Maswali magumu kwa Edward Ngoyai Lowassa

Maswali magumu kwa Edward Ngoyai Lowassa

Mtanzania mwenye akili timamu busara na asiye mpambe hawezi kusema Lowassa anafaa kuwa Rais. Nchi hii italiwa na wachache mpaka lini jamani..Maana kwa Lowassa sioni jipya ni wale wale waarabu wa Pemba.
 
Mkuu
072, afisa uhusiano na msemaji wa Lowassa sio ndugu Pasco, bali ni Aboubakar Liongo!.

Pasco wa jf, japo ni mwanachama, wa chama cha siasa, lakini sio mshabiki, mfuasi na sio mpambe wa mwanasiasa yoyote!, ila Pasco wa jf ni mzalendo na mtu mkweli daima anayesema ukweli wa kupindukia!, huwa anausema ukweli halisi jinsi ile ile ulivyo bila kumungunya maneno na bila kujali ukweli huo, utamfurahisha nani au utamuudhi nani!.

Sasa miongoni mwa ukweli mchungu kumeza kuihusu nchi yetu ni kuwa 2015 CCM ndio itachukua tena nchi!. Ukweli mchungu kumhusu Lowassa, he is the one and only best option that CCM has!, and he can make the best president this country has ever had apart from Mwalimu Nyerere!, sababu ni moja tuu "He has the powers to make things happen!".

Ukweli una tabia moja tuu!, husimama mpaka mwisho!.

Pasco
 
Mkuu 072, afisa uhusiano na msemaji wa Lowassa sio ndugu Pasco, bali ni Aboubakar Liongo!.Pasco wa jf, sio mwanachama, mshabiki, mfuasi wa chama chochote cha siasa hivyo sio mpambe wa mwanasiasa yoyote, ila Pasco wa jf ni mtu mkweli daima kupindukia, huwa anausema ukweli halisi jinsi ulivyo bila kujali ukweli huo, utamfurahisha nani, sasa miongoni mwa ukweli mchungu kumeza kumhusu Lowassa, he is the one and only best option the CCM has, and he can make the best president this country has ever have apart from Nyerere!, sababu ni moja tuu "He has the powers to make things happen!".
Pasco

Unaonaje kama badala ya kubwabwaja ungejibu hayo maswali ukiwa kama mpambe na shabiki wa Lowasa?
 
MASWALI MAGUMU KWA MH. EDWARD NGOYAI LOWASA
Kwako mh. Edward Lowassa,
Ni matumaini yetu kuwa u mzima wa afya. Kuelekea mchakato wa Urais mwaka huu tumesikia kuwa nawe baba utatangaza nia. Sisi wananchi wa mtaani tunayo maswali machache tunaomba utusaidie tupate kujua wakati utakapotangaza nia yako rasmi uwanja wa Sheikh Abeid Karume huko Arusha. Maswali yetu ni machache tu mh. mpendwa:-
1.Tangu umejiuzulu nafasi yako ya uwaziri mkuu kufuatia kashfa ya ufisadi wa Richmond, imekuchukua miaka 7 kujitetea mbele ya umma.Ulikua wapi muda wote huo?
2.Umelieleza taifa na dunia kuwa hukufanya kazi sehemu yoyote zaidi ya CCM tangu mwaka 1977, Je utajiri ulionao umeutoa wapi? Huko CCM kuna biashara gani ulifanya?
3.Kwanini hujawahi na inaonekana huwezi kukemea wala kuzungumzia Rushwa na ufisadi? Unatofautiana vipi na kauli ya mwenyekiti mwenza wa UKAWA mh Freeman Mbowe kuwa wewe ni "dhaifu, usiyeweza kukemea rushwa, ufisadi na ubadhirifu?"
4.Kwanini sehemu kubwa ya wanaokuunga mkono ni wale ambao walifeli au kukataliwa na wananchi au kufukuzwa kazi katika nafasi mbalimbali za chama na serikali kwa kashfa? Mfano Rostam Azizi, Nazir Karamagi, Andrew Chenge, Lawrence Masha, Juma Kapuya, Cyril Chami n.k?
5.Ulizipataje hisa zako unazomiliki VODACOM? Ulizinunua lini na kwa kiasi gani?
6.Wakati unaajiriwa na CCM kama katibu msaidizi miaka ya 70, inasemekana ulimuibia baba yako mzazi ng'ombe ukawauza na kununua gari, kisha mzee wako akaenda kukushitaki kwa viongozi wa Chama kuwa hufai na ufukuzwe kazi. Je, hii ni kweli?
7.Wewe ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM taifa, kikao kinachojadili na kuamua mambo makubwa ya kusimamia serikali inayotawala. Je,umewahi kujenga hoja zipi za kutetea wananchi? Kusimamia serikali? Mara ngapi? Lini?
8.Tangu umekua mwenyekiti wa kamati ya bunge ya mambo ya nje miaka mitano sasa, wewe ni mwenyekiti pekee ambae hujawahi kusimama hata mara moja kusoma taarifa ya kamati bungeni. Je, ni kwanini? Tatizo ni afya yako inakufanya usiweze kusimama kuongea kwa muda mrefu au nini?
9.Kwanini unatumia pesa nyingi sana kutafuta urais wa nchi? Pesa hizo utazirudishaje kwa hao unaowaita marafiki zako? Ikulu kuna biashara gani? Je, ikiwa Urais unanunuliwa, sisi watoto wa masikini watoto wetu wajifunze nini? Kuwa wataendelea kubaki katika tabaka la watawaliwa hadi watakapokuwa na mabilioni ya kutosha?
10.Kumbukumbu zinaonesha kuwa hayati mwalimu Julius Nyerere aliwahi kukukataa kutokana na kuonekana ukiwa na ukwasi usio na maelezo,Je, uliwahi kumjibu mwalimu kabla ya umauti wake kuwa ulipataje mali zako? Ili arekebishe kauli yake?
NAKUOMBA UTUSAIDIE SISI WANYONGE TUJUE KAMA TUNAWEZA KUKUAMINI KWA HILO UNALOOMBA.MAANA TUNA MASHAKA.
WAANDISHI MLIOZUNGUMZA NA LOWASA MLIPASWA KUMUULIZA MASWALI HAYA.
Tunatanguliza shukrani,
Ni sisi wananchi wa kawaida mtaani.
Kolimba Jr.
 
