Maswali magumu kwa Edward Ngoyai Lowassa

Maswali magumu kwa Edward Ngoyai Lowassa

Pasco, wewe unamkubali sana Lowassa na unaamini anaweza kuisukuma nchi yetu kwenye maendeleo tunayoyataka. Nina ombi moja kwako. Pamoja na maswali aliyoyauliza mleta mada, naomba unisaidie kumuuliza Lowassa ni kwa nini aliuuza uwanja wa UFI? Uwanja wa UFI ilikuwa sehemu ambayo wakazi wa Ubungo na Mabibo na hasa watoto walikuwa wanacheza mipira na kufanya mazoezi. Lowassa akiwa waziri mkuu alikuja kwa lugha laini kwamba anaomba autumie uwanja huo kuweka mabomba kwa ajili ya mradi wa maji kutoka Mwanza mpaka Shinyanga. Alisema hiyo itakuwa ni kwa muda tu na mradi ukiisha, uwanja huo utarudishwa kwa wananchi.

Ni kweli mabomba yaliwekwa lakini muda kidogo ujenzi wa ukuta kuzunguka huo uwanja ulianza. Wananchi walipinga kitendo hicho na hatimae ujenzi uliendelea chini ya ulinzi wa polisi wenye silaha nzito. Mradi wa maji uliisha na sasa mle ndani tunaona malori yanapaki mle ndani.

Kitendo hiki kilinifanya nimuone Lowassa kama kiongozi asiyefaha kwani kuchukua eneo la wazi lililokuwa linatumika kwa michezo na kuliuza akikitarajiwa kutoka kwa kiongozi wa ngazi za juu kama yeye.

Tafadhali muulize ni kwa nini aliuuza uwanja wa UFI. Wakazi wa eneo hili bado tuna machungu ya kuchukuliwa eneo letu la michezo.

Tiba
 
Kama makocha wa kibongo wakivurunda 2nakodi nje Why 2sikod rais Mjeruman
Kama kila kiwanda kimebinafsishwa kwa kukosa wazalendo wakuviendesha ni bora akatafutwamwekezaji ikulu huenda atakuwa na huruma na nchi hii, kuliko huyu fisadi aliyeunda genge la kumpigia debe,hao wapambe wake ni watu wenye historia mbaya na baadhi yao walisha fukuzwa kwenye utumishi wa umma, yeye mwenyewe alijigawia ranchi ya taifa na pesa za kufufulia general tyre anazitumia kuhonga watu.
 
Pasco, wewe unamkubali sana Lowassa na unaamini anaweza kuisukuma nchi yetu kwenye maendeleo tunayoyataka. Nina ombi moja kwako. Pamoja na maswali aliyoyauliza mleta mada, naomba unisaidie kumuuliza Lowassa ni kwa nini aliuuza uwanja wa UFI? Uwanja wa UFI ilikuwa sehemu ambayo wakazi wa Ubungo na Mabibo na hasa watoto walikuwa wanacheza mipira na kufanya mazoezi. Lowassa akiwa waziri mkuu alikuja kwa lugha laini kwamba anaomba autumie uwanja huo kuweka mabomba kwa ajili ya mradi wa maji kutoka Mwanza mpaka Shinyanga. Alisema hiyo itakuwa ni kwa muda tu na mradi ukiisha, uwanja huo utarudishwa kwa wananchi.

Ni kweli mabomba yaliwekwa lakini muda kidogo ujenzi wa ukuta kuzunguka huo uwanja ulianza. Wananchi walipinga kitendo hicho na hatimae ujenzi uliendelea chini ya ulinzi wa polisi wenye silaha nzito. Mradi wa maji uliisha na sasa mle ndani tunaona malori yanapaki mle ndani.

Kitendo hiki kilinifanya nimuone Lowassa kama kiongozi asiyefaha kwani kuchukua eneo la wazi lililokuwa linatumika kwa michezo na kuliuza akikutarajiwa kutoka kwa kiongozi wa ngazi za juu kama yeye. Ukiwa waziri mkuu halafu huwezi kulinda sehemu za wazi, then una matatizo makubwa.

Tafadhali muulize ni kwa nini aliuuza uwanja wa UFI. Wakazi wa eneo hili bado tuna machungu ya kuchukuliwa eneo letu la michezo.

Tiba
 
Nikiuliza kwanini watu wachache wanamchukia Lowasa eti sababu ya richmond.
Tafuta facts na uonge na sio kufuata mkumbo.
Nchi inajua Richmond ilikuwa dela ya mkuuu. Lowassa alijitoa kutuliza watu tu.Mbona escrow Pinda hakuachia ngazi?
Lowasa aliachia ngazi huku alikuwa hajui kuwa it was a plotting political assassination.

