nikifurahi daima mbele zake;

31 Nikiifurahia dunia inayokaliwa na watu;Na furaha yangu ilikuwa pamoja na wanadamu.

32 Basi, wanangu, nisikilizeni sasa;Maana heri hao wazishikao amri zangu.

33 Sikieni mafundisho, mpate hekima,Wala msiikatae.

34 Ana heri mtu yule anisikilizaye,Akisubiri sikuzote malangoni pangu,Akingoja penye vizingiti vya milango yangu.

35 Maana yeye anionaye mimi aona uzima,Naye atapata kibali kwa BWANA.

36 Bali anikosaye hujidhuru nafsi yake mwenyewe,Na wao wanichukiao hupenda mauti.
Huu uzi hauhitaji kupingana kwa hasira, tunashirikishana uelewa. Kuhusu hayo, tumesema kwamba Sulemani mwana wa Daudi anaongozwa kunena kama kunukuu maneno ya mwingine aitwaye Hekima (aya ya 1 na ya 12. Labda swali liwe huyo Hekima ni nani!
 
Mm sipotoshi nime qout alchosema Sulemani ila ww ndo unataka kupotosha.
Hv kati ya ww na Sulemani nani anapaswa kuaminika?

Haya ww thibitisha kwamba Sulemani hakuandika kwa akili yake
Ndugu yangu nilipokusoma nimeona kuna namna unapotosha sababu una motive ilio ndani ya nafsi yako,,,ila kifupi Suleiman alikuwa akitekeleza majukumu yenye uhusiano mkubwa na MUNGU,,na asilani asingeweza kufanya yaliyo yake zaidi ya makusudi ya MUNGU.
 
Asante mkuu. Nilikuwa nasisitiza pia kwamba huyo Hekima anayenukuliwa na Sulemani ndiye yule aliyekuwa anajadiliana na Mungu Baba wakati wa uumbaji kwamba "Na tufanye mtu kwa mfano wetu".
 
Asante mkuu. Nilikuwa nasisitiza pia kwamba huyo Hekima anayenukuliwa na Sulemani ndiye yule aliyekuwa anajadiliana na Mungu Baba wakati wa uumbaji kwamba "Na tufanye mtu kwa mfano wetu".
Pitia mistari hii mkuu uisome kwa mda Wakolosai 1:15-19,,,Yohana 1:1-3 Na zaidi ni kiongozi wa wafalme wote wa dunia Mwanzo49:10 na Zaburi 2:7-8 linganisha na Mithali 8:15-16. Naamini hekima na ufahamu ni fumbo katika kuwakilisha nafsi kama ilivyo neno au kuhani mkuu Melkizedeck Mwanzo14:18-19,,Ebrania7:1-25..Ipitie taratibu Unaweza okota chochote.
 
Pitia mistari hii mkuu uisome kwa mda Wakolosai 1:15-19,,,Yohana 1:1-3 Na zaidi ni kiongozi wa wafalme wote wa dunia Mwanzo49:10 na Zaburi 2:7-8 linganisha na Mithali 8:15-16. Naamini hekima na ufahamu ni fumbo katika kuwakilisha nafsi kama ilivyo neno au kuhani mkuu Melkizedeck Mwanzo14:18-19,,Ebrania7:1-25..Ipitie taratibu Unaweza okota chochote.
Asante Mpalasinge. Nimeyasoma maaya yote hayo. Yanaongea kuhusu huyo Hekima aliyesemwa na Sulemani. Mtazamo wako ni sawa na wangu kuhusu hiyo mada. Angalia comment zangu hapo juu. Labda ulifikiri inamjibu mohamedy cadinaly, ndiye ana mtazamo tofauti.
 
Asante Mpalasinge. Nimeyasoma maaya yote hayo. Yanaongea kuhusu huyo Hekima aliyesemwa na Sulemani. Mtazamo wako ni sawa na wangu kuhusu hiyo mada. Angalia comment zangu hapo juu. Labda ulifikiri inamjibu mohamedy cadinaly, ndiye ana mtazamo tofauti.

