Maswali na majibu kuhusu Biblia (bible): Tukutane hapa

Mwanzo4 inajieleza kabisa kwamba habil akakimbilia nchi nyingine na akaoa huko
Mimi naelewa kwamba alienda kuoa ndugu sake waliotawanyika huko na huko baada ya Adamu kuzaa wana wa kiume na wa kike! Au huenda mtazamo wangu si sahihi!
 
Hajaoa ndg zake isipokuwa kulikuwa na watu wengine ambao hawatajwi nimesema kuwa biblia inaanzia hapo kwa adamu na hawa kueleza habari za uumbaji,lakini kiimani adam na hawa ndo wa kwanza ki uchunguzi ni tofauti
 
Hao watu waliumbwa na nani?
 
Ukiingia kuchunguza maandiko utakuta mambo mengi hayako kihalis yanavyotajwa,ila kiimani tunasadiki ualivyo andikwa
 
Hebu tujuze zaidi. Umejuaje hilo!

Proverb 8 / methali 8:22-30

22 The Lord possessed me in the beginning of his ways, before he made anything, from the beginning.

23 I was ordained from eternity, and out of antiquity, before the earth was formed.

24 The abyss did not yet exist, and I was already conceived; neither had the fountains of waters yet erupted.

25 The mountains, with their great mass, had not yet been established. Before the hills, I was brought forth.

26 Still he had not made the earth, and the rivers, and the poles of the globe of the earth.

27 I was already present: when he prepared the heavens; when, with a certain law and a circuit, he fortified the abyss;

28 when he made firm the sky above, and set free the fountains of waters;

29 when he encompassed the sea within its limits, and laid down a law for the waters, lest they transgress their limits; when he weighed the foundations of the earth.

30 I was with him in composing all things. And I was delighted, throughout every day, by playing in his sight at all times,

Naomba kwa mwenye swahili vision na yeye a post hiki kifungu ili na wengine nao pia wapate ktk lugha ya kiswahili
 
OK. Tungemjua huyo ambaye prophecy hii inamwita "I" tusingepata shida kujua kwamba Yeye alikuwepo kabla ya dunia na wanadamu wote kuwepo.
 
Maneno ni ya Sulemani aliyezaliwa na mfalme Daudi miaka mingi baada ya uumbaji. Sulemani anatamka maneno ya mwingine aliyetajwa katika Mithali 8:1, 12; Huyo Ndiye
 
Proverb 8 / methali 8:22-30

22 The Lord possessed me in the beginning of his ways, before he made anything, from the beginning.

23 I was ordained from eternity, and out of antiquity, before the earth was formed.

24 The abyss did not yet exist, and I was already conceived; neither had the fountains of waters yet erupted.

25 The mountains, with their great mass, had not yet been established. Before the hills, I was brought forth.

26 Still he had not made the earth, and the rivers, and the poles of the globe of the earth.

27 I was already present: when he prepared the heavens; when, with a certain law and a circuit, he fortified the abyss;

28 when he made firm the sky above, and set free the fountains of waters;

29 when he encompassed the sea within its limits, and laid down a law for the waters, lest they transgress their limits; when he weighed the foundations of the earth.

30 I was with him in composing all things. And I was delighted, throughout every day, by playing in his sight at all times,

Naomba kwa mwenye swahili vision na yeye a post hiki kifungu ili na wengine nao pia wapate ktk lugha ya kiswahili
Soma taratibu uelewe,,pia soma version za kiswahili hasa King James na Union version.Lugha iliotumika ni mafumbo haiko straight,,Suleiman alikuwa na Roho tofauti ndani yake iliomwezesha kuwa na hekma,,maarifa na Uongozi the same to baba yake Daudi,,,hakuandika ya akili yake bali yale aliyofunuliwa.Usipotoshe haya maandiko ila yatumie kutengeneza mjadala,,usifikie hitimisho Mapema..Maneno ya biblia yana tofauti kubwa sana na innovation za physics na science kwa ujumla.
 
Mm sipotoshi nime qout alchosema Sulemani ila ww ndo unataka kupotosha.
Hv kati ya ww na Sulemani nani anapaswa kuaminika?

