Maswali muhimu kwa JK baada ya kujivua gamba! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maswali muhimu kwa JK baada ya kujivua gamba!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Crucifix, Apr 12, 2011.

 1. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Familia ya kifalme hutawala kwa umoja, yaani baba, mama, watoto nk. Mfalme huwa ni mwakilishi tu wa mawazo ya familia katika jamii. Hivyo ndilivyo ilivyokuwa CCM kabla ya kujivua gamba (king yusufu) na ndivyo ilivyo baada ya kujivika gamba jipya (prince januari)
   
 2. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #2
  Apr 12, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Ndio raha ya kuzaliwa kwenye familia ya KIFALME!
   
 3. h

  hongoli Member

  #3
  Apr 12, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakati wa uchaguzi wa uenyekiti wa UVCCM, JK alimponda Nape kwa sababu kadhaa ikiwemo umri. Alimpeleka Masasi kabla ya kumuibua kwenye secretariat.

  Watu wanazungumzia kuhusu Lowassa aondolewe NEC, you never know atamuibulia wapi. Kwa nini walifanya kikao cha faragha. Je, anaweza kumtosa kimoja wakati hawajajuana barabarani?

  Kama akina Makamba ndio magamba, utashangaa kapewa nafasi nyingine nyeti.

  Bernard Membe kaondolewa kwenye secretariat, huwezi kufahamu kamuandalia "makao" gani. Kwa nini ukuu wa mkoa wa Dar-es-Salaam mpaka sasa bado unakaimiwa.

  Kuna watu walisema Jamhuri Makamba hawezi kupewa nafasi yoyote kwa sababu ya ishu ya Lisa Rockefeller. Nini kimetokea?

  Jaka Mwambi ni close friend wa JK kwa nini kampeleka Urusi?
   
 4. Hassani

  Hassani JF-Expert Member

  #4
  Apr 12, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Si kwamba hatabiriki,ila ni mtu ambaye maamuzi yake yanashinikizwa na external forces,angalia teuzi za watu kama Bilal,magufuli,Sitta..,ni dhahiri hawa watu hawakuwa chaguo lake ila aliwachagua ama kwa kuwapoza,wengine huwa analipa fadhila na wachache kwa matakwa yake,so usishangae hata yeye mwenyewe hajui nani ni chaguo lake,au hata kama ana chaguo anaweza kulazimika kumpigia chapuo mtu mwingine kwa sababu flaniflani.
   
 5. cogent boy

  cogent boy Member

  #5
  Apr 12, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM hilo gamba tu nyoka ni yuleyule na sumu yake......
  Mmeishiwa
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Apr 12, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Sera za CCM ndio zinazo'attract mafidadi...Walitakiwa waanze na kubadili sera!
   
 7. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #7
  Apr 12, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,870
  Likes Received: 6,609
  Trophy Points: 280
  ni kweli.wamefulia
   
 8. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #8
  Apr 12, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Hajui la kufanya wakuuu
   
 9. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #9
  Apr 12, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  JK alitokea Huko kusini kuja kukamata madaraka makubwa,
  NAPE ametokea kusini kuja kukamata madaraka.
  1+1=2, mambo yote hupangwa ila sisi huwa wanatuhadaa tu.
   
 10. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #10
  Apr 12, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  hafanyi maamuzi yoyote magumu, anasubiri dakika ya mwisho baada ya kuona upepo umeelemea wapi ndio anafanya hayo maamuzi! na sidhani kama hua ana mkakati wowote juu ya hayo maamuzi ya kukurupuka, angalia watu aliweka sehemu nyeti , weingi wao hawafanyi kazi yoyote ya maana na hajui nini cha kufanya eg Ngeleja na Masha, nadhani sasa hivi anashukuru Mungu Masha kukosa ubunge , maana na yale mauaji yanayofanyika na polisi dhidi ya wananchi na waandamani pamoja na vita vya wanakijiji na ma-baunsa Masha angemuweka JK kwenye hali ngumu sana
   
 11. malkiory

  malkiory JF-Expert Member

  #11
  Apr 12, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 272
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nepotism!
   
 12. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #12
  Apr 12, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tumesoma kwenye vyombo mbalimbali vya habari kuwa NEC ya CCM imewataka wanachama wake ambao wanahusishwa na ufisadi katika jamii kujiondoa wenyewe katika uongozi wa chama ndani ya siku 90 au kinyume na hapo wataonyeshwa mlango wa kutokea.

  Swali langu ni itakuwaje kama kweli hili tamko likitekelezwa sawa sawa?

