Maswali magumu kwa Edward Ngoyai Lowassa

Maswali magumu kwa Edward Ngoyai Lowassa

ivi tanzania waziri mkuu ni mambo mengi??!!, ilo suala la kuuzwa uwanja wa ufi kwanini msiwaulize watu wa ardhi?, hauoni inawezekana ni kweli lowasa aliomba kwasababu ulizosema lakini kukawa na watu wengine ndio waliouza hilo eneo?

huyu lowasa kwa kudhulumu viwanja ni balaa. Huku moro amedhulumu pia eneo la wizara ya kilimo amejenga hotel kubwa inaitwa nashera . Huyo ni mchafu afahi kutuongoza watz
 
Hamna jibu hapo.Hizo nondo chungu na nzito hawawezi kujibu hilo genge la mafisadi
 
Kamweka Rosti tamu la azizi,bwana mleta RICHMOND awe meneja wake.

Joka la makengeza,a.k.a Mzee wa vijisenti Mzee wa rada,mbakaji Kapuya,Karamagi aliyekuwa anasaini mikataba ya serikali hotelini,hawa ndiyo waliomzunguka.

Alikuwa meneja wa jk wakitumia hela za EPA(kagoda) kuingia Ikulu,atapata wapo kiburi cha kukemea rushwa
 
huyu jamaa anajiita kasenge kweli.... yaani hukuweza kusikia akizungumzia suala la kupambana na rushwa kwa vitendo? usingeweza tena kwa jina kama lako concentration yako kubwa ilikuwa kwenye issue zinazokuhusu. waliokuwa wamesimama walisikia akzungumza suala hilo na kurudia. we ulikuwa umekaa usingeweza au kama uliinama masikio yalikuwa chini usingesikia kasenge.
 
hapo mnapishana kidogo tu,mh el amesema atapambana na ufisadi kwa vitendo...!?
sasa basi swali analouliza ka.... nani sijui ni wapi mh el alipambana na ufisadi.!? hapa naona swali lake linarenga kipindi cha uongozi wake wa uwaziri wowote pammoja na uwaziri mkuu,kwamba wapi mh el alipambana na ufisadi.....!? na sio atakapochaguliwa kuwa raisi baadae...ndukiiii😀
 
jibu la swali la kwanza ni kuwa.. asingepata cha kuongea sasa hivi. ndio maana aliamua kunyamaza ili alizungumzie kwa wakati muafaka
 
Ningechangia lkn Mods huwa hawaonyeshi commends zangu, licha ya kulilalamikia hilo mara kwa mara, that is why I decided to remain only the reader.
 
Nikiuliza kwanini watu wachache wanamchukia Lowasa eti sababu ya richmond.
Tafuta facts na uonge na sio kufuata mkumbo.
Nchi inajua Richmond ilikuwa dela ya mkuuu. Lowassa alijitoa kutuliza watu tu.Mbona escrow Pinda hakuachia ngazi?
Lowasa aliachia ngazi huku alikuwa hajui kuwa it was a plotting political assassination.
Hamna kitu kama hicho political assassination sio kweli kamati ya Mwakyembe ilitoa mpaka vimememo vyake kuwaelekeza waliochini chini yake watekeleze amri yake vyote viliwekwa hadharani bungeni!mbona hakuwahi kuvikana kwamba hayakuwa maelekezo yake?Jamani mkae mkijua wa TZ wa leo siwale wa zamani!Leo kusema tatizo ilikuwa uwaziri mkuu si kweli!Tatizo ni wa TZ wameibiwa na kudhulumiwa na yeye akiwa kiranja wa uovu wote!ifikie mahali mjue wa TZ tuna ubongo wa reasoning capacity!asinge stahili kujuuzulu kama shida ilikuwa cheo chake!kamati ilikuja na facts na ushahidi ulio wazi kama angelikuwa na ushahidi contrary angeuwakilisha palepale bungeni!hakufanya hivyo coz alianikwa mchana peupe na kamati ya bunge!Leo anamsingizia Raisi?Hoja muflisi!Raisi hajawahi kuandika memo hata moja!huyu mzee my take ni muongo na huo uongo utamgharimu kwenye safari yake ya matumaini!Mungu ibariki TZ bariki na watu wake....
 