Haya ww thibitisha kwamba Sulemani hakuandika kwa akili yake
 
Methali 8

1 Je! Hekima halii?Ufahamu hatoi sauti yake?

2 Juu ya mahali palipoinuka karibu na njia,Penye njia panda, ndipo asimamapo.

3 Karibu na malango, mahali pa kuingia mjini,Mahali pa kuyaingilia malango anapiga kelele.

4 Enyi watu, nawaita ninyi;Na sauti yangu ni kwa wanadamu.

5 Enyi wajinga, fahamuni werevu,Nanyi wapumbavu, mpate moyo wa kufahamu.

6 Sikieni, maana nitasema yaliyo mazuri,Na kufumbua midomo yangu kutakuwa maadili.

7 Maana kinywa changu kitasema kweli,Na uovu ni chukizo kwa midomo yangu.

8 Maneno yote ya kinywa changu yana haki;Hapana hata neno lililopotoka au la ukaidi.

9 Yote humwelea yule afahamuye,Yote huelekea mbele yao waliopata maarifa.

10 Pokea mafundisho yangu, wala si fedha,Na maarifa kuliko dhahabu safi.

11 Maana hekima ni bora kuliko marijani;Wala vyote vinavyotamanika havilingani nayo.

12 Mimi, hekima, nimefanya werevu kuwa kao langu;Natafuta maarifa na busara.

13 Kumcha BWANA ni kuchukia uovu;Kiburi na majivuno, na njia mbovu,Na kinywa cha ukaidi pia nakichukia.

14 Shauri ni langu, na maarifa yaliyo sahihi;Mimi ni ufahamu, mimi nina nguvu.

15 Kwa msaada wangu wafalme humiliki,Na wakuu wanahukumu haki.

16 Kwa msaada wangu wakuu hutawala,Na waungwana, naam, waamuzi wote wa dunia.

17 Nawapenda wale wanipendao,Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.

18 Utajiri na heshima ziko kwangu,Naam, utajiri udumuo, na haki pia.

19 Matunda yangu hupita dhahabu, naam, dhahabu safi,Na faida yangu hupita fedha iliyo teule.

20 Natembea katika njia ya haki,Katikati ya mapito ya hukumu.

21 Niwarithishe mali wale wanipendao,Tena nipate kuzijaza hazina zao.Sehemu ya Busara katika Uumbaji

22 BWANA alikuwa nami katika mwanzo wa njia yake,Kabla ya matendo yake ya kale.

23 Nalitukuka tokea milele, tangu awali,Kabla haijawako dunia.

24 Wakati visipokuwako vilindi nalizaliwa,Wakati zisipokuwako chemchemi zilizojaa maji.

25 Kabla milima haijawekwa imara,Kabla ya vilima nalizaliwa.

26 Alipokuwa hajaiumba dunia, wala makonde Wala chanzo cha mavumbi ya dunia;

27 Alipozithibitisha mbingu nalikuwako;Alipopiga duara katika uso wa bahari;

28 Alipofanya imara mawingu yaliyo juu;Chemchemi za bahari zilipopata nguvu;

29 Alipoipa bahari mpaka wake,Kwamba maji yake yasiasi amri yake;Alipoiagiza misingi ya nchi;

30 Ndipo nilipokuwa pamoja naye, kama stadi wa kazi;Nikawa furaha yake kila siku;Nikifurahi daima mbele zake;

31 Nikiifurahia dunia inayokaliwa na watu;Na furaha yangu ilikuwa pamoja na wanadamu.

32 Basi, wanangu, nisikilizeni sasa;Maana heri hao wazishikao amri zangu.

33 Sikieni mafundisho, mpate hekima,Wala msiikatae.

34 Ana heri mtu yule anisikilizaye,Akisubiri sikuzote malangoni pangu,Akingoja penye vizingiti vya milango yangu.

35 Maana yeye anionaye mimi aona uzima,Naye atapata kibali kwa BWANA.

36 Bali anikosaye hujidhuru nafsi yake mwenyewe,Na wao wanichukiao hupenda mauti.
 
Back
Top Bottom