  Swali hili linakuja kwa sababu hii. Ni muda mrefu sasa watanzania wengi wamekuwa wanasikia na kusoma katika vyombo vya habari kuhusu ufisadi mkubwa ulifanywa kwenye Benki Kuu ya Tanzania kupitia fedha za EPA. Miongoni mwa kampuni ambazo zinapigiwa kelele kila siku ni hii ya Kagoda ambao ndiyo ilichota kiasi kikubwa cha fedha hizo. Na kubwa zaidi habari hizi zimeeleza mara kwa mara kuwa fedha hizo zilitumiwa na CCM katika uchaguzi wa mwaka 2005. Sikumbuki kama CCM au rais mwenyewe alishapinga hili kwa ufasaha. Kwanza licha ya uchunguzi kufanyika suala la Kagoda limekuwa ni jambo la sitomfahamu mpaka sasa katika jamii ya Tanzania. Sasa tamko la NEC ya CCM linasema hakuna tena haja ya kudia ushahidi, shutuma tu ndani ya jamii zinatosha kumwadhibu mwanachama mwenye tuhuma.

  Fedha za EPA, Kagoda na matumizi ya fedha kwenye uchaguzi ni shutuma za ufisadi na tamko la NEC ya CCM linataka mwanachama wa CCM ambaye anashutumiwa kwa ufisadi kuondoka mwenyewe ndani ya siku 90 la sivyo ataonyeshwa mlango. Hili tamko linatia wasiwasi wa sitomfahamu hatma ya uongozi wa juu wa nchi hii. Hii ni kwa sababu kama kuna shutuma kuwa fedha za ufisadi wa EPA kupitia kampuni ya Kagoda zilitumika kwenye kampeni za CCM kuwa ajili ya kumpata rais mwaka 2005 ina maana kuwa rais aliyechaguliwa kwa kutumia hizo fedha za kifisadi basi naye ni fisadi ambaye anaipaka CCM matope mbele ya wananchi. Sasa Rais huyu ni mwanachama wa CCM, hivyo tamko la NEC linamhusu pia. Kama kweli NEC wako makini kwenye hili tamko basi tunategemea huyu rais ambaye anatuhumiwa kupatikana kwa fedha za ufisadi wa EPA kuondoka katika nafasi ya uongozi wa CCM kama tamko la NEC linavyoagiza. Kinyume na hapo watanzania wengi wataona hili tamko linakusudia kuwatoa baadhi ya mbuzi kafara tu. Hivyo ni kama kamchezo tu cha kuwapumbaza wananchi.

  Pia napenda kukosoa tamko la NEC ya CCM kwa kuwa halikwenda mbali kama wananchi wengi wanavyopenda kuona. Kama kweli CCM ina nia ya dhati ya kubadilika wanatakiwa sio tu kubadilisha baadhi ya viongozi katika nafasi zao bali kuiagiza serikali yake kuwachukulia hatua za kisheria wale wote wanaotuhumiwa kuwa ni mafisadi. Na mali zote walizopata kwa njia ya ufisadi zitaifishwe na kurudishwa serikalini kwa faida ya wananchi wote.

  Pia napenda kuipongeza NEC ya CCM kwa kutoa hilo tamko. Hii ni hatua nzuri. Naomba basi watanzania wenye nia ya dhati ya kuleta mabadiliko watoe msaada ili hili tamko litekelezwe vizuri. Msaada unaohitajika ni kutoa taarifa za ufisadi uliokwisha fanyika hapa Tanzania ili wahusika ambao wengi ni viongozi wa CCM wawajibike
   
 13. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #13
  Apr 12, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  hawa jamaa hawako serious kabisa na hii mada uliyoleta inaweza kuwafungua macho wale amabo hawajafumbuka. Mfano chukulia kumuondoa Mzee 6 kama 'gamba' na na kumuingiza Mama Meghji inaonyesha hilo tamko lina mzaha kiasi gani. Pia matamko kwa chama hiki sio kitu kinachoheshimiwa, mfano ni katibu mwenezi Chiligati alivyotoa tamko kuwa DOWANS walipwe na mwingine katoa lake pia na mengine yaliyofuatia.
  Lakini mwisho wa yote ni tamko la rais (ambaye kimsingi kama ulivyohainisha hapo juu) anapaswa naye kuachia ngazi kutokana na (tamko) hilo: alivyowapa (sikumbuki muda!!!) wauza madawa ya kulevya, wala rushwa nk.
  Mradi siku hazigandi, tusubiri na wote tutyaona.
   
 14. SOKON 1

  SOKON 1 JF-Expert Member

  #14
  Apr 12, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,115
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  HiĆ­ ni danganya toto kwani sintoona tofauti na kocha wa mpira anafungiwa mechi ila anashiriki mazoezi so wasijidanganye kwani wangeanza kuajibika toka kwa mwenyekiti wao.
   
 15. G

  GAMA LUGENDO Senior Member

  #15
  Apr 12, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 131
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  It is too early to make a conclusion.let us wait and see if the envisaged reforms will be really pragmatic or just empty political slogans which has always been politics of the day here in tanzania.
   