Mkuu hamna aliyezungumzia richmond hapa maswali ni mengi alinayoulizwa mheshimiwa na sidhani kama anamajibu.kama wewe ni mzalendo na unampenda lowassa embu mfikishie haya maswali tupate kujua ukweli
 
Maswali mazuri sana haya nina uhakika kama atayapangua vizuri haya maswali atakuwa na nafasi kubwa sana ya kuingia mjengoni magogoni.
 
MASWALI MAGUMU KWA MH. EDWARD NGOYAI LOWASA
Kwako mh. Edward Lowassa,
Ni matumaini yetu kuwa u mzima wa afya. Kuelekea mchakato wa Urais mwaka huu tumesikia kuwa nawe baba utatangaza nia. Sisi wananchi wa mtaani tunayo maswali machache tunaomba utusaidie tupate kujua wakati utakapotangaza nia yako rasmi uwanja wa Sheikh Abeid Karume huko Arusha. Maswali yetu ni machache tu mh. mpendwa:-

1.Tangu umejiuzulu nafasi yako ya uwaziri mkuu kufuatia kashfa ya ufisadi wa Richmond, imekuchukua miaka 7 kujitetea mbele ya umma.Ulikua wapi muda wote huo?

2.Umelieleza taifa na dunia kuwa hukufanya kazi sehemu yoyote zaidi ya CCM tangu mwaka 1977, Je utajiri ulionao umeutoa wapi? Huko CCM kuna biashara gani ulifanya?

3.Kwanini hujawahi na inaonekana huwezi kukemea wala kuzungumzia Rushwa na ufisadi? Unatofautiana vipi na kauli ya mwenyekiti mwenza wa UKAWA mh Freeman Mbowe kuwa wewe ni "dhaifu, usiyeweza kukemea rushwa, ufisadi na ubadhirifu?"

4.Kwanini sehemu kubwa ya wanaokuunga mkono ni wale ambao walifeli au kukataliwa na wananchi au kufukuzwa kazi katika nafasi mbalimbali za chama na serikali kwa kashfa? Mfano Rostam Azizi, Nazir Karamagi, Andrew Chenge, Lawrence Masha, Juma Kapuya, Cyril Chami n.k?

5.Ulizipataje hisa zako unazomiliki VODACOM? Ulizinunua lini na kwa kiasi gani?

6.Wakati unaajiriwa na CCM kama katibu msaidizi miaka ya 70, inasemekana ulimuibia baba yako mzazi ng'ombe ukawauza na kununua gari, kisha mzee wako akaenda kukushitaki kwa viongozi wa Chama kuwa hufai na ufukuzwe kazi. Je, hii ni kweli?

7.Wewe ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM taifa, kikao kinachojadili na kuamua mambo makubwa ya kusimamia serikali inayotawala. Je,umewahi kujenga hoja zipi za kutetea wananchi? Kusimamia serikali? Mara ngapi? Lini?

8.Tangu umekua mwenyekiti wa kamati ya bunge ya mambo ya nje miaka mitano sasa, wewe ni mwenyekiti pekee ambae hujawahi kusimama hata mara moja kusoma taarifa ya kamati bungeni. Je, ni kwanini? Tatizo ni afya yako inakufanya usiweze kusimama kuongea kwa muda mrefu au nini?

9.Kwanini unatumia pesa nyingi sana kutafuta urais wa nchi? Pesa hizo utazirudishaje kwa hao unaowaita marafiki zako? Ikulu kuna biashara gani? Je, ikiwa Urais unanunuliwa, sisi watoto wa masikini watoto wetu wajifunze nini? Kuwa wataendelea kubaki katika tabaka la watawaliwa hadi watakapokuwa na mabilioni ya kutosha?

10.Kumbukumbu zinaonesha kuwa hayati mwalimu Julius Nyerere aliwahi kukukataa kutokana na kuonekana ukiwa na ukwasi usio na maelezo,Je, uliwahi kumjibu mwalimu kabla ya umauti wake kuwa ulipataje mali zako? Ili arekebishe kauli yake?
NAKUOMBA UTUSAIDIE SISI WANYONGE TUJUE KAMA TUNAWEZA KUKUAMINI KWA HILO UNALOOMBA.MAANA TUNA MASHAKA.
WAANDISHI MLIOZUNGUMZA NA LOWASA MLIPASWA KUMUULIZA MASWALI HAYA.
Tunatanguliza shukrani,
Ni sisi wananchi wa kawaida mtaani.