Kama masema huyu siye sulemani. Thibitisheni basi sio Sulemani na mtuambie huyo hekima ni nan?
 
kwenye kanuni za kimungu sadaka ni muhimu ili jambo lifanyike na hata kwa shetani pia lazima utoe sadaka ili upate uchokitaka, ndio maana mungu aliamua kumtoa yesu kristo kwa ajili yetu kama ambavyo hata yeye anaagiza utoaji wa sadaka kwetu,lakini pia hapo ndipo imani ya kikiristo ilipojengwa kwenye kufa na kufufuka kwa yesu


Yesu Katika Injili


Agano Jipya, na hususan vitabu vitatu vya injili - lina nafasi maalumu kwa Wakristo. Wanavichukulia vitabu hivi vinne kama mwongozo, kwa sababu moja muhimu. Vitabu hivi vinne vya injili viliandikwa KWA AJILI YA Wakristo na viliandikwa NA Wakristo. Katika injili nne Yesu wa kihistoria amewekwa pembeni kwa manufaa ya Yesu aliyefanywa Mkristo (Paulo).


Waandishi wa injili wenyewe bado wana maswali mengi. Ingawa hakuna uhakika ni nani aliyeziandika injili hizi nne, wanazuoni wengi wa Biblia wamekubaliana kwamba Mathayo na Marko hawakuwa waandishi wa injili zinazobeba majina yao.

Injili ya Luka inadhaniwa kuandikwa na rafiki wa Paulo ambaye alikuwa mtu wa mataifa (Hakuwa myahudi) ambaye hakuwahi hata kumuona Yesu; ni sehemu ya kwanza ya maandiko yake juu Ukristo wa Mwanzo ambayo inajumuisha kitabu cha Matendo ya Mitume. Ingawa wakristo wengi wanasema kwamba injili ya Yohana iliandikwa na mwanafunzi wa Yesu aliyekuwa na jina kama hili (yaani Yohana).

Sasa hivi wanazuoni wa Biblia wanatia mashaka juu ya hili kutokana na ukweli kwamba kitabu hiki kiliandikwa mwaka 100 Baada ya kristo, na Yohana, mwanafunzi wa Yesu alikufa shahidi mwaka 70 Baada ya kristo, miaka 30 baada ya kifo chake.


Katika kuikubali nadharia kwamba watu wengine tofauti na wanafunzi wa Yesu waliandika vitabu vinne vya injili lazima pia ikubalike kwamba waandishi hawa inawezekana kwamba hawakuona kwa macho yao au kusikia kwa masikio yao mengi - kama si yote - ya matukio waliyoyaandika.

Hata tukiamua kusema kwamba wanafunzi wa Yesu waliziandika injili kwa mikono yao, tunaelewa kwamba hawakushuhudia matukio yaliyotokea pindi Yesu alipochukuliwa na maaskari kutoka katika Bustani ya Gethsemane kwa sababu imeandikwa: "- - kisha wanafunzi wote walimuacha wakakimbia --", katika injili zote mbili katika Mathayo 26:56 na katika Marko 14:50. Kwa kifupi, mengi tunayoyaona katika injili ni fununu na tetesi tu - si maandiko ya watu, walioshuhudia matukio yenyewe.


Nukta nyingine tunayoweza kuiangalia katika uchunguzi wetu juu ya injili ni kwamba katika injili zote nne hakuna hata moja iliyoandikwa wakati wa Yesu, ikizingatiwa kuwa hakuna taarifa iliyohifadhiwa juu ya kazi zake (Yesu) katika wakati wa uhai wake. Kwa kweli, karibu miaka arobaini ilipita kuanzia kipindi Yesu alipoondoka duniani mpaka kitabu cha kwanza cha injili kilipoandikwa.

Mwishoni wakati injili ya Marko inakuwa tayari, Paulo alikuwa ameshaanza kuhubiri kwa takriban miaka ishirini; na alikuwa tayari ameshaandika barua (waraka) yake kwa Warumi, ambapo alielezea imani na mafundisho yake yote aliyoyaandaa na kuyaingiza katika Ukristo. Kutokana na ukweli huu tunaweza kuona kwamba mafundisho ya Paulo, bila chembe yoyote ya shaka, yaliwaathiri na kuwavuta waandishi wa injili kwa kiasi kikubwa katika maandiko waliyoyaandika.


Vitabu vinne vya injili viliandikwa kati ya miaka 70 B.K. na 100 B.K. ya Marko ilikuwa ya kwanza, ikafuatiwa na ya Mathayo, kisha Luka na mwisho Yohana. Injili tatu za mwanzo zinafanana sana katika uandishi wake, uchunguzi wa haraka utaonyesha kwamba waandishi wa injili ya Mathayo na Luka walichukua (waliibia) habari nyingi sana kutoka kwa Marko walipokuwa wanaandika injili zao. Hii ndio sababu injili hizi tatu zinaonekana kuelezea kitu kimoja.