Kasenge jaribu kupata takwimu za UFISADI kwenye halmashauri kabla, wakati akiwa PM na baada ya kujiuzulu kwake... Kupambana na UFISADI si kupiga mayowe hadharani...
We ndo umekalia Dude la Lowassa hadi masikio umeziba. Wapi Lowassa amepambana na ufisadi kwa vitendo.
 
Tukimchagua lowasa hii nchi ndotunaenda kuizika yani tutajuta eti safari ya matumaini ndo inaanza hizo nipolojo tu ha mwenzake alisema maisha bora kwa kila mtz yakowapi tatizo CCM ni kama ukoo wa panya baba mwizi mama mwizi kaka mwizi dada mwizi au nisawa na mywa viloba ambae vimesha ingia kwenye dam kuacha sio laisi nahuyo jamaa kuacha wizi sio lais coz uko kwenye dam mwalim nyerere alitawala mda mrefu ila hakuacha mali kama za huyo jamaa halafu biashara na siasa wapi na wapi

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Lowassa ni mtu wa maamuzi magumu. Hivyo ameamua kutojibu haya maswali maana pia ni magumu. Uliza maswali kama yale waliyouliza wahariri Dodoma. Kwa mfano
1. Mheshimiwa umependeza na suti hiyo, je ni ghali?
2. Mheshimiwa Unapenda kula nini?
3. Je, Maendeleo ya jimbo lako yanasifiwa sana?
 
Kamweka Rosti tamu la azizi,bwana mleta RICHMOND awe meneja wake.

Joka la makengeza,a.k.a Mzee wa vijisenti Mzee wa rada,mbakaji Kapuya,Karamagi aliyekuwa anasaini mikataba ya serikali hotelini,hawa ndiyo waliomzunguka.

Alikuwa meneja wa jk wakitumia hela za EPA(kagoda) kuingia Ikulu,atapata wapo kiburi cha kukemea rushwa
Usisahau mhindi muuaji. Fazal wa Leopard tours. Ni best yake. Mtakomaje mwaka huu
 
Mkuu
072, afisa uhusiano na msemaji wa Lowassa sio ndugu Pasco, bali ni Aboubakar Liongo!.

Pasco wa jf, sio mwanachama, mshabiki, mfuasi wa chama chochote cha siasa hivyo sio mpambe wa mwanasiasa yoyote!, ila Pasco wa jf ni mtu mkweli daima anayesema ukweli wa kupindukia!, huwa anausema ukweli halisi jinsi ile ile ulivyo bila kumungunya maneno na bila kujali ukweli huo, utamfurahisha nani au utamuudhi nani!.

Sasa miongoni mwa ukweli mchungu kumeza kuihusu nchi yetu ni kuwa 2015 CCM ndio itachukua tena nchi!. Ukweli mchungu kumhusu Lowassa, he is the one and only best option that CCM has!, and he can make the best president this country has ever had apart from Mwalimu Nyerere!, sababu ni moja tuu "He has the powers to make things happen!".

Ukweli una tabia moja tuu!, husimama mpaka mwisho!.