MASWALI YAKO NI MEPESI SANA, MAJIBU KAMA IFUATAVYO:
1.Alijuuzulu uwaziri mkuu kutokana na dhana ya uwajibikaji sio kwa sababu alihusika na ufisadi wa richmond kuhusu kujitetea baada ya miaka 7 inatokana na kamati ya mwakyembe kutoa hukumu bila ya kumpa nafasi ya kujitetea wakati wakifanya uchunguzi. rejea misingi ya haki ya asili(principle of natural justice)
2.kuhusu suala la utajiri ni mipango binafsi na kufanya kazi kwa bidii mfano mtu anaweza kukopa akajipanga vizuri ktk miradi yake akafanikiwa i.e Lowasa ni mfugaji kiasili km alijipanga vizuri akawa na mifugo zaidi 1000 ni utajiri tosha
3.kukemea rushwa na ufisadi sio lazima akemee majukwaani km anavyofanya mbowe ili apate sifa wakati chama chake(CDM) kina harufu ya ufisadi rejea sakata la kufukuza wahindi matapeli waliopata dili ya kusambaza maji Dar es salaam jinsi lowasa alivyosimamia kivitendo sio maneno
4.tupe ushahidi km hao watu unaowataja kweli wanamuunga mkono lowasa na hata km kweli shida ipo wapi wakati kila mtu anayo haki ya kufanya jambo lolote bila kuvunja sheria
5.kwanini unataka kujua hisa za mtu? wewe una maslahi gani na vodacom hizo ni biashara binafsi sio lazima kila kitu aweke hadharani ndio mana kuna mkataba ambao ni wa pande mbili(lowasa vs vodacom)
6.tupe ushahidi wa lowasa kumuibia baba yake ng'ombe,tuambie zilikuwa ngapi,zenye dhamani gani na hiyo gari alinunua wapi, aina gani na shilingi ngapi
7.suala la maamuzi,agenda na hoja ktk halmashauri kuu ya c.c.m nakushauri nenda makao makuu ukaombe nakala za mihutsari ya vikao vya wakati(1970s) huo nadhani utapata picha ya michango ya mh lowasa
8.kuwa mwenyekiti wa kamati ya bunge ya mambo ya nje hakumlazimishi mwenyekiti kusoma taarifa za kamati,cha msingi ni utekelezaji wa majukumu ya msingi ya kamati
9.tupe ushahidi dhahiri unaoonyesha kuwa lowasa anagawa pesa na je kwanini unafikiria pesa ni motisha pekee inayofanya watu kumsupport lowasa?, je hauoni ya kuwa watu wanashawishika kumsupport lowasa kutokana na uongozi,historia,uvumilivu na kujituma kwake?
10.nyerere hakuwahi kumkataa lowasa ila km una uhakika na maneno yako leta ushahidi
N.B; Jamani tusikubali kusikia maneno ya vijiweni pasipo kuwepo ushahidi dhahiri kisha unayameza kama yalivyo tena bila hata kufanya uchunguzi wa kina. Ndio mana upinzani wa Tanzania umedumaa kwa sababu hawana hoja ila mara nyingi wanapenda kuongea majungu,umbeya na unafiki ili wapate huruma ya wananchi
 
Ng'ombe 1000 hata kila mmoja akiuzwa kwa sh. Milioni moja jumla ya fedha tote haizidi 1Bil. Hata hivyo Hilo shamba lake la ng'ombe 1000 liko Wapi? Hizi kauli za jumla jumla tu eti kufanya kazi kwa bidii hazisaidii. Mtu hatajiriki tu: kwa bidii gani wakati alikuwa mtumishi wa mshahara? Hizo biashara zake alizianzaanzaje? Kina Dewji,Mengi,Bakhresa biashara zap zinaonekana. Zake ziko Wapi? Au hao marafiki zake wanaomgawia kina nani? Kwa nini wampe yeye?
 
pasco, wewe unamkubali sana lowassa na unaamini anaweza kuisukuma nchi yetu kwenye maendeleo tunayoyataka. Nina ombi moja kwako. Pamoja na maswali aliyoyauliza mleta mada, naomba unisaidie kumuuliza lowassa ni kwa nini aliuuza uwanja wa ufi? Uwanja wa ufi ilikuwa sehemu ambayo wakazi wa ubungo na mabibo na hasa watoto walikuwa wanacheza mipira na kufanya mazoezi. Lowassa akiwa waziri mkuu alikuja kwa lugha laini kwamba anaomba autumie uwanja huo kuweka mabomba kwa ajili ya mradi wa maji kutoka mwanza mpaka shinyanga. Alisema hiyo itakuwa ni kwa muda tu na mradi ukiisha, uwanja huo utarudishwa kwa wananchi.

