WanaJF!
Kuna imani kwamba CHADEMA ndio matumaini ya watanzania lakini pia kuna imani tena iliyo kali kuwa ndani ya CHADEMA ni mtu mmoja tu aitwae Dr Slaa ndie mwenye uhalali wa kugombea urais kupitia chama hicho kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Mimi kama mtanzania wa kawaida ningependa kuaminishwa kuhusu 'ujembe' wa mtu huyo mmoja ambae ina sadikiwa kuwa atakuwa rais wetu ajae, maana sioni sababu ya kuendelea kuwa tofauti na wapenda mabadiliko wakati wenda kuna hoja za msingi tu zakunishawishi.
Ningependa majibu kutoka kwa wapenda mabadiliko kuhusu maswali yafuatayo;
1. RUSHWA, ni kwa namna gani Dr Slaa ataweza kupambana na adui rushwa ilhali kwa sasa ndani ya chama kuna harufu iliyo pindukia ya ulaji rushwa?, kwenye hili la rushwa ndani ya CHADEMA hufanywa sana kipindi cha kuomba kugombea nafasi ndani ya chama hicho au kugombea nafasi ya udiwani na ubunge kupitia chama hicho, na rushwa inayo zungumzwa hapa sio tu ya pesa, bali pia rushwa ya ngono hutumika. Je, Dr Slaa atakuwa na mbinu nyingine tofauti na hii ya sasa (kutumia TAKUKURU)?
2. MGAWANYO WA RASLIMALI, ni vipi Dr Slaa ataweza kuhakikisha raslimali za nchi (wengine wanaita keki ya taifa) zitaweza kugawanywa kwa usawa ili kila mtanzania anufaike nazo?, kwa sasa ndani ya CHADEMA hakuna kitu kinachoitwa mgawanyo sawa wa ruzuku ya chama ilhali pesa hiyo utolewa kwa lengo la kukijenga chama, lakini kuna taarifa kuwa PATO kubwa uishia makao makuu ya CHADEMA kwa matumizi kama kulipana mishahara na kujaziana posho mifukoni.
3. MAPATO YA SERIKALI, kwenye hili la kukusanya mapato ningependa CHADEMA wawe makini, kuna jitihada za kupinga serikali isikusanye mapato kutoka kwa wananchi (ambao wanaitwa walalahoi) na CHADEMA wanatarajia kuwabana wenye makampuni makubwa ili walipe kodi! Je, ni kweli makampuni makubwa yatakuwa tayari kulipa hayo makodi ambayo CHADEMA wamepanga kuyatoza?
Maswali yanaendelea..

Nimefikia uamuzi wa kutoa angalizo hili kwa watanzania wenzangu baada ya kuona kuna kundi kubwa la vijana kwa wazee linapotea kwa kuamini kuwa CHADEMA ndilo tumaini jipya la kuiletea nchi yetu maendelo.
Binafsi siwezi kuwalaumu watanzania kwa kuwa na imani hiyo kwa CHADEMA, na hii ni kutokana na sisi wananchi kukosa taarifa sahihi za kuhusu mwenendo mzima wa CHADEMA, ila kwa kuwa hilo ndilo tatizo, basi leo nawaletea mwarubaini kwa kuweka 'series' ya USANII wa CHADEMA hapa kama ifuatavyo;
CHADEMA KUSUSIA POSHO ZA VIKAO BUNGENI,
Huu usanii uliongozwa na Mbowe kwa kujitangaza kuwa yeye pamoja na wabunge wa chama chake wanapinga vikali posho za vikao, hivyo ili kuonyesha kwa vitendo chuki yao dhidi ya posho wamehamua kususia posho za aina hiyo.
Ila cha kushangaza ni mbunge mmoja tu wa CHADEMA ndiye amendelea na msimamo huo, nae ni Zitto pekee, wengine wote wanaendelea kuvuta posho kama kawaida, na haikuwahi kutokea siku wakaacha kuipokea posho hiyo. Je, huu sio USANII?
MBOWE KURUDISHA GARI LA SERIKALI ILI KUPUNGUZA MATUMIZI,
Huu nao ni mwendelezo wa USANII wa bwana Mbowe, hili la kurudisha gari lilielezwa vizuri na ndugu Mwigulu Nchemba, kwani wengi tulikuwa hatujui kwanini Mbowe alirejesha gari alilopewa awali na serikali.
Ukweli ulikuwa ni kwamba, lile gari la awali alilopewa lilikuwa ni chakavu kwa kuwa lilitumiwa na kiongozi aliyemaliza muda wake, hivyo Mbowe hakupenda vitu vichakavu, akahamua arudishe gari, baadae ndipo akapewa jingine jipya na akalichukua kimya kimya. Gari lenyewe ni hilo hapo chini. Je, huu sio USANII?
View attachment 107638 Hili ndilo gari jipya ambalo Mbowe alikuwa akilihitaji, na alipewa pende tu baada ya kurudisha lile chakavu. Nadhani mnaweza kuona ni jinsi gani anavyo tumika.
DR SLAA ALILIA KUPEWA MSHAHARA WA ZAIDI YA MASLAHI YA WABUNGE,
View attachment 107639
Huyu Dr Slaa amekuwa akijipambanua kuwa yeye ni adui mkubwa wa ANASA na UFISADI, mpaka ikafika hatua akasema yupo tayari kula mihogo ili tu kupunguza matumizi pale Ikulu ikitokea taifa limempa ridhaa ya kuwa rais. Je, una sadiki haya?
Ni huyu huyu Dr Slaa ndiye aliweka masharti kwa CHADEMA kuwa ikitokea ameukosa urais (ingawa alijua fika ataukosa) CHADEMA itamuhakikishia vipi kuwa ataendelea kuyapata maslahi wanayopata wabunge (itakumbukwa alikuwa mbunge, hivyo ilimlazimu auche ili agombee urais). Huu sio USANII na UROHO WA PESA?.
Je, ni mantiki yoyote ya maana kwa Dr Slaa kuweka madai hayo ya maslahi ndipo agombee urais kwa tiketi ya CHADEMA?
DR SLAA ALILIA LAND CRUISER (VX) KAMA GARI LA KUTEMBELEA,
Ni nani asiyejua kuwa CHADEMA wamekuwa wakipiga vita serikali kununua magari ya kifahari (mashangingi)?, ni hawa hawa CHADEMA wamekuwa wakilahumu serikali kuwa inapenda ANASA kwa manunuzi ya magari hayo ya kifahari.
Ila jambo la kusikitisha ni pale nilipo shuhudia kumuona Dr Slaa nae akidai kuwa yeye kama katibu mkuu wa CHADEMA ana stahili kutembelea gari aina ya Landcruiser VX, hivyo chama kigharamie manunuzi ya gari hiyo. Je, Huu sio USANII?
Angalizo: USHABIKI WA KISIASA NI HATARI KWA MAENDELEO YA TAIFA.