Pasco

PASCO, siku zote na kusoma kama mtu muelewa (good analyst) Ebu kwa tabia za Lowassa, dictatorship kwake ipo au haipo? Utakuwa unajua Idd Amin Dada alipompindua Dr. Milton Obote mamilioni ya watu walijimwaga mitaani kufurahia na kutamka kuwa Uganda imezaliwa upya kwa huyo mwana jeshi ambaye ilisemekana he was always mean, no nonsense man tayari kuwaongoza Waganda kwenye nchi ya maziwa na asali. Soma historia alikuwa anafanya maamuzi bila kufikiria kama mawazo ya watu wengine yako sahihi. Hii tabia si ndio ya Lowassa? Tofauti ya Lowassa na Idd Amin ni kuwa yeye ni tajiri na sio mwana jeshi. Huwezi kujiuliza kwa nini ana utajiri wa kuweza kuishi duniani kana anayeishi mbinguni lakini sasa badala yake anatokwa jasho jingi na kuhonga sana, kugharamikia sana na kununua kila kilicho mbele yake isipokuwa maskini ili mradi apate urais? Ktk ubunge huko Karagwe Sir George Kahama aliupata kwa mtindo huu. Baada ya kuupata akatokomea Dar, ikawa ni kutoka kwake Dar na kwenda kubarizi bungeni na baada ya Bunge kurudi kwake Dar. Baada ya miaka kadhaa akawa amerudi huko Karagwe. walipomuuliza kuwa kapotelea wapi aliwambia dhahiri bin shairi. Kuwa alikuwa anafaidi pesa zake maana ubunge alionao si mapenzi ya wapiga kura kwake bali ni pesa yake maana ana ubunge wa kununua. Je Lowassa si anaenda kupata urais wa kununua? Pasco Watanzania zaidi ya 80% ni wakulima. Na ktk hao wakulima 96% ni wakulima maskini yaani wa kulima na jembe la mkono. Hawa ndio wengi nyumba zao ndio zile zinaitwa mbavu za mbwa. Ndio wale hula chakula kisicho lishe. Ndio hawa watoto wao sana sana ni sekondari za kata na akiugua lazima afe. Anakuja Lowassa ktk kutangaza nia hakuna muwakilishi hata mmoja kati ya wao . Anatamba kuwa anapenda matajiri hawapendi maskini. (Pasco ebu nitafutie kwa % ya uchumi wa Tanzania unavyo milikiwa, wakulima wana % ngapi? Najaribu kufikiria labda ni chini ya 20%. Hawa >80% Lowassa anazungumzia kuwafanya matajiri yaani waingie ktk kumiliki 80% ya uchumi ambayo muda mwingi imekuwa ikimilikiwa na yeye na rafiki zake. Tusemezane anataka kwenda kuleta mfumo wa kurudisha mali kwa wenyewe kistarabu? Rafiki zake wanataka kupitia kwake kutubu kwa Watanzania? Pasco unaishi sijui wapi? Unatarajia nini pale bubu anapo zidiwa? Hujui bubu huyu anaweza kusema? Sasa ccm inataka mabubu Watanzania waseme? Is ccm ready for that. Ebu muulize Lowassa ajibu maswali hapo juu kama wewe ni freelance. Matatizo yetu sio mtu matatizo yetu ni mfumo. Kwa mfumo wa CCM Malaika lazima ageuke shetani.
 
Mkuu kayamgo, haya usemayo haya yote ni kweli, ni kweli Lowassa ni fisadi, ni tajiri anauchukia umasikini!, na pia ni kweli CCM sasa imehodhiwa na mafisadi hivyo ni chama cha kifisadi, na kupata uongozi ndani ya CCM sasa ni kupitia rushwa, na urais wa siku hizi ni kununua!. Tangu ile 2005 JK alikuwa ni masikini, lakini ni Lowassa ndiye aliyemsaidia kupata pesa za kuununua urais kupitia Kagoda hivyo JK pia aliununua urais, hivyo kama urais sasa ni bidhaa!, and it is for sale!, na wewe umeipenda bidhaa hiyo, na umeikuta iko dukani for sale, umeona bei yake na kama unazo hizo fedha, why not buy it?!.

Kwa vile JK ni masikini lakini alisaidiwa kuununua urais, Watanzania tumeendelea kuwa masikini as reflection ya kiongozi wetu mkuu!, JK ni masikini na hajawahi kuuchukia umasikini!, as a result Watanzania bado ni masikini!. Lowassa sio masiki ni tajiri, anapenda utajiri, anauchukia umasikini, akiingia madarakani atautokomeza umasikini na kila Mtanzania atakuwa tajiri!.

Niliwahi kusikiliza mahubiri fulani ya Mchungaji Getrude Rwakatare, alisema Umasikini ni laana!. Tanzania ni taifa lenye laana ya umasikini kutoka na kuchagua viongozi masikini!. 2015 tusichague tena kiongozi masikini ili tuondokana na hii laana ya umasikini!.

Say Yes to Lowassa, say Kwaheri umasikini!.

Pasco
 
Back
Top Bottom