Wizi ni hulka ya mtu. Kumbe alianza Wizi kwa kumuibia baba yake Ng'ombe!! Mpk Leo anaendeleza Wizi na unafiki.
 
akijibu haya mimi nahamia chichiem tena nitampigia kampeni huku kijijini kwetu
 
Lowasa anahasira sana, akiulizwa maswali asiyokuwa na majibu nayo anasonya na ku crush hilo swali. Anajazba. Juzi waati anaulizwa maswali magumu kidogo anawahi kusema nitayajibu arusha, ile hali akijua arusha ataleta blabla zake na hakuta kuwa na maswali tena. Hopeless politician
 
Mkuu 072, afisa uhusiano na msemaji wa Lowassa sio ndugu Pasco, bali ni Aboubakar Liongo!.Pasco wa jf, sio mwanachama, mshabiki, mfuasi wa chama chochote cha siasa hivyo sio mpambe wa mwanasiasa yoyote, ila Pasco wa jf ni mtu mkweli daima kupindukia, huwa anausema ukweli halisi jinsi ulivyo bila kujali ukweli huo, utamfurahisha nani, sasa miongoni mwa ukweli mchungu kumeza kumhusu Lowassa, he is the one and only best option the CCM has, and he can make the best president this country has ever have apart from Nyerere!, sababu ni moja tuu "He has the powers to make things happen!".
Pasco

Aise kiongozi wewe ni mtu hatari sana tena sana.mtu mwenye akili akisoma hili andiko lako atakuelewa.don't fools people. Hiyo ofisi unayofanyia kazi wachukue tahadhari mkuu wewe ni zaidi ya Nyoka.
 
Mkuu 072, afisa uhusiano na msemaji wa Lowassa sio ndugu Pasco, bali ni Aboubakar Liongo!.Pasco wa jf, sio mwanachama, mshabiki, mfuasi wa chama chochote cha siasa hivyo sio mpambe wa mwanasiasa yoyote, ila Pasco wa jf ni mtu mkweli daima kupindukia, huwa anausema ukweli halisi jinsi ulivyo bila kujali ukweli huo, utamfurahisha nani, sasa miongoni mwa ukweli mchungu kumeza kumhusu Lowassa, he is the one and only best option the CCM has, and he can make the best president this country has ever have apart from Nyerere!, sababu ni moja tuu "He has the powers to make things happen!".
Pasco

Unajua kuna wakati pasco huwa nakuona kama umevulugikiwa na akili, yaan kwa mtu kama ww na mkongwe jf unajitoa ufahamn kiasi hiki, ama kweli nimeamini pesa(rushwa) ni mbaya..

Lowasa huyu leo awe rais??
Tunapaswa kukupima akili maana huenda ukawa umechanganyikiwa...
Ushaur nenda hosp ukaexamine afya,
 
Hao marafiki zake wanaomgawia hela ya kutapanya kwenye kampeni ni kina nani?? Kwa nini hili asiuliZwe nà vyombo vya dola? Au ndo hivyo dola imeshapata ganzi?
 
Nilikuwa namkubaali huyu lowassa ila sasa naona nilikuwa under peer pressure hafai huyu mtu sio kiongozi ni mwizi mkubwa
 
Nikiuliza kwanini watu wachache wanamchukia Lowasa eti sababu ya richmond.
Tafuta facts na uonge na sio kufuata mkumbo.
Nchi inajua Richmond ilikuwa dela ya mkuuu. Lowassa alijitoa kutuliza watu tu.Mbona escrow Pinda hakuachia ngazi?
Lowasa aliachia ngazi huku alikuwa hajui kuwa it was a plotting political assassination.
 
Back
Top Bottom