Maswali muhimu kwa JK baada ya kujivua gamba!

Mhhhh! Kishabwabwaja! Sasa kama siku zote conflict sio unhealthy si wangemuacha Makamba tu aendelee!? Bado wana safari ndefu sana ya kukisafisha chama chao na kwa haya mabadiliko waliyoyafanya juzi bado hakuna mabadiliko yoyote ya maana.
Huko ni kujivua gani gamba sasa wakati sura zile zile zinaonekana, CHILIGATI ndani ya nyumba tena. Wamejipaka majivu/masizi na kudai eti wamejivua gamba. Mwenyekiti bado yule yule, makamu wenyeviti bado wale wale, Makamba blood bado imo, Mnauye blood imo pia utafikiri chama cha Kisultani?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
mwaka huu tutajionea mambo mpka basi...mwee CCM bana mnatufurahisha sana
 
He meant that having diversity of perspective ni vizuri ndani ya chama, mawazo mbali mbali ni mazuri sio chama kinakuwa unitary katika mawazo...hayo mambo ya ki communist hayafai. Lakini lazima wawe na umoja katika utekelezaji wa maamuzi na sera...angesema hivyo...

Well said.....nafikiri ambao hawajaelewa sasa watakuwa wameelewa nini alimaanisha akhsante sana..
 
Mheshimiwa.

Ni miezi mitano tu imepita toka asimame majukwaani na kushawishi watanzania wawachangue watu hawa! ukisema eti ni wasafi,wachapa kazi, jembe la zamani makali yale yale na ahadi nyingi tamu tamu kibao. Pia ulisisitiza na mara nying kwamba CHADEMA wasisikilizwe..maana ni waongo,wazushi,wadini,wakabila na waleta vita na wanatukana watu hawa. Tukiacha hizo ahadi ambazo umeshasema matatizo yetu huwezi kuyamaliza na utayaacha (hata cjui kwanini ulituoa ahadi za uongo sasa!). Lkn hili leo kali!, ni miez mitano tu imepita, wewe huyo huyo unaagiza kuwatimua hawa watu kwenye chama sababu ni mafisadi!!

Mheshimiwa, Vip wananchi waliodanganywa na kuwapa watu hawa dhamana ya kuwaongoza na wawakilishe bungeni !!?? kumbe ulikuwa unajua wanaenda kuwakilisha matumbo yao tu! Tukupe adhabu gani mheshimiwa kwa uongo huu?? Mheshimiwa, hebu chukua hatua unayostahili kujiadhibu mwenyewe, kama kweli umedhamilia kuvua gamba!!. Na hawa watu majimboni wafanywe nini ?? maana hawakuchagaliwa kwa ridhaa ya wananchi ...ila nikwa uongo wako, mheshimiwa??


Na huyu Wilson Mkama mbona ni mwenyekiti wa bodi ya Tz Standard Newspapers (TSN) inayochapisha magazeti ya serikali (Dailynews na Habari leo), na sasa mmempa ukatibu mkuu wa chama. Mheshimiwa umesahau kama haya magazeti ni ya watz siyo ya chama? Huo uamizi una dhana gani? .. Kuzika kabisa democrasia mliyokwishaiua?? ..au kuzidi kuua uhuru wa vyombo vya habari ?? ...au ndo mikakati ya kupunguza nguvu ya CHADEMA?? . Je wahitaji hata kwa hili tuandamane ndiyo utajua ni haki yetu!!?
 
Je pale watakapochangia chama michango ya kugharimia chaguzi za ndani na kampeni atafanyaje? Watarudishwa?
 
Tatizo ni mwandishi aliyemhoji, angemkumbusha historia yake pale halamshauri ya jiji, hakuwa mtendaji au mfuatiliaji mzuri akiwa mkurugenzi wa Dar city council, kwa mfano pale alipodai kwamba alikuta zaidi ya 2bn missing from Keenja's reign, baada ya kuyasema kwa wanahabari alikaa kimya, je kwenye mdude mkubwa ccm ataweza kupaza sauti?
 
Nimesikia kauli ya Chiligati kupitia TBC1 kwamba chama kimewapa muda watuhumiwa wote wa kashfa za Richmond, Kagoda, n.k wajipime na kuchukua uamuzi wa kujiuzulu wenyewe. Vinginevyo, eti chama kitawaondoa. Mzee Chiligati amefafanua vizuri kwamba hata kama chama hakina ushahidi ilimradi tu mtu ametajwatajwa na wananchi, basi ni vizuri ajiondoe mwenyewe.

Sijui kama alijiandaa kutoa kauli hiyo lakini naona kama utekelezaji wake unamkumba hata Mwenyekiti wake wa chama. Mara nyingi kikwete amehusishwa kwenye skendo nzito nzito kama za Richamond. Asipojiuzulu, nae watamwondoa nguvu?
Ni lini uliona viongozi wa CCM na serikali yake wakajiandaa kabla ya kuzungumza na umma? Kila mmoja hukurupuka tu na ukimwuliza Makamba atakwambia hizo ni kauli zao binafsi na si za chama. Kazi kweli kweli kwenye Chi-Chi-Em
 
hapa ccm wameibua mkebe mwingine .. dalili za mapema zaonyesha atajaza kiatu cha makamba perfectly
 
Nyoka akijivua gamba hawezi kugeuka kuwa kobe! Bado ni yale yale, maintanance of the same circle!
 
...nafikiri ambao hawajaelewa sasa watakuwa wameelewa nini alimaanisha akhsante sana..
Yeye kasema kuwa na migogoro ni vizuri kwa chama, period.

Tena kasema anaweza kulieleza hili Kiingereza kuliko Kiswahili maana Kiswahili kina matatizo, "conflict is healthy" for the party. Sasa apologists wake mnataka kusaidia kumtafsiria.

Pinda alivyoanza kuchemka siku ya kwanza anateuliwa mkamtolea tafsiri nyingi za "alichokuwa akimaanisha," baadae mkamchoka. Sasa huyu wengine tunaona hizi ni tell-tale signs za mtu asiye na umakini wa kuzingatia kinachoendelea kwenye chama sasa hivi.

Kuna tatizo la makundi anaambiwa,
yeye anasema migogoro ni healthy. Mchemfu mkubwa, bora Makamba!

Wilson-Mukama.jpg



 
CCM ipate kansa mara ngapi wakati tayari inaugua kansa iliyoingia hadi kwenye mifupa, ubongo na sana wanaweka vichochezi tu vya kuimarisha kansa mwilini mwao. Watakufa muda si mrefu hao.
 
Ni kweli jamani conflict ni nzuri, kwa kuwa conflict ni mwanzo wa mabadliliko ambayo huleta maendeleo, ila sasa inategemea na watu wenyewe waliopatwa na conflict hiyo mfumo wao wa kiutawala upo vipi, ukiwa mbaya ni balaa ukiwa mzuri ndio unaleta mabadiliko.Kwa mfano Canada kulitokea conflict kati ya chama tawala na vyama vya upinzani bungeni kuhusu vipaumbele vya taifa ktk bajeti ya mwaka ujao wa fedha, mvutano ulikuwa mkubwa ikabidi wabunge wapige kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu ambaye ndiye kama rais tz,hivyo wanafanya uchaguzi mpya kabla ya wakati yaani siyo lazima miaka mitano ifike. Kwa hiyo kama mfumo wa utawala ni mzuri conflict ni mwanzo wa mabadilko, ila sina hakika kama kwa mfumo wetu wa utawala tz conflict inaweza kuleta mabadiliko zaidi ya vurugu, hilo sina uhakika ila naona ni balaa.
 
Back
Top Bottom