Injili ya Yohana inatofautiana sana na injili nyingine, hata hivyo hii ndio yenye mashaka zaidi juu ya ukweli na usahihi wake hasa kwa sababu mwandishi alijishughulisha zaidi na umuhimu wa Yesu katika imani ya ukristo kuliko yale yaliyosemwa na kufanywa naYesu.


Tunaweza kuhitimisha, kwa sababu ya uchache wa muda, kwamba kuandika kutokana na tetesi au fununu, na mvuto wa Paulo aliowaathiri waandishi, sura ya Yesu iliyoletwa kwetu katika injili si ya yule Yesu wa kihistoria (Yesu halisi).

Badala yake, waandishi hawa waliandika juu ya Yesu aliyetokana na masimulizi ya kale, kwa kutumia hoja ya kithiolojia kwamba waandishi hawa waliukristisha ukweli (yaani waliufanya ukweli uwe wa Kikristo). Waandishi walikuwa na imani kali za kikristo, na waliandika wakiwa na mtazamo huu akilini.


Matokeo yake ni kwamba injili hizi nne zina visa na masimulizi ya kale badala ya ukweli.

Ujumbe wa Yesu aliokuja nao kutoka kwa Mungu wote umepotea kwa sababu ya shinikizo la yale ambayo watu walitaraji na kutaka Yesu aseme na kufanya badala ya lile lililofanyika kiukweli.
 
Nimekuwa na maswali mengi kuhusu biblia pindi navyoisoma na kukosa majibu au mtu wa kumuuliza kwa wale ambao Mungu amewapa uwezo wa kutafsiri kitabu hiki kitakatifu ninaomba mtupe majibu yenu hapa.


Kwa kuanzia naomba niulize swali. Bible inasema Mungu alimuumba Adam na Hawa. Ila ukija kusoma katika bible unaona kama walikuwepo watu wengne duniani kwa mfano katika Mwanzo 4. Adamu na Hawa walikuwa na watoto wawili Kain na Habili baada ya Kain kumuua Habili mazungumzo kati ya Mungu ya Kaini yaliashilia kuna watu wengine zaidi ya Adam na Hawa.

Mwanzo 4: 1-15.

1 Adam akamjua Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, "nimepata mtoto mwanaume kwa bwana."
2 Akaongeza akamzaa ndugu yake, Habili. Habili alikuwa mchunga kondoo, na Kaini alikuwa mkulima ardhi.
3 Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana.
4 Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake;
5 bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana.
6 Bwana akamwambia Kaini, "Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana?
7 Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde."
8 Kaini akamwambia Habili nduguye, "Twende uwandani" Ikawa walipokuwapo uwandani, Kaini akamwinukia Habili nduguye, akamwua.
9 Bwana akamwambia Kaini, "Yuko wapi Habili ndugu yako?" Akasema, "Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?"
10 Akasema, "Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia katika ardhi!
11 Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako;
12 utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao dunian."
13 Kaini akamwambia Bwana, "Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki.
14 Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua."
15 Bwana akamwambia, "Kwa sababu hiyo yeyote atakayemwua Kaini atalipiziwa kisasi mara saba." Bwana akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga.


Swali langu ni hili, hao watu ambao wangemzulu Kaini ni watu gani ni wazazi wake Kaini ambao ni Adamu na Hawa au kulikuwa na watu wengine ambao Kaini alikuwa anawaofia? Na kama ni wazazi wake kwanini biblia haijaweka wazi kuwa walikuwa wanawazungumzia Adam na Hawa? Naombeni msaada kwa watu ambao mmeelewa icho kifungu mnisaidie. Natunguliza shukrani.
Nahisi hawa watu ni wale waliotokana na Seth pamoja na watoto wa kike wa Adamu
 
mungu,malaika ni mfumo wa kihoro...ambayo haifi anaposema tufanye mtu kwa mfano wetu anawambia malaika,huyo awe kwenye mfumo wa roho,sis binadamu tumegawanyika katika sehem mbili kuna mwili na roho,mwili ndio unaozikwa ila roho haifi ila mbuzi yeye ana mwili wa nyama akifa mbuzi ndio basi,binadamu tunaishi sehemu mbili kwa wakati mmoja tunaishi kwenye ulimwengu wa roho na ulimwengu huu wa dunia,naona naenda mbali ila cha msingi ni kwamba binadamu tumeumbwa kwenye mfumo ule wa malaika na mungu...wa roho isiyokufa.
Biblia inasema roho itendayo madhambi itakufa, wewe unasema roho haifi. Sikuelewi mkuu
 
Back
Top Bottom