 16. Zed

  Zed JF-Expert Member

  #16
  Apr 12, 2011
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 359
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  The best way to evade Tanzanians' wrath on any hot issue is to postpone it for 90 days! Well believe me , experience tells me, we do have short memories. Actually, we tend to forget so quickly. After 90 days, I'm almost sure there would be very few of us, who would be remembering this issue! Just like EPA cases or Radar issue or Mbagala explosions. So, what is claimed to be a period of grace for mafisadi in CCM, in fact, is as good as a closed case or a new lease for more ufisadi! Once Nyerere, the founder of the very party said, Linalowezekana leo lisingoje kesho! If CCM are keen to clean-up their party, why would they hesitate to boot mafisadi out now? Do they expect them to repent? Certainly not! So, why? Why do they give them time? Why? Was CCM's own confession "mafisadi have bogged us down" a statement too quickly said than thought? May be... and that is typical JK. Remember once he said, he has no partnership in his regime? Well, that turned to be "too quickly said than thought". In fact he had RA as major shareholder! Don't expect much from CCM. CCM is as good as dead! With their own philosophy of peeling its skin, CCM is like an onion, once you start peeling it you remain with nothing!
   
 17. Joyum

  Joyum Senior Member

  #17
  Apr 12, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  What is needed here is wananchi to keep pushing a litle longer and sisiem will be history. People power must prevail to ensure this deadly party is forgetten for good.
   
 18. anti-fisadi

  anti-fisadi JF-Expert Member

  #18
  Apr 12, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  [QUOTE=Zed;1846782]The best way to evade Tanzanians' wrath on any hot issue is to postpone it for 90 days! Well believe me , experience tells me, we do have short memories. Actually, we tend to forget so quickly. After 90 days, I'm almost sure there would be very few of us, who would be remembering this issue! Just like EPA cases or Radar issue or Mbagala explosions. So, what is claimed to be a period of grace for mafisadi in CCM, in fact, is as good as a closed case or a new lease for more ufisadi! Once Nyerere, the founder of the very party said, Linalowezekana leo lisingoje kesho! If CCM are keen to clean-up their party, why would they hesitate to boot mafisadi out now? Do they expect them to repent? Certainly not! So, why? Why do they give them time? Why? Was CCM's own confession "mafisadi have bogged us down" a statement too quickly said than thought? May be... and that is typical JK. Remember once he said, he has no partnership in his regime? Well, that turned to be "too quickly said than thought". In fact he had RA as major shareholder! Don't expect much from CCM. CCM is as good as dead! With their own philosophy of peeling its skin, CCM is like an onion, once you start peeling it you remain with nothing![/QUOTE]

  kwa kiswahili sijui tuseme ni ubabaishaji, au changa la macho, hebu tuseme zengwe la kisiasa tuone

   
 19. KYALOSANGI

  KYALOSANGI JF-Expert Member

  #19
  Apr 12, 2011
  Joined: Jan 21, 2011
  Messages: 1,898
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  Tuliambiwa CCM itajivua gamba na jana ndio tumeambiwa wamejivua hilo gamba!
  Naomba niwaulize wataalamu wa sayansi za wanyama ,
  kama mfano huu ilivyo je CCMitakuwaje baada ya kujivua gamba ,
  Mfano wa kujivua gamba ni kama afanyavyo nyoka je akijivua gamba huwa nabadilikaje au anabakikuwanyoka tu
   
 20. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #20
  Apr 12, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  "Kujichubua", "kujipiga mkorogo" imekuwa kawaida sasa kwa baadhi ya kina mama na kina baba wanaotaka weupe wa bandia. Watu wanaojichubua hudhani kuwa watu weupe (wazungu, wahindi na waarabu) ni bora kuliko Waafrika, hivyo nao hufanya hivyo ili wapandishe hadhi yao. CCM nayo imefuata mkumbo wa kupaka mkorogo bila kujali madhara itakayo yapata.

  Rais Jakaya Kikwete tarehe 5 Februari 2011 aliwaambia wana CCM kuwa chama chao kilitakiwa kujivua gamba ili kiwe kipya. Hakika wazo hilo lilikuwa ni sahihi na kama lingefanyiwa kazi, chama kingerudisha hadhi yake. Hata hivyo, wana CCM walichokifanya jana si kujivua gamba, bali ni kujichubua kwa mkorogo. Kwa kufanya hivyo wapo katika hatari ya kupata kansa ya ngozi.

  Weupe waliojitengenezea CCM ni wa muda tu. Aidha ung'avu wa mkorogo hauwezi kuufikia ung'avu wa asili. Kusema La kuvunda halina ubani, yaweza isiwe sahihi sana; lakini Asiyesikia la mkuu huvunjika guu, ni sahihi kabisa. Ivumayo haidumu, lakini sasa JUNGU KUU KWA MARA YA KWANZA LITAKOSA UKOKO.

  TFDA fanya msako, choma vipodozi vyote vya kujichubua, vinginevyo CCM inajiumiza.

  Yangu macho mpaka 2015.
   
Loading...