Ni kweli mabomba yaliwekwa lakini muda kidogo ujenzi wa ukuta kuzunguka huo uwanja ulianza. Wananchi walipinga kitendo hicho na hatimae ujenzi uliendelea chini ya ulinzi wa polisi wenye silaha nzito. Mradi wa maji uliisha na sasa mle ndani tunaona malori yanapaki mle ndani.

Kitendo hiki kilinifanya nimuone lowassa kama kiongozi asiyefaha kwani kuchukua eneo la wazi lililokuwa linatumika kwa michezo na kuliuza akikutarajiwa kutoka kwa kiongozi wa ngazi za juu kama yeye. Ukiwa waziri mkuu halafu huwezi kulinda sehemu za wazi, then una matatizo makubwa.

Tafadhali muulize ni kwa nini aliuuza uwanja wa ufi. Wakazi wa eneo hili bado tuna machungu ya kuchukuliwa eneo letu la michezo.

Tiba
ivi tanzania waziri mkuu ni mambo mengi??!!, ilo suala la kuuzwa uwanja wa ufi kwanini msiwaulize watu wa ardhi?, hauoni inawezekana ni kweli lowasa aliomba kwasababu ulizosema lakini kukawa na watu wengine ndio waliouza hilo eneo?
 
ivi tanzania waziri mkuu ni mambo mengi??!!, ilo suala la kuuzwa uwanja wa ufi kwanini msiwaulize watu wa ardhi?, hauoni inawezekana ni kweli lowasa aliomba kwasababu ulizosema lakini kukawa na watu wengine ndio waliouza hilo eneo?

Hivi wewe ndie Pasco? Mimi nimemwomba Pasco amuulize Lowassa au wewe ndie Lowassa? Kama wewe sio Lowassa, kaa kimya. Nina uchungu ujue?

Tiba
 
hivi wewe ndie pasco? Mimi nimemwomba pasco amuulize lowassa au wewe ndie lowassa? Kama wewe sio lowassa, kaa kimya. Nina uchungu ujue?

Tiba

ungemfuata nyumbani kwake, huu ni mtandao wa kijamii acha ukuda mtu yoyote anaweza kujibu
 
ungemfuata nyumbani kwake, huu ni mtandao wa kijamii acha ukuda mtu yoyote anaweza kujibu

Huna majibu halafu unajitia kujibu. Unaniongezea hasira ujue? Mtu ambaye hawezi kutambua umuhimu wa maeneo ya wazi hatufai kabisa huyo .

Tiba
 
Huna majibu halafu unajitia kujibu. Unaniongezea hasira ujue? Mtu ambaye hawezi kutambua umuhimu wa maeneo ya wazi hatufai kabisa huyo .

Tiba[/QUOTE
KWANI JAMII FORUM NDIO WIZARA YA ARDHI? KM UNATEGEMEA UTAPATA MAJIBU HUMU BASI UMEKOSEA MLANGO JARIBU SEHEMU NYINGINE ALAFU HUNA SABABU KUPADWA NA HASIRA UTAPATA VIDONDA VYA TUMBO BURE KWA TANZANIA SUALA LA KUUZWA VIWANJA VYA WAZI NI KILA SEHEMU SIO HUKO KWENU PEKEE HATA KWETU LIPO. "Usisubiri wanasiasa wafanye mabadiliko, mabadiliko ya kweli yanaanza na wewe"
 
Nilitegemea leo Mzee wetu anayekubalika na wananchi wengi aongelee tatizo la Rushwa na Ufisadi mambo yanayotukwamisha. Lakini, kataja vipaumbele vingine kama elimu na kuondoa umaskini. Kwa ujumla, kama huwezi kuondoa Rushwa na Ufisadi tutaendelea kuogelea katika dimbwi la umaskini. Wale wapambe wa mzee, mwambieni japo ayagusie hata kama Roho inamsuta, lakini japo tutafarijika na kumhukumu nayo hapo mbeleni.
 
kasenge mbona unalialia kama umekalia DUDE! ... Lowassa hapambani ni Rushwa kwa maneno matupu! Yeye ni mtu wa vitendo na leo ameweka bayana... tafuta hotuba yake uelimike Zaidi ...
 
Back
Top Bottom